Ni mradi gani au ndoto gani ambayo uliumia sana sababu haikufanikiwa? Ipi imefanikiwa na kukupa furaha sana?

DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
1,654
3,327
Hello JF family,

Kwangu binafsi mradi ulioniumiza sana niliufanya nikiwa na miaka 16 wa kufuga kuku. Nilijenga kibanda nikaanza na kuku wawili. Nikawaendeleza hadi wakafika 25. Nikatumwa na mama sokoni siku moja nikaona kuku bei nafuu sana nikamnunua, lakini kumbe alikuwa mgonjwa. Akaja kuambukiza kuku wote 25 wakafa.

Nilijifunza somo lakini kwa hasara na maumivu makubwa ukizingatia kwetu tulikuwa maskini na baba alishafariki na nilikuwa nategemea sana hao kuku wanisaidie. Mradi ulionifurahisha sana ulipofanikiwa ni ujenzi wa nyumba binafsi na ya biashara.

Mungu ni mwema.
 
Nilikuwa na duka la simu nadhani ni maduka ya mwanzo kabisa kuwa mtaani maaana zamani simu zilikuwa zinauzwa k/koo tu.
Basi Asubuhi moja kijana wa kazi akaludi analia akinitaarifu kuwa duka lote wameiba na Mlinzi yuko hoi hajitambui.
Nikajipamoyo nika biresha nakaendelea na biashara na kilicho saidia nilikua na Biashara nyingine tofauti na simu.
Vinginevyo sijui ingekuwaje maaana walisafisha waliacha makava tu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
masagati,
Asante sana Masagati kutuambia lililotokea. Pole sana ndugu yetu kwa hilo. Mungu ni mwema ulikuwa na biashara nyingine. Kwa kweli Tanzania yetu wizi unarudisha sana watu nyuma. Kuna watu majizi kweli kweli na ndio hao wengine wakikamatwa wanachomwa moto kabisa japo naona siki hizi hayo matukio yamepungua. Mara nyingine wafanyakazi unakuta wanakuibia. Hata marafiki au ndugu pia. Ni jambo la kusikitisha. Na ukienda polisi hawakusaidii. Ni kuji-protect pale inapowezekana. Lakini mara nyingine hata uweke ma-grille mazito je bado wanaweza kukuvamia. Na nchi yetu sijui kama insurance/ bima za biashara za kufidia wizi zipo kweli za bei nzuri na ambazo zitafidia kila kitu. Nilishaibiwa simu ya iPhone. Nikaizima kwa cloud na kutuma ujumbe wairudishe ila hakuna aliyefanya hivyo. Baadaye najua waliifanya spea tu. Yani afadhali auze kwa buku kadhaa spea kuliko akurudishie (Niliahidi reward ya 100k) ila wapi. Mungu na atusaidie.
 
Nilipata idea ya kutengeneza sausage za kitimoto na beef ...nikapitia hatua zote....!...nikapata mafunzo kwa masister fulan hv wantengeneza sausge nzuri san zina ladha nikagharamika mafundisho!..
Later nikaagiza machine china, ..ss nikawa nimekubaliana na kijana anayetengeneza/aliyenifundisha zile sausage kuwa tufanye robbying aje kwangu...ila mlinzi yule wa pale kwa masister akaniambia dogo amefundishwa arts nyingi sn za kuchez na nyama na wa italiano lakini ni MVIVU sn hpend kujituma! So kuwa makini....kufupish stry nikapewa abc na sido kuwa na frem 3!(moja ya kuweke materials..nyinginr ya production na nyinginr kuhifadhia hzo sausge Nikapata nikalipa...! Nilimsubiri yule kaka zaidi ya kusema usubiri...hakutokea ..nikawa nimekula hasara tu...
Limashine lipo tu home😏!

Mishe nilizonazo ss hv alihamdulilah kila nikigusa panafunguka ingawa chngamoto ni mob!
 
Pole sana kijana alikuangusha. Ni kweli kuna vijana wavivu sana. Yani wengine ndio hivyo sio waaminifu na wengine wavivu. Mungu na akupatie mtu mchapa kazi unayeendana naye. Asante kwa ushuhuda wako.
 
Yaan yule kaka Mungu akamguse tu akili yake ..alipelekwa italy kusomea mpishi akaspeciliaze kw aitalian foods ww nkbidhi nyama alafu ondok yaan anajua mno mno mapishi y nyama..kinifundisha vingi sn hd hizo jibini (cheese) uwii likapew machine likauza kwa bei ya hasara!.asante san mkuu..ni fursa nzuri san kule songea pia kuna masister wanatngeneza sausage nzur san san sana!...bs tu !
 
Inasikitisha mtu ana uwezo sana na utaalamu na kipaji, lakini hakimsaidii yeye wala jamii hainufaiki. Kweli wahenga walivyosema kwenye miti hakuna wajenzi. Basi tujitahidi sisi binafsi kama kuna miti, basi tujenge. Manake tuchangamkie fursa zinazotujia kwa asilimia zote. Mungu akutangulie my friend katika shughuli zako zote za ujasiriamali.
 
Amen amen mkuu!
 
Back
Top Bottom