Ni muda wa kufufua wazo la Jenerali Twaha, tuanze kuukomesha usultani wa Dodoma

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Katika Bunge la mwisho wa utawala wa Baba wa Taifa ilizuka hoja ya ukomo wa uraisi. Nina hakika hoja hii ilipenyezwa na yeye mwenyewe ili kulinda Taifa dhidi ya usultani. Mwalimu aliona kuwa Nyerere ni yeye. Mtu mwingine akipewa madaraka yasiyo na ukomo kama yeye anaweza kugeuka sultani. Lakini nakumbuka pia wakati hoja hii ikijadiliwa mbunge mmoja akiitwa Jenerali Twaha Ulimwengu alitoa mawazo yake.

Jenerali alihoji ni vipi rais awekewe ukomo lakini wabunge wasiwekewe ukomo. Akapendekeza kuwa ukomo wa rais ndio uwe pia wa wabunge. Loh! Zogo likazuka huku kuanzia Spika wa wakati ule na ambaye naye alikuwa mbunge wa Ukerewe akipinga. Ikatolewa sababu nyepesi mno. Eti kunatakiwa "continuity". Eti raisi na wabunge wakiondoka kwa pamoja patabaki ombwe la kiutendaji! Hakuna shaka yoyote kuwa wabunge walitaka kujilinda kwa maslahi binafsi tu. Hakuna bunge ambalo wabunge woote watamaliza vipindi viwili kwa pamoja na liwe na wabunge wapya tupu!

Nadhani sasa ni muda wa kufufua wazo la Jenerali japo naye sasa wala halizungumzii. Tumeshaona usultani bungeni. Kuna wabunge Mwalimu aliwaacha na bado ni wabunge. Kuna wabunge Mwinyi aliwaacha na bado ni wagombea 2020. Kama hoja ni katiba si wao ndio walijiwekea kinga kikatiba? Kipindi hiki tumechelewa lakini sasa tuanze kuukomesha huu usultani wa Dodoma.
Kuna faida kubwa mno kuweka ukomo. Chache: kutoa ajira kwa vijana. Kuwapa vijana fursa ya kuongoza na kuleta mawazo mapya. Kupunguza kiburi cha masultani.

THE SULTANS OF DODOMA MUST BE STOPPED NOW
 
Weeee thubutuuu hapo ndo utakua umewagusa kumoyo yani

Wataungana wooote na ndo utajua hawapo kwa maslahi ya mtu masikin
 
Back
Top Bottom