Ni muda muafaka sasa TRA isisumbue watu

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
593
2,037
Msitegemee yule mfanya Biashara aliyekuwa mwadilifu akilipa kodi kwa uzalendo ataendelea tena kuwa mwadilifu ni lazima kwa sasa watu watabadilika tu

Fikiria mfaya biashara anatoa Risiti na analipa kodi vizuri alafu anaweka pesa yake Beniki siku anatoa au kutuma mahali nayo mnailima kodi na tozo, yaani mtu alipe kodi alafu kifaida alichobaki nacho nacho mnakuja tena kumkata Tozo , laizma wafanya biashara waadilifu mtawakera tu

Kama hizi tozo mliziweka kwa ajili ya wale watukutu wasiopenda kulipa kodi basi mfikirie na wale waliokuwa wanatoa risiti na kulipa kodi ipasavyo mtakuwa mmewapa mzigo mkubwa kiasi gani, hili swala la Tozo lilitakiwa lisiingie kwenye mabenki huku ndio mmeharibu kabisa maana ni aibu mfanyakazi anapata mshahara umemkata kodi alafu unakuja kuchota akiba yake kwa kisingizio cha Tozo

Ni muda muafaka sasa Tra watulie maana Kwa sasa kila mtu mnamkata tozo kilazima maana yake kashalipa kodi sasa mambo ya kukamatana huku mtaani na mijini kudai risiti muache sababu kwa sasa mmeamua kila mtu kuingia kwenye account yake anapotoa pesa mnachukua pesa kinguvu kwa kisingizio cha Tozo
 

ThemiOne

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
227
252
Sasa kwa sisi wafanyakazi ni shida zaidi kwani hatuna pakuchomokea .. tunatamani kupokea mshahara dirishani kwa muhasibu ....
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom