Ni Muda muafaka wa Upinzani kupigania Katiba Mpya

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
2,431
2,000
Katiba mpya ndo suluhisho Pekee lililobaki kwa Upinzani kuinuka na kuwa Imara zaidi.Lakini bila kudai katiba mpya nchi itazidi kuwa ya Kijani Mpaka Yesu anarudi.

Upinzani waunganishe nguvu zao kwa pamoja kuipigania hii Katiba.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,645
2,000
Hata hivyo kwa ukatili na kiburi walichofanyiwa awamu hii, somo litakua limewaingia. Walitakiwa waweke sharti tangu mwanzo la kususia huu uchaguzi iwapo kusingefanyika marekebisho ya msingi!

Lakini hilo halikufanyika. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019, na ule wa marudio ya wale Wabunge na Madiwani njaa, kauli za kutatanisha na kukatisha tamaa za Rais aliyeko madarakani, Spika wa Bunge, nk.

Vyote hivi vilikua ni viashiria tosha ya kwamba kutakua na maigizo yanayoitwa uchaguzi, lakini hawakutaka kuelewa na kuchukua hatua. Watakua nje ya Bunge sasa. Ni wakati wao sahihi kupigania mabadiliko ya kweli.

Tumerudishwa miaka ya 1960's - 1970's! Hakika ni jambo la kusikitisha sana.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,079
2,000
Tulisema hapa kuwa matokeo yakitoka zitaanza blaa blaa za katiba Mpya sijui Tume huru ya Uchaguzi n.k

Laiti Mbowe na Zitto wangejua kuwa wao binafsi hawatopita basi wangetangaza kususia, sema walidhan wap wangepenya kama alivyokuwa anawapenyeza Kikwete miaka yake yote 10 ya Uongozi
 
Ila kwanini haya yote yawepo hili nadhani ni funzo kwao huu ndo muda sahihi wa kupigania katiba mpya
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
4,494
2,000
Katiba mpya ndo suluhisho Pekee lililobaki kwa Upinzani kuinuka na kuwa Imara zaidi.Lakini bila kudai katiba mpya nchi itazidi kuwa ya Kijani Mpaka Yesu anarudi.

Upinzani waunganishe nguvu zao kwa pamoja kuipigania hii Katiba.
Huu upinzani mfu na katiba wapi na wap
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom