Ni muhimu vituo vya afya kuweka mazingira salama kwa ajili ya wanawake walio katika hedhi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,544
Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na huduma bora kwa ajili ya wanawake walio katika hedhi katika vituo vya afya. Kwanza kabisa, hedhi ni sehemu ya kawaida ya mwili wa mwanamke na hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa wanawake wanapata huduma bora wanapokuwa katika kipindi hiki. Vituo vingi vya afya nchini hasa vijijini havina mazingira rafiki kwa wanawake kuweza kujihifadhi vyema.

Imekuwa ngumu kwa baadhi ya wanawake kupata mazingira sahihi ya kubadili na kuhifadhi taulo za kike wawapo kwenye baadhi ya vituo vya afya. Hivyo ni muhimu sana serikali ikalitazama jambo hili ili kutunza afya za dada na mama zetu.

Ili kuboresha huduma hizi nashauri serikali ifanye yafuatayo:
  1. Kutoa elimu juu ya afya ya hedhi na jinsi ya kutunza usafi wakati wa hedhi.
  2. Kutoa vifaa vya usafi wa hedhi kama na ikibidi kugawa taulo za kike watakazotumia wakati huu.
  3. Kuwa na mazingira salama na yenye usafi kwa ajili ya wanawake wanaohitaji kubadilisha pedi au taulo wakati wa hedhi.
  4. Kutoa huduma za matibabu kwa wanawake wanaosumbuliwa na tatizo lolote la afya wakati wa hedhi kama vile maumivu ya tumbo, kutokwa damu nyingi au tatizo la endometriosis.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom