Ni msukumo upi unapelekea wimbi la vijana kugombea uongozi kupitia CCM?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni msukumo upi unapelekea wimbi la vijana kugombea uongozi kupitia CCM?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Jul 30, 2010.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Vijana waliojitokeza kugombea nafasi za ubunge na uongozi katika ngazi nyinginezo kwa tiketi ya CCM ni wengi na wanazidi kuongezeka. Wengi wa vijana hawa ni wasomi na wenye shahada za juu kielimu, na baadhi yao wamebahatika kuishi nchi mbalimbali za ng'ambo na kujionea yaliyoko huko.

  Hatua wanazochukua kufanya hivyo ni haki yao na ni jambo la kupongezwa pale ambapo nia na malengo ni maendeleo ya Taifa letu. Lakini kwa kuwa wengi wao ni vijana walio elimika (nakujua vyanzo vya matatizo yetu), inakuwakuwaje wanagombea kupitia CCM? Nasema hivi kwani kitu kimojawapo ninachoamini kuwa ni kikwazo katika kuleta kasi ya maendeleo ya Taifa letu ndani ya mfumo wa vyama vingi ni kutokuwepo kwa uwakilishi wa kutosha wa upinzani, haswa katika ngazi ya ubunge.

  Basi nauliza:

  --- wakiwa ni vijana wasomi, nini kinawafanya waende CCM hali chama hicho kina wabunge wengi tayari tena wanaozidi wapinzani maradufu?

  --- je, hawaamini kuwa kuendeleza upinzani ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu?

  --- ni nini ambacho wanaweza kubadilisha wakiwa ndani ya CCM ambacho imeshindwa kukifanya mpaka leo hii kama chama tawala?

  --- wanahofia nini kuingia upinzani na kuundeleza wakiwa kama vijana wenye lengo la kuendeleza Taifa hili kwa nia njema kabisa huku wakiujenga mfumo wa vyama vingi?

  ---

  Steve Dii
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Vijana wenyewe wengi wanarithishwa mikoba na baba zao, baba zao CCM, sasa unategemea nini ?
   
 3. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mkuu SteveD
  Umeanzisha jambo zuri, si vijana tu, vijana wasomi na hata wa umri wa kati ambao ni wataalamu wa kuweza kuchanganua mambo. Wote wanaenda kugombea kupitia CCM. Wengine wakitokea katika nchi ambazo tunadhani zinafuata demokrasia ya kweli katika kuchagua viongozi.
  Kwa maoni yangu ni kuwa wengi wao wako motivated hasa na matokeo ya wao kupata wanachotaka, si hasa kupigania kubadili au kuondoa uozo uliopo katika uongozi, na hatimaye shida za watanzania. Wengi wanaweka maslahi yao mbele, kwa kuona kuwa ni vyema wakaungana na hao waliopo ili wafanikishe na wao kupata.
  Kwa hiyo utaona hapo ubinafsi, na greedy (nadhani ulafi ndio kiswahili chake) ndio vinawahamasisha.
  Jambo la pili ni kuwa hawajiamini, hii ni kutokana na ukweli kuwa wanajua machinery za CCM zilivyo busy kujaribu kuvuruga kila kitu upinzani unajaribu kufanya kwa nchi hii, kwa hiyo kwa wao kukubalika wanahitaji zaidi machinery hizo hizo, ujasiri wa kupigana wao kwa kuamini kuwa wanaweza kujenga hoja na wananchi wakaelewa hawana.
  Ndio maana kwa maoni yangu, nikiona mtu yeyote ajiitaye msomi na hajawahi kuona kuwa matatizo yetu mengi yamesababishwa na uongozi wa CCM ambao haujali kuboresha maisha ya mtanzania wa kawaida bali ya watu binafsi na familia zao, natilia mashaka kama kweli ana nia ya dhati ya kujaribu kuleta mabadiliko yoyote, na huenda hatafsiri nadharia alizozisoma.
  Ni ukweli kuwa wabunge wa CCM wamekuwa wengi katika Bunge toka upinzani ulipoanza, lakini mchango wao hauonekani si tu kwa kutoa bungeni bali hata kushirikiana na wananchi wao kujaribu kuleta changamoto za kimaendeleo, kwa kuwa wanajua muda wa campaign watanunua wananchi
  Ni haki yao ndio, lakini lazima tuangalie utashi wao ni nini?
  Mpaka wakati huu, kwa siasa za Tanzania zinavyoendeshwa, mimi namheshimu sana mtu anayeamua kwa dhati kuamua kuleta upinzani wa kweli. Licha ya mengi wanayokumbana nayo katika kutekeleza majukumu yao, pamoja na wakati mwingine kuzomewa na wabunge wengi wasikilizaji wa CCM bungeni, wamesimama imara.
  Ni wakati mwafaka sasa kwa wale tuliobahatika kupata elimu, na wengine kuona viongozi katika nchi zingine wanavyowajibika kwa wananchi wao, tujifunge vibwebwe kila mmoja kwa nafasi yake kuleta mabadiliko ya uongozi katika nchi hii. Tunahitaji viongozi ambao wataona kazi ya umma ni utumishi kwa wananchi, na ni heshima ambayo wamepewa na wananchi, hivyo hawapaswi kuichezea.
   
 4. N

  Nyadundwe Senior Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 16, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 45
  "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM" Saint J.K. Nyerere.

  Kwa mfumo wa chama kimoja tulionao Tanzania, tunahitaji nguvu mpya ya vijana hawa ili kusaidiana na majasiri wengine waliopo ndani ya huyo mdudu na kushambulia kutoka ndani. Sipendi kufikiria kwamba nia zao ni kujitafutia umaarufu, utajiri wa haraka kwa njia ya marupurupu na ufisadi... ingawa huo ndiyo ukweli wenyewe!
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nyadundwe

  Ni kigumu unacho ongea wengi wanafungwa midomo wakisimama kwenye ukweli ndani ya CCM,hilo liko wazi mifano iko dhahili kwa nini kijana msomi unaenda huko rudia kusoma MASWALI YA Steve Dii na pia Mpiga filimbi has said it all.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pia usisahau wale wana-bongo flava...:plane:
   
 7. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  njaa ni kitu kibaya sana sasa ukiijumlisha na tamaa ndio unapata huu mtiririko wa watu kufanya ubunge ni kazi na si uongozi.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Most of these young fellas believe in by default and not effort.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hata wakienda huko kwene upinzani, ubunge wenyewe unasaidiaga nini?
   
 10. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Steve, this is an interesting debate.

  Mimi nafikiri kuna sababu kubwa nne zinazowafanya vijana na wasomi wengi kukimbilia CCM. Mosi, siamini kwamba wengi wanaogombea wanasukumwa na haja ya kuleta mabadiliko katika nchi hii. Wengi wa wasomi wanagombea kwa lengo la kuongeza status, kuvizia vyeo na kuwa sehemu ya status quo, ukiachilia mbali swala la kipato. Mambo yote haya hayapatikani upinzani; yanapatikana CCM. In short, siasa zetu hazijajengwa katika falsafa na imani fulani. Ni watu wachache sana ambao wana clear vision and thinking about what they want to achieve through politics. Wengi wetu ni business as usual. Na mimi niwe mbunge, niwe waziri, niwe karibu na fulani, nipate mkopo wa gari, n.k

  Pili, wasomi wengi wa Tanzania ni woga mno na wapo too careful. Sasa woga na kuwa too careful hayaendani na upinzani. They think they have too much to loose.

  Tatu, wasomi wengi na wanasiasa kwa Tanzania wanaitegemea mno serikali kiasi kwamba serikali ikiamua kuwaweka kando ni kama vile ndio mwisho. Hawaoni maisha nje ya serikali-iwe ni wafanyakazi au wafanyabiashara. Na wanafahamu fika kuwa kujihusisha na serikali za upinzani ni kuhatarisha usalama wao kikazi au kibiashara. Utashangaa kwa nini wafanyabiashara nao wanaitegemee serikali. Ni hivi, wafanyabiashara wengi wa bongo wanafanya biashara kwa short cut: wanakwepa kodi, biashara zao hazipo katika viwanja vilivyopimwa, n.k. Kwa kifupi wengi wao hawafuati sheria sawasawa na hawaamini kwamba unaweza ukafanya biashara ikanona ukiwa unafuata sheria. Sasa wanafahamu mara watakapoamua kwenda upinzani, serikali ya ccm itawaangalia kwa makini na hapo ndipo watakapokiona.

  Nne, it seems to me that there are very few Tanzanians who are daring. Watu wengi wanataka wawe sehemu ya mafanikio, lakini sio sehemu ya mapambano ya kutafuta hayo mafanikio. Ndio maana sisi tu wepesi wa kulaumu badala kuchangia. Hatutaki kushiriki kuunda. Tunataka tukute vimeundwa ndio na sisi tuende. Sasa siasa za upinzani zinahitaji ujasiri, kujitoa, n.k. Wengi wetu tunataka tuwe kama wao, tufanye kama wao, tufikiri kama wao. Tunaogopa sana kufanya kitu tofauti. Amini usiamini, siku chama kingine kikashinda, utaona jinsi ambavyo CCM watakuwa disserted. Utaona utitiri wa wagombea kwenye chama hicho kitakachokuwa kimeshinda. Hata hivyo, Mungu bariki, naona tumeanza kubadilika. There are now quite a number of brave men and women, both young and aged, ambao wameamu kujitoa. The situation is now far more encouraging than disappointing.
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nikisoma hayo maelezo hapo juu......halafu natafakari wana JF kama Mwakalinga na Mpoki na wengine..........duuuhh!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  We call those kind of people the "me too" crowd....

  But pheeewww.....your post is deep man! I'm still digesting it. You are definitely a truthfighter.
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Wakuu mlioyasema ni makubwa. Kimsingi roho ya ufisadi inalitafuna taifa vibaya sana, tena kwa kasi mbaya. Wote hao wanalenga kujinufaisha na mfumo fisadi uliopo kwenye CCM na serikali yake. Hakuna mwenye nia njema na uchungu wa kulitumikia taifa.
  Jamani roho ya ufisadi inalitafuna taifa vibaya! Chukulia hata maofisini mwetu, mtu akifanikiwa kuiba anaitwa ati "mjanja"! Huyu jamaa shapu sana mda mfupi tu mambo yake safi! Huyo mwizi na wanaomsifia wote mafisadi. Hata watu wadogo kazini ni wadokozi ile mbaya. Mimi hufikiria na kujiuliza, hili taifa tunaelekea wapi....hardly unapata mtu mwaminifu katika kila sekta!
  Kwa kuwa CCM ni chama cha ulaji....kila mtu anakimbilia huko kupata ulaji.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nadhani kuwa msomi ni pamoja na kutumia elimu au ujuzi wako kikamilifu kusaidia jamii. Ukiangalia the so-called wasomi ambao kweli wana-contribute something to the society in pro bono au non-distructive ways to the nation, utagundua bongo hakuna wasomi, kama wapo ni wa kuhesabu. Waliopo wanafanya kazi kwa mfumo wa stripper au changudoa, hafanyi kazi mpaka aone channel ya mshiko.. wachumia tumboni. Wachumia tumboni hawa wenye mavyeti, wanawa-encourage hata wengine kupata degree za kununua au feki.

  Unakutana na mtu anayejiita profesa, lakini hana hata website, au last time alipo-contribute academically ni more than umri wa mtoto wa form 4. Ni mfumo wa kibazazi tunaoulea wa kutaka kuvuna bila kwenda shambani ndio ulipotufikisha hapa. People have to quit politics and instill discipline of contributing something to our economy. Tz haihitaji mtu wa kututafsiria au kufanya ukalimani wa matatizo ya wananchi, kule Dodoma huku akila posho za summer camping. Tunahitaji watu wazalishe, waende moja kwa moja jkwene shughuli zinazohusiana na maendeleo.SIASA HAPANA. Tena hawa wenye mavyeti walitakiwa waongoze msafara, sio kukaa nyuma. Nahodha wa jahazi hukaa mbele. Period.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wengi njaa tu inawaahangaisha....
  Zamani enzi za neema za mzee ruksa...
  Watu walikuwa hawana interest na siasa..
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Historia inaonesha kuwa ukombozi wa nchi nyingi za afrika haukuletwa na wasomi wengi. Ni wasomi wachache tu waliokuwa chachu ya mabadiliko na waliungwa mkono na wananchi wengi ambao hawakuwa wasomi. Wasomi wengi walikuwa wameridhika na hali halisi kwani usomi wao uliwawezesha kupata pesa za kula wao na familia zao. Na wengi walikuwa busy kuwapendezesha watawala ili wapate ujira wao.

  Hata sasa hali ni ileile kwamba wasomi wengi wanaojiunga na chama tawala tayari wananufaika na hali ilivyo sasa. Wanachofanya sasa ni "kujiposition" ili waneemeke zaidi. Inawezekana kuna wengine wana nia ya kweli ya ukombozi wa nchi lakini kwa ambao nimeongea nao na ambao ninawafahamu siku nyingi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa wanaingia CCM kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya chama.
   
 17. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  vijana wengi wenye elimu ya juu wana uchu wa maendeleo ya kifedha zaidi,fikra za kimapinduzi kwao hazipo,
   
 18. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kitila Mkumbo
  kalijibu swali thoroughly inside out. Mimi naona hakuna true revolutionaries ndani ya CCM. To be a true rev lazma ukubali kuweka kila kitu chako rehani kwa maslahi ya ukombozi wa taifa. Wangapi wako tayari? Ninauhakika naweza wahesabu kwa vidole vyangu.
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimejaribu kuongea na wengi ambao ama wanagombea au wanaunga mkono CCM. Wao wanasema hivi.
  1. Ni rahisi kushinda ukiwa CCM (bila kujali utafanya nini baadaye au uajiunga na kambi ipi huko Bungeni).
  2. Upinzani ni kama haupo (bila kujali kama wao wangesaidia kuwepo kwa huo upinzani)
  3. Hata ukishinda kupitia upinzani haupewi hadhi (na serikali) kama mbunge wa CCM
  4. Unapoteza opportunities nyingi za biashara na uwakilishi kwenye vyombo mbali mbali (hasa hasa bodi za mashirika ya umma tena yale yenye pesa nyingi) ukiwa upinzani.

  Kwa maoni yangu,
  1. Watu hao ni wajasiriamali kama machinga na wengine. Lazima wawekeze mahali ambapo faida ni kubwa sana kwa mtaji mdogo unaowekeza (very high return on investment) na pia hawati sehemu yenye high risk.
  2. Hawana mpango wowote katika akili zao wa kuleta mabadiliko katika jamii na kuwasaidia wananchi. Hao wananchi wanawafanya kama nyenzo zao za kuzalisha mali kwa kuwatumia katika huo uwekezaji wa kisiasa.
  3. Kwao maisha mazuri ni utajiri wao na manufaa kwa familia zao tu. Hawajui kuwa maendeleo ya namna hiyo ni hatari na yanasababisha upotevu wa amani. Hawajui kwa nini nyumba nyingi zina mageti kama magereza.
  4. Wako tayari kufanya lolote hata kuuza nchi au wananchi (kama wale waliouza watumwa) ili mambo yao yaende. Zao la ufisadi lazima lidumu katika ufisadi.
   
 20. C

  Chesty JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,353
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Jambo kubwa sana ambalo limepelekea hayo yote yaliyotajwa hapo juu ni strategy mbaya sana ambayo CCM wameifanya ya kufifisha dola, kumaliza uwezo wake wa kutenda independently, kutekeleza sheria zake na hivyo kuseparate itself from the party system.
  Hiyo maana yake ni nini, ukiwa kiongozi ndani ya CCM basi hakuna nguvu ya dola itakayo kugusa mara utakapokwenda kinyume na sheria mfano wizi wa mali ya uma, rushwa n.k.
  Sasa ukichukulia kwamba baadhi ya wasomi wanauchu na utajiri wa shortcut the likelihood is tutaona wengi wanakimbilia CCM.
   
Loading...