Ni muda muafaka sasa kwa sekretariati ya ajira kuhamia Dodoma

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Sekretarieti ya ajira ni chombo muhimu sana katika upatikanaji wa haki katika michako ya ajira kwenye utumishi wa umma, kimepunguza udanganyifu na urasimu wa ajira kwa asilimia kubwa pamoja na kwamba bado kuna loops zinazowabeba watoto wa vigogo katika baadhi ya taasisi zinazolipa vizuri, pamoja na mapungufu machache naipongeza kwa dhati ofisi hii ya ajira kwa kazi nzuri inayofanya. Watoto wengi wa maskini wamepata kazi hapa bila kutoa rushwa wala kujuana na mtu yeyote wa kuwashika mkono Zaidi ya vyeti vyako tu, Hata mimi walinipa ajira japo niliamua kuiacha baada ya kuitumikia kwa miaka kadhaa na kuamua kufanya mambo yangu binafsi, Nakumbuka haikuwa rahisi baada ya kufanyiwa taratibu za usaili na kuniona nafaa miongoni mwa watu tuliokuwa tukishindana nao zaidi ya 800+, huku nafasi zikiwa 5.

makao makuu ya ofisi hii yako Dar es salaam, zamani yalikuwa jengo la maktaba lakini siku hizi nasikia yamehamishiwa kigamboni ( sina uhakika sana kwa hili), kwa kipindi hiki ambacho tatzo la ajira ni kubwa kupita kiasi kwa vijana wa kitanzania na walio wengi wanatoka familia maskini sidhani kama ofisi hizi kubaki nDar es salaam kunawatendea haki, Hapa itawapa unafuu kwa wale wanaoishi au wenye ndugu Dar tu na wengine watakuwa wanatuma maombi tu ikifika kipindi cha usaili wanashindwa kuhudhuria kutoka na ughali wa gharama.

Siungi mkono hoja ya kuwa na ofisi kila kanda maana hii itaongeza udanganyifu na wigo mpana wa kuvuja kwa mitahani ya usaili, ninachoshauri ni mamlaka za ofisi zihamie jiji la DODOMA pale ndo katikati ya Tanzania kuna unafuu wa mtu anaetoka Kigoma,Bukoba,Mwanza,Rukwa,Songwe, Ruvuma, Mara na kila kona ya Tanzania kufika kwa siku moja kuliko Dar ambao baadhi ya watu wanasafiri siku2 ili wafike. Hapa kutakuwa na wigo wa watu kuhudhuria saili kwa wingi kuliko sasa watu wanatuma maombi ya kazi na wakiitwa kwa usaili kama wahusika wanatoka mbali kuhudhuria inakuwa probability kutegemeana na upatikanaji na ukosefu wa nauli.
 
Back
Top Bottom