Ni muda sasa wa sisi vijana kuwa makini na huu upotoshaji kabla hatujachukua maamuzi ambayo tutayajutia kesho

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,406
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia na kuona baadhi ya watu wakitushauri vijana kuhusu baadhi ya maswala hasa yanayohusu elimu bila kufanya upembuzi yakinifu au kuwa na data za ku-justify arguments zao. Hoja yao kubwa imekuwa 'zama zimebadilika siku hizi' mara oooh elimu sasa haina nafasi, mara vijana walio mtaani wana mafanikio kuliko graduates n.k.

Yes, nakubali kuwa kuna graduates wengi bado tunasuasua na wengine wamekata tamaa ila binafsi mi naona bado hii sio sababu ya kuwakatisha tamaa au kupuuza nafasi ya elimu. Hii sio sababu ya kusema kuwa kijana aliye mtaani ana unafuu wa maisha kuliko graduates. Faida pekee ya vijana walio mtaani ni kuwa wana experience na mishe mishe au maisha ya mtaa kuliko graduates lakini bado hata graduate anaweza kuexperience na kuadopt mazingira with time.

Sababu za kupuuza elimu au kusema wanafunzi wanapoteza muda kwangu mimi hazina mashiko kwa sababu zifuatazo ambazo nimeziobserve katika mazingira yangu:-

1. Asilimia kubwa ya vijana walio mtaani wana maisha magumu kuliko graduates au wasomi. Strength yao kubwa ni kuwa wana uzoefu na harakati za mtaani kama kubeti, kusaidia mafundi na bodaboda au mishemishe zingine zote za kujitafutia kipato kwa sababu wamekaa mda mrefu ila 'hawana maisha'. 1/10 ya vijana walio mtaani ndio wamefanikiwa bila shule.

kuna watu nimeanza kuwaona mtaani wakipambana toka miaka 15 iliyopita ila hadi leo bado hali zao ziko chini na hawana uhakika wa kipato. Kuna soft arguments zinatumiwa kumpuuza kijana aliye chuo, utasikia mbona diamond hajasoma, mbona mkude hajasoma, mbona shabalala hajasoma ila wanasahau kujiuliza je ni vijana wangapi kati ya ambao hawajasoma wana maisha kama ya tshabalala?..simple answer ni 0.0001%.

Tusiende mbali, hapo hapo ulipo hebu fanya tathmini yako binafsi. Jaribu kulinganisha maisha ya vijana 100 unaowafahamu ambao hwajasoma na maisha ya graduates 100 ambao unawafahamu. Binafsi, kuna graduates wa kuanzia 2013 hadi 2020 ninaowajua wana uhakika wa maisha kuliko vijana walio mtaani tangu 2010.​

2. Under ceteris peribus, kijana aliyesoma ana probability kubwa ya kufanikiwa kuliko ambae hajasoma. Kuna mtu anakaa na cheti chake miaka 8 ila akija kuchomoka unampata kwa tochi..nina mifano mingi mmoja unamhusu dad yangu. Alimaliza chuo since 2014 ila kaajiriwa 2019 tena mshahara mkubwa tu wakati kuna vijana wengi tu walikuwepo mtaani hata kabla ya 2014 ila bado hawana matumaini na kesho zao.

Ni kweli siri ya mafanikio haijulikani ila bado vijana waliosoma wanawapiga gaps sana ambao hwajasoma.. usipuuze thamani ya elimu kwa kulinganisha na vijana ambao hawajasoma kisa wanamiliki bodaboda, genge za matunda au maduka. Hapo bado hawajafanikiwa ila wana unafuu wa maisha na hii ni kutokana na kuuzoea mtaa kitu ambacho hata graduate atazoea na kuadapt.

Faida kubwa ya graduate ni kuwa wanaweza fanya hata kazi za ambao hawajasoma na kusukuma maisha (endapo graduates hatutaona haya) ila kijana ambae hajasoma hawezi fanya kazi za graduates. kuna fursa zingine ambae hajasoma hawezi hata kuzihangaikia ila graduate anakuwa n a advantage.

Kiufupi tusipuuze elimu kisa tu vijana ambao hawajasoma wanamiliki boda boda, wamenunua kiwanja kupitia biashara ya genge. Tuanze kupuuza elimu ikiwa tu asilimia kubwa ya vijana ambao hawajasoma watakuw na uhakika wa walau laki 3 kwa mwezi.

kiufupi, hata mwalimu wa shule ya msingi ana unafuu wa maisha kuliko asilimia kubwa ya hawa vijana wa mtaani ambao tunawaita hustlers na kupuuza elimu.. SAMAHANINI SANA WALIMUU, SIJAMAANISHA KUWADHARAU.

Simple assignment...Chukua graduates 10 wa 2010, halafu chukua vijana waliomaliza form four na kubaki mtaani tangu 2007 halafu linganisha maisha yao..Kuna kitu fulani kinaongezeka kwenye maisha ya graduates..Vijana tusipotoke, na tusimuache elimu aende zake.

wasalaamu.
 
Wenye elimu wanaonekana hawana maana awamu hii tu ika akija kiongoz mwingine mambo yanaweza kubalika tukazane kula mtori nyama tutazikuta chini wadau
 
Kaka mbona una hasira sana hapa ni kila mtu ashinde mechi zake😁
Hahahha hapana..hii ni kama debate na naandika kwa hisia ili tu watu wasihadaike...siku hizi kuna vijana wengi wanataka kuacha chuo ili wakapambane mtaani.
 
Mtoa uzi wewe ni walewale ambao mmeshakuwa Brainwashed. Graduates wengi ni Broke...wanaishi pay cheque to paycheque. Tatizo lenu mnadhani kuwa na kazi kuamka kila siku asubuhi kuelekea ofisini ndio maisha Bora. Vijana wengi graduates wanaishi maisha ya Kitumwa hawako Huru financially. Sababu tatizo ni la watu wengi na wewe ukiwemo basi huwezi kuona.
 
Ukisema watu waliosoma ndo wana nafasi kubwa ya kufanikiwa ni uwongo tu

Ukisema watu wasiosoma ndo wana nafasi kubwa ya kufanikiwa ni uwongo

Ukisema watu fulan muhimu kuliko wengine ni uwongo tu

Dunian mtu ambae anafanikiwa ni mtu ambae haogop kujifinza kitu kipya, Pia haogopi kufeli Haijalish umesoma au ujasomaa
 
what is education! Bora uulize kidhungu mkuu,maana mabeberu walituambiga lugha yetu haijitoshelezi.Mimi mwenyewe kueleza kwa lugha ya kizalendo elimu ni nn mtihani
Elimu nzuri ni inayoambatana na vitendo vyenye matokeo
 
Kwanza mtoa mada nakupongeza kwa kuichokoza Makusudi

Kwani Elimu ni nini?
Inapatikana wapi?
Kusoma ni nini?
Je kusoma ndo kuelimika?

Kwa mtizamo wangu kupata Elimu ya maisha siyo mpaka darasani, hata mtaani kuna watu wamepata elimu ya uvuvi, uashi, ufundi gereji, hata uselemala/Useremala, Kuna watu wamejifunza kutunza bustan, wengine udereva,

U graduate siyo Elimu pekee,

Pia kuna suala la msingi la kutambua kwamba Elimu inayotolewa haiendani na maisha, maana katika andiko lako looote umeongelea kwa wanaotegemea kuajiriwa lakin sikuona ulipotoa Mfano wa aliyejiajiri kwa Elimu yake,

Nakupa mfano mdogo tu ukuenda Mjini Dar es salaam kuna jamaa wengi hawana Elimu ya shuleni ila wana Elimu ya mtaani wanawakopesha mpaka hao graduates

Sibezi Elimu ila tubadili mtalala

Britannica
Doctor (PhD)
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia na kuona baadhi ya watu wakitushauri vijana kuhusu baadhi ya maswala hasa yanayohusu elimu bila kufanya upembuzi yakinifu au kuwa na data za ku-justify arguments zao.. Hoja yao kubwa imekuwa 'zama zimebadilika siku hizi' mara oooh elimu sasa haina nafasi, mara vijana walio mtaani wana mafanikio kuliko graduates n.k.

Yes, nakubali kuwa kuna graduates wengi bado tunasuasua na wengine wamekata tamaa ila binafsi mi naona bado hii sio sababu ya kuwakatisha tamaa au kupuuza nafasi ya elimu. Hii sio sababu ya kusema kuwa kijana aliye mtaani ana unafuu wa maisha kuliko graduates. Faida pekee ya vijana walio mtaani ni kuwa wana experience na mishe mishe au maisha ya mtaa kuliko graduates lakini bado hata graduate anaweza kuexperience na kuadopt mazingira with time.

Sababu za kupuuza elimu au kusema wanafunzi wanapoteza muda kwangu mimi hazina mashiko kwa sababu zifuatazo ambazo nimeziobserve katika mazingira yangu:-

1. Asilimia kubwa ya vijana walio mtaani wana maisha magumu kuliko graduates au wasomi. Strength yao kubwa ni kuwa wana uzoefu na harakati za mtaani kama kubeti, kusaidia mafundi na bodaboda au mishemishe zingine zote za kujitafutia kipato kwa sababu wamekaa mda mrefu ila 'hawana maisha'. 1/10 ya vijana walio mtaani ndio wamefanikiwa bila shule.

kuna watu nimeanza kuwaona mtaani wakipambana toka miaka 15 iliyopita ila hadi leo bado hali zao ziko chini na hawana uhakika wa kipato. Kuna soft arguments zinatumiwa kumpuuza kijana aliye chuo, utasikia mbona diamond hajasoma, mbona mkude hajasoma, mbona shabalala hajasoma ila wanasahau kujiuliza je ni vijana wangapi kati ya ambao hawajasoma wana maisha kama ya tshabalala?..simple answer ni 0.0001%.

Tusiende mbali, hapo hapo ulipo hebu fanya tathmini yako binafsi. Jaribu kulinganisha maisha ya vijana 100 unaowafahamu ambao hwajasoma na maisha ya graduates 100 ambao unawafahamu. Binafsi, kuna graduates wa kuanzia 2013 hadi 2020 ninaowajua wana uhakika wa maisha kuliko vijana walio mtaani tangu 2010.​

2. Under ceteris peribus, kijana aliyesoma ana probability kubwa ya kufanikiwa kuliko ambae hajasoma. Kuna mtu anakaa na cheti chake miaka 8 ila akija kuchomoka unampata kwa tochi..nina mifano mingi mmoja unamhusu dad yangu. Alimaliza chuo since 2014 ila kaajiriwa 2019 tena mshahara mkubwa tu wakati kuna vijana wengi tu walikuwepo mtaani hata kabla ya 2014 ila bado hawana matumaini na kesho zao.

Ni kweli siri ya mafanikio haijulikani ila bado vijana waliosoma wanawapiga gaps sana ambao hwajasoma.. usipuuze thamani ya elimu kwa kulinganisha na vijana ambao hawajasoma kisa wanamiliki bodaboda, genge za matunda au maduka. Hapo bado hawajafanikiwa ila wana unafuu wa maisha na hii ni kutokana na kuuzoea mtaa kitu ambacho hata graduate atazoea na kuadapt.

Faida kubwa ya graduate ni kuwa wanaweza fanya hata kazi za ambao hawajasoma na kusukuma maisha (endapo graduates hatutaona haya) ila kijana ambae hajasoma hawezi fanya kazi za graduates. kuna fursa zingine ambae hajasoma hawezi hata kuzihangaikia ila graduate anakuwa n a advantage.

Kiufupi tusipuuze elimu kisa tu vijana ambao hawajasoma wanamiliki boda boda, wamenunua kiwanja kupitia biashara ya genge. Tuanze kupuuza elimu ikiwa tu asilimia kubwa ya vijana ambao hawajasoma watakuw na uhakika wa walau laki 3 kwa mwezi.

kiufupi, hata mwalimu wa shule ya msingi ana unafuu wa maisha kuliko asilimia kubwa ya hawa vijana wa mtaani ambao tunawaita hustlers na kupuuza elimu.. SAMAHANINI SANA WALIMUU, SIJAMAANISHA KUWADHARAU.

Simple assignment...Chukua graduates 10 wa 2010, halafu chukua vijana waliomaliza form four na kubaki mtaani tangu 2007 halafu linganisha maisha yao..Kuna kitu fulani kinaongezeka kwenye maisha ya graduates..Vijana tusipotoke, na tusimuache elimu aende zake.

wasalaamu.
Hapa mjini anaheshimiwa mwenye pesa tu, tafuta pesa upunguze kujieleza.

Chukuwa Maprofesa wote Tanzania nzima hakuna wa kumfikia Diamond Platnumz ambaye sina hakika hata kama darasa la saba kamaliza.
 
Alimaliza form four....Ila Kuna akina diamond wangapi na kuna maprofesa wangapi....jiulize utapata jibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom