Ni Muhimu Sana Kuwajumuisha Watu Wenye Ulemavu Katika Fursa za Ajira

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,794
Ujumuishaji wa watu wenye ulemavu kwenye ajira (3) m.jpg


Watu bilioni moja (takribani asilimia 15 ya idadi ya watu duniani) wana ulemavu na takribani milioni 785 kati yao wana umri wa kufanya kazi.

Kote duniani, watu wenye ulemavu wanakumbana na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira kuliko watu wasio na ulemavu. Wanapoajiriwa, pia wana uwezekano mkubwa wa kuwa na kazi za malipo ya chini na matarajio duni ya kazi kuliko watu wasio na ulemavu.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, 80% ya wenye ulemavu katika baadhi ya nchi duniani wana ukosefu wa ajira huku 20% ya watu maskini zaidi duniani wakiwa na aina fulani ya ulemavu.

Vikwazo katika nyanja nyingine pia imekuwa ni changamoto kubwa inayowakabili. UN inaeleza pia kuwa 80% ya watu wenye ulemavu wanaishi katika nchi zinazoendelea, na 19% ya watu wenye elimu duni wana ulemavu, ikilinganishwa na 11% ya wenye elimu bora.

Vilevile, 90% ya watoto wanaoishi na ulemavu katika nchi zinazoendelea hawako shuleni.

Hata hivyo, Wanawake wenye ulemavu wanatatizwa zaidi katika soko la ajira kutokana na ukweli kwamba mara kwa mara wanabaguliwa kulingana na jinsia zao na hali yao ya ulemavu.

Ukosefu wa fursa sawa za ajira kwa watu wenye ulemavu ni moja ya sababu kuu za umaskini na kutengwa kwa watu wengi wa kundi hili.

Ikilinganishwa na wasio na ulemavu, watu hawa wanakumbana na viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira na kutokuwa na shughuli za kiuchumi na wako katika hatari kubwa ya ukosefu wa ulinzi wa kijamii ambao ni ufunguo wa kupunguza umaskini uliokithiri.

Vikwazo vya ushirikishwaji kamili wa kijamii na kiuchumi wa watu wenye ulemavu ni pamoja na mazingira ya maeneo yasiyofikika na usafiri usafiri usio Rafiki, kutopatikana kwa vifaa na teknolojia saidizi, katika utoaji wa huduma, na chuki ya kibaguzi na unyanyapaa katika jamii.

Mwamko wa kimataifa wa maendeleo yanayojumuisha ulemavu unaendelea kuongezeka. Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) unakuza ujumuishaji kamili wa watu wenye ulemavu katika jamii. CRPD inasisitiza umuhimu wa maendeleo ya kimataifa katika kushughulikia haki za watu wenye ulemavu.

Hata hivyo, ingawa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu inasema kwa uwazi kwamba ulemavu hauwezi kuwa sababu au kigezo cha ukosefu wa upatikanaji wa programu za maendeleo na utambuzi wa haki za binadamu, bado kuna tatizo la kuwaacha nyuma watu wenye ulemavu katika nyanja mabalimbali.

ULEMAVU DUNIANI (3).png

Kila siku wanakumbana na changamoto zinazokwamisha uwezo wao wa kufanya hivyo kuchangia kwa ukosefu wa usawa katika maisha ya jamii zetu. Huu sio tu uvunjifu wa haki zao bali ni hasara kwa jamii. Pia inaleta athari mbaya kwa uchumi kwa kuzingatia thamani ambayo watu hawa wanaweza kuleta kwa taasisi ikiwa wataajiriwa.

Dhana potofu kuhusu kazi na ulemavu zinaendelea kuwepo, ikiwa ni pamoja na dhana potofu kwamba kuajiri watu wenye ulemavu kunaweza kusababisha hasara ya kifedha kwa makampuni na taasisi kwani hutengeneza hofu ya kuwahudumia kimiundombinu.

Mashaka haya si sawa kuwa nayo; ushirikishwaji wa ulemavu una matokeo chanya katika utendaji wa kibiashara na kitaasisi, kwani mara nyingi watu hawa hujikuta katika mazingira yanayochochea kukuza ujuzi wao kama vile uvumilivu, utatuzi wa matatizo, wepesi, fikra bunifu na utayari wa kujaribu mambo mapya ili kuendana na mazingira yanayowazunguka.

Tafiti pia zinaonesha kuwa kuajiri watu wenye ulemavu hufanya sehemu za kazi ziwe shirikishi zaidi na bora kwa kila mtu, na hivyo kujenga mazingira yasiyo na unyanyapaa.

Ulemavu ni suala nyeti na kubwa katika eneo la ushirikishwaji. Waajiri lazima wazingatie mambo mengi wakati wa kuajiri waombaji walemavu, lakini badala yake, ubaguzi hufanyika kwa sababu hawaoni watu wenye ulemavu kama sawa na wao.

Baadhi ya waajiri wana tabia ya kuwaona watu wenye ulemavu kama kundi la watu walio duni, na tunajua kwamba ni mtazamo usio sahihi, na ni wajibu wetu kuwarekebisha.

Kuajiri watu wenye ulemavu katika kampuni pia huleta manufaa ya sifa. Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Baraza la Kitaifa la Biashara na Ulemavu la Marekani (US National Business and Disability Council) uligundua kuwa 78% ya watumiaji watanunua bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni inayowezesha ufikiaji wa watu wenye ulemavu.

Kila mtu, ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu, inabidi kutazamwa na kutendewa kwa usawa, hasa katika ulimwengu wa ajira. Ni kweli kwamba kuna waombaji wengi wa nafasi za ajira wenye elimu ya kutosha na waliohitimu bila mahitaji maalum, lakini watu wenye ulemavu wanaweza pia kutekeleza majukumu yao kuendana na sifa zao.
 
Nikweli kabisa ila walemavu na wao wasitumie ulemavu wao vibaya. Kuna wale wale walemavu wa pale Mtaa wa Congo wanapaki Bajaji wapumbavu sana. Wanautumia ulemavu wao vibaya, hata wakifanya upuuzi wanasingizia kuonewa kwasababu ya ulemavu wao.
 
Back
Top Bottom