Ni muda muafaka kwa vyama vingine vya upinzani kufuata nyao za CHADEMA

Youngblood

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
18,744
55,442
Kwa Maslahi makubwa ya nchi, napendekeza vyama vingine vya upinzani viungane na maamuzi waliofanya CHADEMA kuacha na huu uchaguzi.

Yani hakuna haja yeyote kushiriki katika huu uchaguzi ambao umejaa rafu nyingi tena zilizo dhahiri kabisa.

Kushiriki ni kupoteza muda wa bure,hakuna kitu kitakachobadirika, jamaa wameamua kushinda,watashinsa tu.

Tena napendekeza ikiwezekana hata uchaguzi mkuu ujao kama mambo yatakwenda kama hivi tususie pia hakuna uchaguzi hapa ni kusumbuana tu.

Ishu ya msingi tupambane tupate katiba mpya,bila hivyo hizi sarakasi haziwezi kuisha mpaka mwisho wa dunia.
 
Wengine acha waje na mawazo mapya tofauti na ya chadema. Tumemiss maandamano na wanasiasa wasasa waoga mno, dunia iko mbali na lazima kelele zinahitajika Sasa.

Kwani Nini kichafuke tu!!!??
 
Ni kweli kabisa Mkuu,siku hizi wanasiasa hasa CHADEMA ambacho ndicho chama kikubwa cha upinzani hawana jipya kabisa,yani wamekuwa waoga kupindukia.
Wengine acha waje na mawazo mapya tofauti na ya chadema. Tumemiss maandamano na wanasiasa wasasa waoga mno, dunia iko mbali na lazima kelele zinahitajika Sasa.

Kwani Nini kichafuke tu!!!??
 
Chadema kishiri uchaguzi kisishiriki hakuna mtanzania mwenye time nao wala hakuna mtu anaeliongolea hilo kabisa ni kama hawajafanya maamuzi yoyote

Nashangaa hiyo nguvu ya umma wanayosema wanayo ni ipi? Au nguvu ya umma ya kuinua chips kwenda mdomoni?

Chadema kimechokwa na wananchi ndio maana hata wananchi hawaoni umuhimu wao nchini
 
Yaani chadema mkosee wenyewe kufuata kanuni alafu muonewe huruma?
Mbona chadema mnadeka hivyo?
*utaratibu*
Kama hujaridhika, kata rufaa!
Huo ndiyo utaratibu siyo kudeka!
Mnadai demokrasia wakati ndani ya chama chenu hakuna!
 
Back
Top Bottom