Ni muda gani mtu hupata mafao yake ya Pension baada ya kustaafu?

Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.
Copy and Paste
Wacha tuisome tu, hakuna namna
 
Na hawa wabunge wetu hawa shida tupu. Wakiipitisha hii utakuwa ni uozo wa karne
 
Ni kwamba taarifa zikipokelewa pale PSPF wanazi scan zinakuwa softcopy zinaingizwa kwenye mfumo wa computer we pale nenda na jina na chek namba.
 
Mzee wangu ali staafu mwaka jana mwezi 7 hadi leo hajalipwa mafao yake, wenye kuyafahamu haya na muda wake mtujuze kama kutuliza mukari tutulize maana mzee amesubiri haelewi lini atalipwa.
Jamaa naona anavizia salio hapo,haaa haaa ,just joking
 
Bill hiyo inaenda kuua wastaafu.
1. Mafao utalipwa 38% na 62% utakuwa unalipwa monthly. Mfano kama ilikuwa ulipwe milioni 100 maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi. Ubaya wa hili siku ukifa malipo kila mwezi hukoma. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.

2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma.

3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu.

4. April 2018 sheria itaanza kutumika.

Kwa ufupi muswada huu utaumiza watumishi wote. Wabunge wetu wasipoliona hili kuwasemea watumishi basi tutaumia.
Copy and Paste
Maelezo yana mapungufu.muswada uko kwenye tovuti na umeweka mambo wazi
 
Mwezi mmoja unatakiwa upate kama kila kitu kilikuwa sawa. Je ulienda kule pspf kupata print out ya mchango wa mwajiri ? Kama kuna gap hulipwi mpaka mwajiri ajaze hizo hela zilizopungua. Sababu nyingine ni kama alishawahi kufanya kazi ya contract halafu aliporudi kazini alianza kazi bila kuandika barua ofisini kwamba mkataba umeisha narudi na ofisi inajibu. Hiyo barua ni muhimu sababu isipokuwepo unaokana hukurudi kwenye rekodi. Kwa ujumla kama kuna gap wizara serikalini wagumu sana kulipa au naona hela inakuwa haipo. Rafiki yangu nae ana kisukari na mkurugenzi boss ni rafiki yake. Alipostaafu akakuta gap lakini mkurugenzi ambaye ni rafiki yake miaka 2 akawa hapeleki Pspf kujazia. Yule mstaafu akatafuta wakili akampelekea samansi. Mkurugenzi alilipa zile pesa na jamaa akapata mafao.

Kwa kesi yako wewe taarifa unazotoa hapa hazitoshi. Tueleze document zilipokelewa. Na kama zimepokelewa utaweza kujua file limekwama wapi.
Mimi nilistaafu miezi 2 ilipita sipati mafao. Kuna dada mmoja alikaa na fail langu 3 weeks. nilifuatilia nikaenda orofa ya sita.Kumbe kuna mhe. mmoja waziri wa makesi kama ya epa haya baada kupigwa chini, walimtoa kazi lakini pesa wakimwachia akafungua benki ambayo anakopesha wafanyakazi na hasa serikalini. Sasa ili kupata wataokopa alicheza tu na maafisa utumishi wengi tukakopa. Sasa nilivyostaafu nikawa bado nadaiwa. kuna fomu unajaza madeni yote. Hivyo yule dada alikaa na lile file sababu nina deni lakini hakuona mkataba wa wizara na hiyo benki. akapata kigugumizi. Nilipofuatilia deni likafutwa nikalipwa. Pale chini ukichukua karatasi ya namba muulize customer care doc au file liko wapi sababu inaonyesha.

Kama kila kitu kiko sawa PSPF hawasumbui. Nilihitaji kuomba mkopo mwanzoni wa 2018 kuongezea mtaaji PSPF wamenipa mkopo mdogo wa 6m ndani ya wiki 2 na sijafuatilia zimeenda docement. Bila kufuatilia hupati. Ile taasisi siku hizi kila kitu kiko mfumo computer.

Naomba uende mwenyewe usiamini sana mambo mengine huenda taarifa zenu haziko sawa.
Yaani umeandika vyema na mtiririko wenye kutia moyo sana.
 
Kwa sasa PSSSF wanajitahidi sana sana kwenye kuwahi.

8 months tu yale malimbikizo (monthly payments) ya hiyo miezi yanaingia then na mzigo wote unafuatia mwezi unaofuata.
 
Acha kuulizia pension!Siku hizi pension kule nchi ya asali na maziwa hutumiwa kujenga SGR!
 
CCM washakomba mihela yote kwenye mifuko ya jamii,CCM ni dubwasha hatari sana kwa afya za wastaafu.
 
Kwa sasa PSSSF wanajitahidi sana sana kwenye kuwahi.

8 months tu yale malimbikizo (monthly payments) ya hiyo miezi yanaingia then na mzigo wote unafuatia mwezi unaofuata.

Hahahah miaka 4 sasa hao psssf wameshindwa kulipa mafao ya watu,wanasema wanasubiri rais asaini.
 
Hahahah miaka 4 sasa hao psssf wameshindwa kulipa mafao ya watu,wanasema wanasubiri rais asaini.
Kwenye kulipa kwa wakati sina shida kabisa nao PSSSF kwa upande wangu na ninawapongeza.

Imechukua just 8 months mzigo akaupata,shida ni mwajiri hakupeleka taarifa sahihi za mstaafu ikiwemo michango kwa mwaka mzima toka apande daraja.

Shida ni utapeli tu unaofanywa na wafanyakazi kitengo cha huduma kwa wateja na kesi iko polisi.

(Wanaigiza ukarimu na kujali wateja huku lengo ni kumpotosha mtu ili wamtapeli)

Miaka minne?? Sasa anaishije huyo mstaafu?
 
Umestaafu 2017,jamaa wanakaa kimya kama hawapo vile huku wewe unahangaika kwenda ofisini kwao kila siku.

Ikifika 2019 Wanachokifanya ni kwamba kama unawadai mil 90,wanakulipa mil 40 awamu ya 1 then wanaanza kukupa ka pension ka kila mwezi huku pesa zako mil 50 zilizobaki wanakupiga danadana wakisema wanasubiri rais asaini pesa zao mpk sasa 2021.

Wastaafu wanaishi maisha ya kukopa kukopa mtaani mara huko platinums,wamekua ombaomba/machokoraa.
 
Back
Top Bottom