Ni muda muafaka sasa kwa CCM kukubaliana na Uhalisia ulipo

Umsolopa ganz

Senior Member
Jun 11, 2015
162
39
Watanzani wenzangu,

Tumeshuhudi mengi sana,hasa minyukano,matusi,kuvunjiana heshima,kejeli na mambo ambayo kwa kweli,ukijaribu kuyatafakari utagundua ya kwamba zama zimekwisha badilika,lakini pia ukijaribu kufikiri unajiuliza kwa nini maadili ya kichama yepotea?

Hapo miaka ya nyuma chama chetu chama cha wakulima na wafanyakazi kilikuwa kikitunza heshima,watu waliheshimiana,watu hawakudharauliana,bali sote tulikuwa kitu kimoja!

Imefikia mahala kwa sasa katibu wetu mkuu tunamuomba awe mkali kwa hili la nidhamu hasa hasa miongoni mwa wanachama.

Ni wakati sasa wa kukaa pamoja wana ccm kujitafakari kujipima na kufanya maamuzi yatakayo kidhi kiu ya watanzania wote,mungu amejalia tumepata wagombea wengi tu na wote wanavigezo madhubuti kabisa.

Muda sasa baadhi yao kujitafakari kama wamekidhi vigezo vyote 13 + 1.

Nini maana yangu ya kujumlisha 1.

1 inasimamia kukubalika na watu wa rika zote, Wakulima, Wafanyakazi, NGO'S, Taasisi za dini, nk.
 
Back
Top Bottom