Ni muda muafaka sasa kwa serikali kurasimisha sekta ya udalali wa nyumba(real estate/property management)

13 mega pixel

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
7,378
Points
2,000

13 mega pixel

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2013
7,378 2,000
My point, hakuna nchi inayojengwa na watu wa nje, nchi inajengwa na wananchi wenyewe, Tanzania itajengwa na watanzania kupitia kodi, naomba kuorodhesha baadhi ya faida za kulipa kodi kwa mwananchi

1. Uzalendo- kulipa kodi inauma na utataka kujua jasho lako linatumika vipi katika maendeleo ya nchi yako, inakufanya uwe na hisia za umiliki wa nchi yako, utauliza tuu

2. Maendeleo - unapolipa kodi na ikatumika vizuri inakuletea maendeo, zitajengwa shule nzuri, barabara, huduma za maji, afya n.k

3. Ushiriki- inafurahisha pale unapojua kuwa kwa nguvu zako umesaidia kufanya jambo fulani kwa manufaa ya wote

Tatizo

....watanzania utaratibu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi hatukuwa nao, actually kodi zilikuwa zinafichwa fichwa ili kuwafanya watu wa kisiasa wachaguliwe waendelee kuzitafuna peke yao, utawala wa magufuli tunaona mambo yanatendeka...

Wazo langu...

Kuna kodi ambayo serikali inaipoteza bila sababu za msingi, nayo ni withholding tax kwenye rental properties, hasa hizi zilizopo mtaani, namaanisha chumba kimoja ulichopanga, upande au nyumba nzima, kuna kodi tunaikwepa na endapo ingekusanywa na serikali huduma zetu zingeboreka maradufu...

Fikiria, mtu yupo radhi kumlipa dalali kodi ya mwezi mmoja kwa kumtafutia nyumba/mteja wa nyumba lakini anaona ugumu kulipa 10% ya witholding tax kwa serikali

Naishauri serikali, itunge sheria ambayo itamlazimisha mmiliki wa nyumba ambayo ni ya kupangishwa kuwa na real estate agent/management firm ambao(yo) watakuwa wakala wa ukusanyaji wa kodi hii

Kwa namna gani...

1. Nyumba zote za mtaani zinazopangishwa zitambuliwe kuwa zinapangishwa na ni kazi ya mjumbe husika kufuatilia hilo

2. Nyumba zote zinazopangishwa zisajiliwe kuwa zinapangishwa kuanzia kwenye kata, wilaya hadi mkoa

3. Nyumba zote zinazopangishwa lazima ziwe na agent/au firm itakayozisimamia au hata akiwa ni mwenye nyumba mwenyewe lakini ajisajili kama agent wa kukusanya kodi hiyo

Faida ya ushauri wangu

1. Kurasimisha sekta ya udalali, madalali nao wawe ni kada inayotakiwa kulipa kodi ya kipato chao

2. Kuongeza ajira

3. Kukusanya kodi maradufu

4. Kuwaongezea wajumbe wa nyumba 10 majukumu na hata wanaweza kuanza kuingia kweny payroll kama government employees

5. kupata haki, kwa maana ya kwamba hii sheria itakuja na vipengele vitakavyoainisha haki haki za wenye nyumba na wapangaji

n.k

Nawasilisha
 

Forum statistics

Threads 1,392,176
Members 528,565
Posts 34,100,975
Top