Ni muhimu shuleni likafundishwa somo la fedha na biashara kama hali ilivyo huku kitaa

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,133
2,000
Uongo mbaya, shuleni mtu unaweza fika Form Six au chuo lakini kupambana na maisha mtaani mtu wa darasa la saba akakuacha mbali kabisa.

Kama elimu haimfundishi mtu kupambana na maisha yake ina faida gani? Haiingii akilini mtu asome hadi form six miaka 13/14au hadi chuo miaka 16/17 halafu ashindwe kupambana na mazingira yake. Sasa alijifunza nini?

Ni vema elimu yetu ifundishe watu jinsi ya kuishi kwenye mazingira yao. Mambo halisi.

Binafsi ningependa kuona somo la fedha yaani namna ya kutunza, kuwekeza, kupanga bajeti, mikopo, namna ya kuanzisha biashara, biashara ya ku-export, changamoto nk likifundishwa kwa kuzingatia mazingira yetu. Chuo tunafundishwa ujasiriamali lakini ni nadharia zaidi, halikupi vitu sahihi ambavyo mtu utavikuta mtaani.

Ni wakati elimu yetu iwe na vitu practical ndani yake. Vitu ambavyo mtu atavikuta mtaani. Apate elimu itayonuwezesha kuishi mtaani.
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,133
2,000
Ungependa kuona jambo gani la msingi ambalo lipo kwenye mazingira yetu likifundishwa mashuleni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom