Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,316
- 8,227
Mada: Ni mradi upi ungerudisha mtaji wa uwekezaji kwa TPDC kwa haraka zaidi
Habari za leo wa kuu,
Mimi ni kijana wenu, leo nimekuja na mada hii yenye tija kwa taifa.
Taifa letu linayo gesi asilia ambayo, ina matumizi mengi
1. Gesi asilia inatumika kupikia majumbani
2. Gesi asilia inatumika kutengenezea mbolea zinazotumika kwenye kilimo. Mbolea zote tunazo agiza nje ya nchi zinatengenezwa kwa kutumia gesi asilia.
Sitaweza kuelezea kanuni zinatumika hapa ila ukitaka kujua zaidi waweza kuni PM kwasababu hivi ndio vitu navyo shinda navyo.
3. Lakini pia gesi asilia inatumika kutengenezea mafuta safi ya petrol na diesel ukiachana na haya yanayopatika kwa kuitenganisha mafuta ghafi.
4. N. k
Kwa analysis za kiuchumi nilizo fanya, Miradi miwili huo wa kutengeneza mbolea na wa kusambaza gesi majumbani inaweza kufanywa na serikali yetu bila kushirikiana na kampuni za nje (Joint venture ama sharing agreement).
Nimezungumza hivi ili niitoe Liquified Natural Gas Project (LNG) ambao ni mradi wenye tija zaidi ila unahitaji mtaji mkubwa kuwekeza. Hivyo lazima serikali ishirikiane na kampuni za nje ili kuwekeza mradi huu.
Basi nikirudi kwenye maada tajwa pale juu. Wote tunajua idadi ya watu Tanzania inayo weza kumudu kununua gesi asilia ni kubwa. Tatizo linalo kuja gesi asilia inahitaji uwekezaji mkubwa wa bomba za kuwasambazia wateja waliopo mikoani. Hivyo basi swala hilo kiukweli huchukua muda kujenga miundo mbinu ya kusafirishia hiyo gesi.
Kwenye swala la mbolea, nako pia wote tunajua kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu na mtanzania yeyote yule hata maskini anajua kwamba ili aweze kulima kilimo Bora kitacho mpatia mazao mengi na Bora anahitaji mbolea. Hivyo mbolea inatumika mahali pote Tanzania, hata watu maskini kabisa nao pia hutumia mbolea.
Hivyo mbolea ikitengenezwa Tanzania ninao uhakika kwamba itaweza kununuliwa na asilimia kubwa ya Watanzania.
Faida moja kubwa ya kuwa na kiwanda cha kutengeneza mbolea Tanzania
1. Tutaondoa adhaa ya kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi, hii inasaidia kupanda kwa uchumi wa nchi
2. Zipo faida nyingi ila mimi nime egemea kwenye hiyo ya kwanza.
Swali:
1. Je, ni mradi upi wenye tija ya haraka kwa serikali na wananchi?
2. Ni mradi upi ungerudisha mtaji wa uwekezaji kwa TPDC kwa haraka zaidi
Msisahau kwamba Miradi mingi ya mafuta na gesi huchukua muda mrefu sana kuanza kuleta faida. Hivyo ili urudishe gharama ulizo tumia kuwekeza inabidi uwe na soko imara na la uhakika.
Ni mimi: Meneja wa makampuni
Elimu: Bachelor of Science in Oil and Gas Chemistry
University: Aberdeen University