Uchaguzi 2020 Ni mtoto tu atakayeweza kuelewa haya yanayoropokwa na wakina Sumaye na genge lake. Msisahau kumchagua Tito Kitarika na Mhere Mwita kwa BAVICHA imara

Nov 27, 2019
27
95
Ni Mbowe huyuhuyu anayenyanyaswa na DC wa Hai?

Ni Mbowe huyuhuyu aliyewekwa ndani zaidi ya miezi 3 bila dhamana?

Ni Mbowe huyuhuyu aliyevunjiwa Bilcanas na kuharibiwa Mashamba?

Ni Mbowe huyuhuyu anayeshtakiwa kwa mauaji ya Akwilina?

Ni Mbowe huyuhuyu ambaye ameua na kutisha Wapinzani wake na haguswi na dola? Dola hii hii ya CCM inayomnyanyasa imeshindwa kutumia tuhuma zote hizo kummaliza?

Kuamini ya Sumaye na wanaosema Mbowe anawatishia na wengine kusema kampiga risasi Tundu Lissu Ni aidha huna Akili kabisa au unatumiwa na Dola/CCM na hicho ndicho anachothibitisha Sumaye. Finished

Tito ni kijana makini sana katika kundi la vijana wa Chadema. Tito ninayemfahamu ni kijana aliyeasisi Chaso mkoa wa Arusha na kuakikisha Chaso inakuwa na nguvu ndani ya Arusha

Ni kijana aliyeshiriki kukijenga chama kupitia chadema ni msingi katika mikoa ya Arusha,Iringa, Manyara na Dar.

Mhere Mwita ni kijana aliyejipambanua katika ujenzi wa chama mkoa wa Mara na kanda ya Serengeti kwa ujumla, amekuwa kijana imara aliyejitoa bila kuogopa mateso ya dola
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,823
2,000
Chekecheo limewekwa sawia hata kuweza kutofautisha kati ya nafaka na pumba. Sindano zinaingia kilio kila kona, ndani ya chama na hata nje ya chama. Cha kushangaza hata msajili wa chama anaonyesha kutokufurahishwa na matokeo. Kulikoni!?
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,102
2,000
Mbowe ana mapungufu yake lakini kwa sumaye hapana sumaye alitakiwa kwanza aseme aliwezaje kuua wapemba mwaka 2001 na kuuza nyumba za serikali wakiwa na mkapa na magufuli kwanin alishndwa kujenga democrasia ccm miaka yote aje ajenge chadema huu ni upumbavu.

Sikubaliani na mbowe kuendelea ila apingwe na watu wenye moral authority na credibility yao isiwe ya kutiliwa mashaka mfano Mnyika, Lissu, Heche Sio under-cover agent and unpredictable leader kama wakina Lowassa, Sumaye na makapi wengine.
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,110
2,000
Demokrasia ndani ya Chedma ilizikwa na hiki kipengele ndani ya katiba ya sasa ya Chadema.

ukomo_wa_uongozi_chadema.jpg
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,516
2,000
Hivi Ccm mna pangia Chadema safu ya uongozi? Yaani naona MNA tamani kama ingewezekana muweke MTU wenu ashindane na Mbowe na ikiwezekana tume ya uchaguzi wasimamie uhesabuji was kura ili muibe kura za Mbowe... Mambo ya aibu kabisa. ..
Chadema wasithubutu kumkata mwambe kwenye Uchaguzi

Nawaonya kwa mara ya mwisho
 

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,499
2,000
Haya mambo magumu ! Kuyaelewa ukiwa nje! Ni sawa na mchezo wowote ule. Commentators huwa wengi ! Na wengi huanzia katikati ya mchezo bila tafakuri ya nyuama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom