Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,386
Kwa mambo yanayoendelea nchini,ni wazi ombwe la uongozi katika awamu ya Rais Magufuli linaelekea kuwa kubwa mno kuliko ilivyowahi kuwa nyakati za Rais Mwinyi na Jakaya Kikwete;ni wazi CCM na Rais Magufuli hawana uwezo na maarifa ya kuongoza nchi hii tena. Lakini kwa kuwa wanang'ang'ania kutawala, basi ni busara tangu sasa na ifikapo mwaka 2020,wafanye mambo mawili muhimu:
1. Kikwete abaki kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM hadi pale tutakapojiridhisha kuwa nchi hii hatuna uongozi na/ama kiongozi wa kiimla - huyo atatutafuna sote, tunaompinga na hata wale akina Makonda walio tayari kulamba viatu vyake hata viwapo na vumbi.
2. Ikibidi mwaka 2020 wamsaidie "akawinde ndege" huko kwao Chato kwa kuwa naye ameonesha kuwa yuko tayari kwa hilo - ni hatari kuongozwa na Rais anayenung'unika na anayeonesha dhahiri kukata tamaa.
Hebu tufikirie ishu ya sukari, na hebu Watanzania tufikirie ishu ya wanafunzi wa UDOM...kuongozwa na Magufuli kwa miaka 10 itakuwa ni adha kubwa mno kwa taifa