Ni muda muafaka sasa wa opereshi UKUTA

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
wakuu hapa nchini kumekuwa na matukio mengi ya kisiasa yasioyoakisi misingi ya katiba na democracy iliyokuepo na kusimikwa na waasisi wa taifa hili kwa muda mrefu

hapo nyuma vyama vya upinzani vililiona hili na vilianzisha opereshi UKUTA kupinga udikteta unaofanywa hapa nchini lakini operesheni hii haikufanikiwa

Sababu za kutokufanikiwa nahisi operesheni hii kwa wakati ule haikuwa muda sahahi,
kwa sasa naona ndio muda muafaka wa kuanzisha upya opereshi UKUTA ili kuweza kupinga vitendo hivi viovu vilivyokithiri hapa nchini!

Watanzania wazalendo wote kutoka chama tawala na vyama vya upinzani tuungane kwa nguvu zetu zote tuanzishe na kuifanikisha operesheni UKUTA nchi nzima!

Ni dhahiri sasa hakuna atayepona kwa utawala wa namna hii na kuvumilia mpaka 2020 ni kuumizwa na kurudishwa nyuma kimaendeleo, watanzania hatuna furaha ni kwasababu ya maguvu na ubabe unatumiwa na wachache tuliowapa mamlaka watutumikie, kwanini wasitutumikie?

Tuamke sasa twafwaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom