Ni muhimu kufunga ndoa na mtu ambaye wazazi wa pande zote wameridhia

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,563
3,704
Wakuu,

Kuna kisa kimoja kimetokea mwanandoa mmoja(mwanamke) amejinyonga na kumuacha mtoto wa miezi 6. Amejinyonga kutokana na mateso aliyokuwa anayapata kutoka kwa mumewe kupigwa na kusalitiwa lakini sababu kubwa iliyomshindikiza kujinyonga ni kukosa pakwenda, wazazi wake mwanamke hawamtaki mwanaume aliye nae na wazazi wa mwanaume hawamtaki mwanamke aliye nae.

Mwanamke huyo alikuwa katika wakati mgumu pale baba mkwe alitoa maagizo kwa mumewe andike talaka na mwanamke huyo alipojaribu kuondoka na kurudi nyumbani kwa mama yake, Mama yake alisema hamtaki akitaka ampokee akamwache mtoto wa miezi 6 kwa mumewe akajikuta hana pakwenda na alichukua maamuzi ya kujitoa uhai.

Mwanaume yupo matatani mkewe amejinyonga chumbani, baba yake baada ya kupewa taarifa hajajishughulisha na chochote, ameshikiliwa na polisi sijui upande wa mwanamke watasemaje?
 
Nimepitia NA mpaka sasa wazazi hawanielewi wala kushuhulika NA mimi wala kaka au Dada zangu.
Upande wa kike pia hawakunitaka.
Mwanamke nae katumia hiyo kama fursa kunisumbua NA kutaka kunipa madawa.
Hatimaye nimeondoka home nipo maeneo napambana kivyangu.
Hata hamu YA kuoa sina kabisa.
 
Nimepitia NA mpaka sasa wazazi hawanielewi wala kushuhulika NA mimi wala kaka au Dada zangu.
Upande wa kike pia hawakunitaka.
Mwanamke nae katumia hiyo kama fursa kunisumbua NA kutaka kunipa madawa.
Hatimaye nimeondoka home nipo maeneo napambana kivyangu.
Hata hamu YA kuoa sina kabisa.

Anataka kukupa madawa ili iweje, limbwata usimwache au sumu ujifie?
 
Back
Top Bottom