Ni Mungu pekee ndie mtetezi wa wanyonge, hakuna binadamu aliye mtetezi wa wanyonge tuache kufulu kwenye siasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
habari wadau!

Huu usemi MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI. kwa mfano Kikwete tukimsema mnyonge mnyongeni haki haki mpeni. JK ana unyonge gani?

Nimekwenda kwenye ibada moja ya meneno ya mtumishi wa Mungu aliyohubiri yamenifanya nipanue ubongo wangu na kujua siasa ya sasa inafanya watu wakufuru na kujion wao ndio Mungu kwa maslai ya kisiasa na kuona wao ndio wao bila wao mambo hayaendi.

Mungu ninae mwabudu anazo sifa za utetezi wa wanyonge na toka kuumbwa kwa dunia hakujawai kutokea nabii wala mtume aliyekuwa mtetezi wa wanyonge zaidi ya kutekeleza lile analoagizwa na mara zote huwa linawapendelea watu flani au taifa fulani au kabila flani.

Kwa mfano Mussa alipowatoa wana wa Israel toka Misri (wale watumwa) walikuwa wanyonge na aliyewatoa sio Mussa bali Mungu na hakuna mahala popote Mussa alisema yeye ni mtetezi wa wanyonge.

hapa kwetu tanzania Nyerere hata siku moja sijawai kumsikia akisema yeye ni mtetezi wa wanyonge najua alijua mtetezi wa wanyonge ni Mungu pekee ndio huinua vinyonge na kuvitukuza.

tukumbuke mnyonge sio lazima awe mtu maskini hili neneo linatumika vibaya na kuonekana mnyonge ni mtu maskini. Unyonge unaweza kuwa katika kupata haki, kupata stahili yako, kupata uhuru wako iwe kukutana au kuabudu, unyonge katika kupata huduma zozote ikiwa na unyonge wa kupata haki zote kwa mujibu wa katiba.

je huyu anaye jiita mtetezi wa wanyonge anatoa hayo kulingana na makundi yote kama Mungu anavyotaka au kwa mujibu wa katiba ya nchi?

Je katika hayo haya anayafanya katika kuleta usawa na kuondoa unyonge wa mtu katika kufanya mambo kulingana na sehemu alipo? tukumbuke kuwa tajiri au maskini unyonge uko palepale itategemeana na hali uliyonayo na unahitaji kitu gani ila kwa kuwa wapo wanaotakiwa kufanya kwa upande wao wanashindwa kwa kuwa wanajua huna cha kuwafanya au wanalazimika kutofanya kwa shinikizo fulani.

je vitu hivi anavifanya kwa wanyonge hawa?

1. HAKI- ukiwa mtetezi haki ni kitu cha msingi sana haijalishi anayestahili haki hiyo ni tajiri au mskini. Mungu wetu ni wa haki je huyu anayejiita mtetezi ni kuwafanya matajiri waishi kama mashetani ndio haki? na mtoa haki ni Mungu pekee yeye ni nani awahukumu?
2. UPENDO- Mbona hana dalili za upendo zaidi ya kujenga visasi na uadui baina ya watu huku ubaguzi zaidi ukiwa kichama zaidi kuliko kujali utanzania?
3.

INAENDELEA
 
Kwa imani yako, kwa imani yangu YUPO.
Kinacho matter si imani, kinacho matter ni ukweli.

Na ukweli ni kwamba Mungu huyo hayupo.

Mkiendelea kuamini amini Mungu mtaonewa na hao wanaoonea wanyonge milele.

Wanafurahi kweli wakisikia mnamtaja taja Mungu.

Kwa sababu wanajua mnavyozidi kumtegemea Mungu, ndivyo mnavyozidi kutegemea kitu ambacho hakipo na wao wanavyozidi kupeta.

Jenerali Ulimwengu kagusia hili kwa juu juu wiki hii.
 
Ukisoma ulichokiandika unakiri uwepo wa Mungu naahukuru kwa tutambua uwepo wa Mungu
 
Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana,mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.Waovu na waache njia zao mbaya,watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya;wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia,wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Mawazo yangu si kama mawazo yenu,
wala njia zangu si kama njia zenu.
Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia,
ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu,
na mawazo yangu mbali na mawazo yenu".

Amen
 
Thibitisha kwamba Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom