Ni mwajiriwa? Fanya haya yafuatayo ufaidike

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,764
92,201
Nimeona leo tuzungumzie suala la kujiriwa na namna ya kuongeza kipato cha ziada kwa njia halali.

Kuajiriwa si dhambi, kuajiriwa si utumwa lakini ajira hio huweza kugeuka na kuwa shubiri kwako kwa nyakati zote za maisha yako, ukajikuta u mtumwa wa ajira, unaishi kwa kukopa na madeni yasiyo na heshima. nimefikiria haya yafuatayo nikaona ni vyema kuwashirikisha, ni mawazo na mtazmo binafsi.

Moja, hakikisha unatunza akiba ndogo hata kama ni shilingi elfu 20 tu kwa mwezi, kisha fikiria kitu kidogo cha kuifanyia pesa hio, kizuri kwa maana ya kwamba kitu ambacho unadhani kitasaidia kuiongeza hio 20 elfu kwa mwezi, fungua genge, weka kijana, au uza maji ya baridi, mwachie dada wa kazi auze barafu pale nyumbani (zingatia usalama) huu ni mfano waweza kuja na wazo jingine.

Jiunge na Saccoss ambazo kwa sasa ziko nyingi sana, kubali kupeleka kiasi kidogo cha pesa kwenye account yako ya saccoss huku ukiwaza kitu kizuri cha kuifanyia akiba hio, sishauri akiba yako uiache benk maana kuna makato ila kwenye saccos/vicoba hakuna makato na kama yapo basi ni madogo sana hivyo una uhakika wa kuikuta pesa yako siku ukiihitaji.

Kwakua umeajiriwa kumbuka kuwa unakopesheka, usikope tena kwa mara ya kwanza ili ujenge nyumba! Ununue gari au ununue fenicha za ndani! Utapotea. labda kama huo mkopo uwe na uwezo wa kununua hio nyumba na kisha uje uitumie kama asset ya kufanyia mambo mengine, baadhi ya mabenki wanakopesha nyumba lakini ownership hubaki kuwa yao hadi siku ukimaliza deni! What if??

Unaweza kubuni mradi mzuri kwako na kwa familia yako ambao hautakua unakugharimu sana usimamizi, washirikishe wana familia wako, kwa mfano ufugaji huweza kukusaidia sana, ule muda wa kila siku wa kukaa Bar (sio wote) unaweza kutumika kwenye banda lako au bustani yako ya matembele na ukajiongezea kipato kidogo

Lakini pia waweza kubuni mradi ambao mtaji utakua ni mkopo utakaochukua, na hapa kwenye kubuni mradi hakikisha unatulia, usianzishe mradi kwa kuwa fulani anafanya hivyo, Mangi ana duka na mimi nafungua duka, anafuga kuku au kware na mimi nafanya hivyo! Utapotea, chukua muda mwingi sana sana kujiridhisha, huenda ikakuchukua hata mwaka au miaka kupata wazo la matakwa yako.

Kumbuka ukifanya mradi au biashara ambayo haipo kwenye interest yako utaishia kuharibu tu, buni wazo ambalo litakufanya kila ukishtuka usingizini au kazini ndio limejaa kichwani, then commit yourself. hakikisha muda wa kazini hauathiri sana miradi yako.

Kisha soma vitabu, makala, angalia videos na sources nyingine za taarifa juu ya kile unachotaka kukifanya ili kujiridhisha kuwa unakiweza, unakipenda na utakifanya, kumbuka hakuna aliyeumbwa kushindwa, ni heri ujaribu ushindwe kuliko usijarbu na uangamie.

FAIDA zake ni hizi

  • Ukiachishwa kazi leo unakua umeshajiandaaa, huanzi kuwa mwanafunzi wa kufanya miradi bali mwalimu
  • Ukizeeka unaweza kuitumia pensheni yako vyema kuendeleza miradi na sio kuanzisha miradi
  • Inakusaidia kiafya kwakua mwili unakua active muda wote, unazunguka huku na kule na siko kukaa mahali pamoja tu
  • inakusaidia kukujengea familia njema na yenye maono mazuri

Kumbuka, it is never too late to try, hakuna atakayekuajiri uwe na kipato kizuri kumshinda yeye (akulipe zaidi)
Kumbuka uwezo wako wa kufikiri ndio mafanikio yako, hakuna mchawi, hakuna elimu mbaya au nzuri hakuna kushindwa kama huamini kwenye kushindwa. Kama wengine wanaweza kwanini sisi tushindwe, angalia kichwani mwako una nini, ondoa dhana ya kwamba sina capital, sina nauli, sina uzoefu sina hiki au kile, jitahidi challenges hizo ziwe opportunities.

Niwatakie siku njema
 
mawazo mazuri sana umenena mkuu
Kuna dada mmoja mzuri tu, anafanya kazi bank fulani ya kigeni hapa nchini, anatembea na machine yake ya Max malipo, anauza umeme na hizo utilities nyingine, kuingizi elfu tano kwa siku ni kubwa sana kuliko kutumia elfu 20 kwa siku.
 
Aksante mpwa kwa somo zuri.

naomba nikurudishe kwenye ile mada ya kachero wa TANAPA, vipi umepata mrejesho wake? umeulinganisha na shutuma zako za mwanzoni?

sorry mpwa kuingiza kitu tofauti, ni kwa sababu natumia simu, ningekuwa na pc ningeenda kule kule
 
Hapo sijakuelewa, unasema mkopo wa kwanza usinunue gari wala kujenga nyumba una maana gani? Kwa mshahara wa laki 6 Bila kukopa ili ujenge au ununue gari utawezaje? We maisha ya mjini hapa si unayajua Mkuu hembu funguka
 
Una haribu mada
 
Mkopo unahitaji kulipwa na usipolipwa mapema basi unakuwa mzigo mwisho wa siku unapelekea kuuza asset zako ili kulipa huo mkopo...

Hence unless unao uhakika kwamba mkopo unauchukua utamaliza nyumba ambayo itakuwa asset au unakopa ili ununue gari la biashara ambalo litaingiza kipato, basi ni vema ukope ili uzalishe (biashara) alafu faida hio uliozalisha ndio itakujengea nyumba na kununulia gari...

Ingawa kuna tofauti kidogo kama unaishi kwa kulipa laki moja kila mwezi ambayo ni milioni moja na laki mbili kwa mwaka basi sio mbaya ukakopa ili kujenga kibanda chako ambacho mwisho wa siku utakuwa una-save hio laki moja kila mwezi
 
Saafi kabisa umeuliza swali zuri, wakati naandika nilichagua sana maneno ya kutumia, na wewe pia umeyaona hayo maneno, nimesema MKOPO WA KWANZA, hua mara nyingi vijana wengi ambao kimsingi hapa ndio nimewalenga, wakianza kazi hua hawajui complications za mikopo! mikopo tena ya mshahara inafilisi, kwahio ningeshauri mkpo huo wa kwanza ambao kimsingi (kwa kutumia mfano huowa laki sita) hutapata zaidi ya milioni sita au saba ambazo hutaweza kujenga nyumba kwa pesa hio, lakini pia ukinunua gari siku za mwanzoni kabisa za kazini jitahidi basi ununue gari ambayo unaweza kuitumia kama source ya income, kwa mfano, miaka ile ya 2000 namfahamu mtu ambaye alinunua gari akawaanaikodisha kwenye sherehe za harusi. kwahio kwa huyu hakuna tatizo, tatizo langu ni kwa yule ambaye ni fresh from college.

Hapo vipi Mkuu?
 
Je malengo ya Graduates wa leo ni nini juu ya maisha yao na maisha ya Nchi yao? Utasikia

  • nikiajiriwa tu nipate Mark X, Verossa, Cooper, Xtrail, BMW,
  • Niwe na demu mkali
  • Nivae nguo na wigi za brand fulani
  • Ninunue simu kali
  • Nipange nyumba kali
  • Jioni nijirushe kidogo
Akifika kazini anakuta hali ni tofauti kabisa na matarajio yake na hivyo huanza kufanya deal ili aweze kufikia malengo yake na hapa ndipo wizi, rushwa na ufisadi hujitokeza. Laiti kama Graduates wetu wangepata ushauri nasaha juu ya huko wamakokwenda baada ya kumaliza vyuo, laiti wangekua wamejengea utayari wa kufungua makampuni, miradi yao kutokana na taaluma zao! laiti haya yangefanyika.......
 
dah!! nimekuelewa sana mkuu Elli na nashukuru sana kwa uzi wako huu,,hakika utawasaidia wengi ambao wataona umuhimu wake
 
Last edited by a moderator:
mada nzuri sana, nilikopaga millioni tano kwa mshara wa laki sita, nikawa nakatwa laki mo na themann mpaka leo naumia, bodaboda niliyonunua ili kufanyizia biashara hadi leo imekufa...
 
Mkopo unahitaji kulipwa na usipolipwa mapema basi unakuwa mzigo mwisho wa siku unapelekea kuuza asset zako ili kulipa huo mkopo...

Hence unless unao uhakika kwamba mkopo unauchukua utamaliza nyumba ambayo itakuwa asset au unakopa ili ununue gari la biashara ambalo litaingiza kipato, basi ni vema ukope ili uzalishe (biashara) alafu faida hio uliozalisha ndio itakujengea nyumba na kununulia gari...

Ingawa kuna tofauti kidogo kama unaishi kwa kulipa laki moja kila mwezi ambayo ni milioni moja na laki mbili kwa mwaka basi sio mbaya ukakopa ili kujenga kibanda chako ambacho mwisho wa siku utakuwa una-save hio laki moja kila mwezi
Asante sana
 
mada nzuri sana, nilikopaga millioni tano kwa mshara wa laki sita, nikawa nakatwa laki mo na themann mpaka leo naumia, bodaboda niliyonunua ili kufanyizia biashara hadi leo imekufa...
Aiseee huwa nawaambia watu kuwa miongoni mwa biashara kichaa ni biashara ya bodaboda. Nilishaweka mawazo yangu na ushuhuda wangu kwenye uzi fulani hapa JF baadhi ya watu walinipinga sana. Nilikua nazo sita yaaani niliiishia kupata bonge la hasara
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom