Ni muhimu kushindana kwa hoja katika kuidai au kuipinga Katiba Mpya

Rama N Ally

New Member
Jun 8, 2021
2
3
Wanaotaka katiba mpya na wasioitaka wote ni watanzania. Katiba mpya siyo chokochoko wala chanzo Cha uhasama, isiwe chanzo cha machafuko au kupeana majina mabaya kama ya usaliti, adui wa maendeleo, kutumika na ubeberu, udikteta , n.k. Hoja za pande zote ziheshimiwe na kuwekwa mezani.

Ni muhimu kushindana kwa hoja katika kuidai au kuipinga katiba mpya na Wala si kutishana, kuvunjiana heshima au kusagiana kunguni kwa pande zote mbili. Wanaoipinga waje na hoja madhubuti na wanaoidai waje na hoja madhubuti pia.
 
Anaita chokochoko sababu inaenda kuondoa utukufu na kila mtu akafuate sheria na taratibu ndicho hicho hataki huyu maza.
 
Back
Top Bottom