Salam wakuu,
Ni muda wa kujadili yanayotuhusu vijana, nimekaa nakufikiria kuhusu tatizo kubwa la ajira ambalo kwa sasa ni kama janga la kitaifa kwa vijana, wasomi na wasio wasomi nikajaribu kupambanua mambo kadha wa kadha.
Kuna suala moja ambalo mama kila kijana atajaribu kulidadavua kwa jicho la tatu litaondoa kama sio kupunguza tatizo la ajira nchini (unahitajika moyo wa ujasiri)
Suala hilo ni KUJIAJIRI, hili suala sio geni kabisa masikioni mwetu lakini utekelezaji wake unahitaji mambo ya fuatayo;
-Kujitambua
-Kujiamini
-Kuthubutu
Kama kijana unatakiwa kuwa na maarifa ya kukuwezesha kukabiliana na matatizo yanayokuzungua(life skills).
Vijana wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu serikali kutowajali wakati kwa upande wa pili serikali inawategemea vijana kama nguvu kazi ya taifa, kwa hiyo vijana tunatakiwa kuiambia serikali itufanyie nini na sio serikali ituambie tufanye nini.
Tunahitaji kuwa na taifa lenye vijana wenye positive mind, kiasi kwamba serikali itutegemee vijana na sio vijana tuitegemee serikali.
Nina mengi ya kuzungumza lakini nia na madhumuni ya uzi huu ni kutaka kuwasilisha kile nilichojaribu kufikiria kuhus jinsi gani tunaweza kuijenga nchi sisi kama vijana.
Katika eneo ninalotoka nimejaribu kufanya utafiti nikagundua kuwa kuna vijana wengi, wanaojishughulisha na wasiojishughulisha pia, lakini wanaojishughulisha wengi wao wanafanya shughuli za utoaji huduma na sio uzalishaji ambapo kimsingi tunaweza kuingiza kipato kikubwa zaidi endapo tutajikita katika shughuli za uzalishaji.
Kunavijana wengi sana wanahitimu vyuo na kukaa nyumbani kwa muda mrefu pasipo kujishughulisha na kitu chochote huku wakiilaumu serikali.
Binafsi sipendi kuwa miongoni mwao kwasababu nahisi nimeshagundua tatizo liko wapi hivyo naandaa mashambulizi mapema.
Nimekuja na proposal, kutokana na hali ilivyo vijana tunataliwa tufikirie nje ya box jinsi gani tunaweza kutoka katika mfumo uliopo.
Ninawazo la kuanzisha kikundi cha vijana wenye positive mind, self commitment na self awareness, nia tuwe tuna jadili mambo muhimu kuhusu maisha yetu kama vijana, tufikirie jinsi gani tunaweza kutengeneza pesa kutoka katika maeneo tuliyopo.
Sitaki kuamini suala la failure kimaisha maana nahisi kama vijana tukijitambua mapema, si rahisi tufikie umri wa kuitwa baba bila kuwa na mafanikio.
Nina malengo makubwa sana kuhusu organization hiyo kama itafanikiwa kuanzishwa na kupata members wenye sifa tajwa.
Nitaanzisha whatsapp group kwa ajili ya mambo mbalimbali yanayotuhusu.. hope kila kijana mwenye kujielewa atajiunga.
Organization itakuwa ni non-political, itakuwa na non stop movements na mambo makubwa mengi sana,
tumekuwa tukiachwa nyuma Mara kadhaa lakini sio kwamba hatuwezi,ila kuna vitu tunapungukiwa.
Hili ni wazo tu wakuu, kwa maoni na ushauri mnakaribishwa.
Asanteni!