Ni Mungu pekee ndiye hutoa haki na hukumu ya kweli na si mwanadamu

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
326
250
Nimeamua kuwaelimisha watanzania walio wengi wanaojifanya kujisahaulisha kuhusiana na uwepo wa Mungu

Kwanza naomba nimuonye mgombea wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kauli zake anapoomba kula kwa watanzania akidai atatenda haki.

Pili nimpongeze Dkt. Magufuli kwa kauli zake za kumuogopa Mungu kuwa atawatetea wanyonge na wanaodhulumiwa.

Watanzania nawaomba sana muelewe kwamba haki utolewa na Mungu pekee ila wanadamu tunapeana nafuu kwa sababu unapohubiri kwamba unatenda haki wakati wewe ni wakili ni dhambi kwa Mungu.

Hivi mtu kama Tundu Lissu ameshawatetea waarifu wangapi? na ni kweli hawakufanya hayo makosa au walishinda kwa nguvu hoja nani anajua, katika mahakama za kidunia haki huwezi kupata kwa sababu pale hawanaangalii nafsi ila wanaangalia ushahidi na kama mnavyojua mtu mjanja ndiye ushinda kesi mahakamani, kuna wakati kesi inaitaji ushahidi kama haupo unaachiliwa hata kama umeua kabisa.

Uchawi pia upo ukiona ushahidi unataka kukufunga unaenda kwa mtaalam wa kienyeji anaua mashahidi wote. Haki iko mbinguni, duniani huwezi kutenda haki hasa ukiwa na mamlaka yatatokea matukio ambayo wewe kama Rais huwezi kuwa wakili wa upande wa raia kwa sababu sheria haikuruhusu. Ukishakuwa Rais huo ni muhimili mwingine huwezi ingilia mambo ya mahakama sasa unajiuliza.

Lissu anapata wapi ujasili huo au amesahau.

Watanzania wenzangu kamwe tusikubali kudanganywa kwamba atatenda haki hana uwezo wa kutenda haki kwa sababu haki utolewa na Mungu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom