Ni muda sasa wa kuwa na Mihimili miwili ya Serikali

marine 1

Member
Jul 29, 2015
60
67
Maoni huru.

Kwa miaka Zaidi ya sita sasa nimejaribu kufuatilia kwa kina mwenendo wa Serikali na manufaa ya kila sekta kwa nchi na taifa Kwa ujumla.

Kwa utafiti wangu, NaweZa kusema Kwa dhati kabisa kwamba mihimili wa Bunge haulisaidii taifa, na pengine tungeendelea zaidi Kwa kutokuwa na kundi Hilo la wachache wanaotunyonya.

Bunge ndio mihimili wenye watu wengi zaidi na wanaolipwa pesa nyingi. Hata hivyo Bunge limekuwa kituo cha kupitisha Tu yanayoletwa na serikali, na mengine yanapitishwa bila hata wabunge kuyaelewa.

Bunge limekuwa kituo cha mipasho, kujisifu kuwa ni darasa la Saba, kujisifu serikali na Rais na kejeli za hapa na pale.

Tunaweza kubaki na serikali na mahakama. Wawakilishi wetu wawe ni wakuu WA mikoa na wilaya ambao watachaguliwa Kwa Kura katika maeneo husika na mshahara Yao ibaki kuwa hii. Watajumuika kwenye mabaraza ya madiwani kujua changamoto za maeneo yao. Watawakilisha Kwa mawaziri katika Baraza la mawaziri.

Hiyo tutapunguza mzigo wa mshahara Kwa kikundi hichi cha watu wanaojiita wawakilishi WA wananchi ambao kimsingi ni wanyingaji wa wananchi.
 
Kweli kabisa.
Ila nina wasiwasi, panyaroad wataongezeka sana mtaani.
Manaake siasa ndio mtaji mkubwa wa watu wengi. Wanajiita chawa
 
Kweli kabisa.
Ila nina wasiwasi, panyaroad wataongezeka sana mtaani.
Manaake siasa ndio mtaji mkubwa wa watu wengi. Wanajiita chawa
Yaani mipesa waliokuwa nayo ndio waende kuwa panya rd. Hao hata wakifukuzwa wote hawatashuka kiwango hicho,
 
Back
Top Bottom