Ni mpambano kati ya CCM yenye kujenga uchumi shirikishi wa dola dhidi ya upinzani unaoshadadia soko holela katika huduma za kijamii

Oct 6, 2020
27
50
Kuanzia tarehe 28/08/2020 vyama vyama siasa nchini vilianza mikutano ya ufunguzi wa kampeni zake za kunadi wagombea Urais na ilani zitakozowaongoza katika kuwashawishi wapiga kura. Chama kilichoanza ni Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CDM) kilichoanzia mbio zake huko Mbagala Zakheim. Siku moja baadae, yaani tarehe 29/08/2020, Chama Cha Mapinduzi kilizundua kampeni zake huko Jijini Dodoma. Na tarehe 31/08/2020 Chama Cha ACT-Wazalendo kilizindua ilani yake Jijini Dar es Salaam, katika Hotel ya Protea. Mpaka sasa vyama hivi vinavyoonesha ushindani wa kutaka kuchukua dola; kwa CCM kumsimamisha mgombea wake anayemaliza awamu yake ya kwanza ya uongozi, Dkt. John Joseph Magufuli; CHADEMA wamemsimisha Antipas Tundu Lissu; na ACT-Wazalendo wamemsimamisha Bernard Camillius Membe.

Uzinduzi wa ilani hizi za vyama vitatu vinavyoonesha ushindani unatupa mwanya wa kufanya tafakuri na uchambuzi wa itikadi zinazoongoza ilani hizo na athari zake katika kustawisha jamii katika upatikanaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji, makazi n.k. Katika kufanikisha hilo uchambuzi huu utaanza na kuainisha falsafa kuu za mtazamo kuhusu uchumi ambazao zinatoa nafasi ya kuona namna gani fikra za uchumi-siasa zitakavyoathiri sekta nyingine wanazoainisha katika ilani zao. Na maswali ya muhimu katika kufanya uchambuzi huu ni namna gani ilani inajikita katika kuondoa fikra na uchumi tegemezi; kwa namna gani suala la umasikini wa kitabaka na ujengaji wa uchumi kutoka chini unazingatiwa katika kuboresha ustawi wa watu masikini. Na jambo kubwa la msingi pia ni hoja inayoibuka ya je, ni maendeleo ya vitu au watu? na uhusiano wake katika huduma za kijamii.

04.JPG

Kabla ya kwenda katika maeneo husika ya huduma ya kijamii. Ni vema kutoa kwa muhtasari fikra kuu zinazoongoza ilani za vyama vya CCM, CHADEMA na ACT kama zilivyonishwa na vyama ndani ya ilani zao na pia kwa kupitia hotuba zao za uzinduzi. Hii itatusaidia kulinganisha msukumo wa mawazo yao na namna wanavyotamani kuboresha huduma za jamii. Sehemu inayofuata hapa chini inatupitisha katika mawazo makuu yanayoongoza mtazamo wa vyama hivyo.

Kupitia mgombea wake, CCM imeweka bayana msimamo wake wa kujenga uchumi wa kitaifa unaomilikiwa na wanatanzania wenyewe wanaosukumwa na uzalendo. Katika hili, inasitizwa kuwa msukumo mkubwa ujikite katika kubadilisha maisha ili walio wengi ambao ni wanyonge washiriki katika uchumi huu kwa lengo la kuondoa unyonge na tofauti za matabaka. Na msukumo huu wa mabadiliko unaonekana katika mtazamo mkuu na lengo pana la “Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi”. Na vipaumbele vya ilani vinavyoanishwa vinaakisi kimantiki na kimkakati mtazamo huu mpana wa uchumi, siasa na huduma za kijamii zinazoendelea na kuwashawishi wapiga kula kuwa sehemu ya umiliki wa mambo yao wenyewe kama taifa huru.

images-2.jpeg

Kwa umuhimu kabisa, tunaona ubunifu unajikita katika kutengeneza muunganiko wa uchumi wa kitaifa unaokumbatia mshikamano wa kijamii/ujamaa unaoboreshwa ili kwenda sambamba na ubepari wa kidola na maarifa yanayotokana na mazingira na mahitaji ya Tanzania. Kwa kifupi, tunaona msukumo wa kujenga “ubepari wa kidola-ushiriki jumuishi-maarifa bunifu” kama silaha ya kujenga Tanzania mpya. Na mawazo ya CCM yanaonekana yakisukumwa na hitaji la falsafa jamii shirikishi na kujitegemea. Ilani inatoa msukumo kwa dola/serikali kuendesha kuwekeza kwenye njia za kuendesha uchumi kwa ajili ya kuwekeza kwenye huduma za kijamii, yaani kufifisha nguvu ya soko linaloonekana kutokuwa na haki katika kustawisha jamii wakati huo dola kuwa na nguvu kwa niaba ya wananchi katika kuboresha maisha ya raia wake.

Katika hili tunaona CCM inaendelea kujenga uchumi sambabamba na mapinduzi ya kubomoa unyongonefu ya fikra za sisi ni wanyonge na wasio stahiki kuendesha mambo yetu wenyewe. Katika hili mgombea wa CCM anaendelea kuwajengea imani chanya watanzania kuwa kwa umoja wao wataweza kufanya makubwa. Na kuthibitisha hilo, katika hotuba anasema “tukiamua tunaweza” na kusititiza kauli yake ya kila mara kuwa “Tanzania ni nchi tajiri”. Kuendelelea kuchochea mabadiliko hapa tunaona CCM inatambua kuwa mapinduzi ya uchumi wa kweli hayawezekani bila kuleta mapinduzi ya fikra ambayo kwa pamoja tokea ukoloni na ukoloni mamboleo katika Africa na nchi nyingine zilizotawaliwa, watu walifanywa tegemezi na kujiona dhaifu dhidi ya wakoloni wanaonekana kuhodhi ufunguo wa ustaarabu na ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na ki-maarifa.

Kwa upande wa CDM mtazamo wao unajengwa katika mtazamo wa haki ya kiliberali unaomchukulia mtu na kumtenganisha na jamii. Pia mtazamo huu unaamini katika haki ya soko lisilodhibitiwa kwa kudhani kuwa soko linaweza kuwa na utashi wa kipekee bila msukumo, wa kuleta haki ya mtu mmoja na jamii. Falsafa hii, pengine kutokana na historia ya mgombea wa CDM kuwa mwanasheria, inaipa ukuu sheria na soko katika kukabili mienendo ya watu na maisha yao. Kwenye uzinduzi wake, na kama ilivyoanishwa katika ilani yake inasititiza kutengeneza “soko huru” na linaloongozwa na sekta binafsi. Katika mtazamo huu, tunaona msisitizo zaidi upo kwenye haki za mtu binafsi/individual rights na kunyamazishwa kwa haki za msingi za kijamii/social rights.

Katika kuhuwisha mtazamo wao wa kisheria, kile wanachokiita welekeo wa kutengeneza maendeleo ya watu na siyo vitu, yanashadadia soko kama na sekta binafisi, hapa kimsingi wanazungumzia haki ya mtu mwenye uwezo wa kushindana katika soko kumiliki mali na maarifa alindwe kisheria. Umiliki “jumuishi/collective ownership au commons ownership” unaonekana kama kikwazo kikubwa katika haki ya mtu mmoja mwenye nguvu ya kisheria hata kama zinakidhana na maslahi mapana ya haki za kijamii. Tutakuja kuona hata viupaumbele vya kuboresha huduma za kijamii vinalenga katika kupanua wigo wa ubidhaishaji/commodification huduma kupitia kile wanachokiita ubia na sekta binafsi kama kitu muhimu chenye kugawa kwa usawa, huduma kupitia nguvu ya soko ambapo kuna muuzaji na mnunuzi.

TAN19.jpg

Ubinafsi/individualism na uwajibikaji wa mtu mwenyewe kupitia uwezo wake wa kushindana kwenye soko bila uthibiti kwa hoja kwamba sheria na soko wakati wote vina tabia ya kutenda haki imesisitizwa sana. Kanuni za jabari wa mwituni na uthabiti wa simba wa nyika, wa mwenye nguvu mpishe ndio maono ya upinzani. Kilichofichika hapa, ni jambo la muhimu la kuwa washindani wanaoingia kwenye soko hawana nguvu sawa za kupambana. Mapambano ya soko mara nyingi ni kati ya vita ya Daudi na Goliath. Wenye nguvu ya mtaji na kumiliki soko ndio hao wenye nguvu ya kuchezesha sheria zilalie upande na maslahi yao. Na nadhani mgombea wao analitambua hilo, ndio mara kwa mara Tanzania ilivyokuwa inajaribu kutafuta haki katika kulinda rasilimali zake dhidi ya mataifa makubwa alisikika akisema “tutanyolewa kwa kipande cha chupa na bila maji”. Lengo hapa lilikuwa ni kuwatia watu na serikali hofu wasilinde rasilimali za nchi dhidi ya wanyonyaji.

Vivyo hivyo, chama cha ACT, pengine kutoka na kuhodhiwa na kiongozi aliyosoma uchumi, mawazo yanayotawala sehemu kubwa yanaakisi taaluma binafsi ya kiongozi mkuu wa chama, mwanauchumi Zitto Kabwe. Kwake pia anachanganya nadharia za sheria za ki-unaharakati, kama ilivyo kwa CDM zimejengwa katika haki za kiliberali za maslahi binafsi. Kupitia muhtasari wa ilani yake uliotolewa pale Protea Hotel, tarehe 31/08/2020, tunaona bayana msisitizo wa kuacha soko huru na kukaribisha wenye mitaji kutoka nje kuhodhi maeneo ya kimkakati ya kiuchumi.

Pengine, uzinduzi wao wa Ilani kufanyika Hotel ya Nyota tano unasukuma itakadi yao ya “kula bata”/kuponda mali na dhana ya ushiriki wa wananchi wa kawaida wakati walengwa wakuu hasa masikini vijijini na mtaani wakiachwa kando. Na jambo lingine linadhihirika katika nadharia za kiuchumi zilizochukuliwa na kupachikwa kutoka Magharibi ni kutaka kusisitiza utegemezi wa kutegemea uzalishaji wa nguvu za nishati/fossil fuels ambavyo vimepigiwa kelele kuharibu mazingira ambao kwa kiasi kikubwa nchi masikini na watu wake wamekuwa waanga wa kupoza athari zinazozalishwa Ulaya kupitia nishati hizi kwa kupewa kiasi kidogo cha fidia kupitia miradi ya “ukaa hewa”/carbon forestry.

Tunaona ushiriki wa kuua nishati mbadala na rafiki za nishati kama vile Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji kwa kutumia “wataalam wa nje” na wanaendelea kusema “kuhusu namna bora ya kutekeleza miradi mikubwa kwa ubia kati ya Sekta Binafsi. Fikra tegemezi na kufifisha uwezo wa kujitegemea unajionesha waziwazi. Na kasumba hii ya kuona maarifa ya ndani na fikra inayoheshimisha mawazo ya kimapinduzi, imekuwa ikijitokeza kwa Zitto akiona wale wasiofuata mantiki za mawazo yake kama “Mazwazwa”. Hii ni ishara ya Umangi Meza na imekuwa ikijidhihirisha kwa yeye kuhodhi kila kitu ndani ya chama kama “Kiongozi Mkuu

Kwa kiufupi, Ilani hii kama ilivyo ya CDM ,uchumi wa viwanda kama kiungo muhimu umeachwa kando.Tunaona zaidi msisitizo ukiwa kwenye ubinafsishaji/privitization, ubidhaaishaji/commodification, usokoishaji/marketization kupitia uchumi ulioodhiwa na soko bila uthibiti wa dola. Dhana zinazoanzishwa kuongeza matatazo ya kimazingira, kama ilivyoelezwa nishati za makaa ya mawe na anasa au kula bata/consumerism zinaimarisha zaidi nguvu ya mtaji na kuongeza umasikini wa kitabaka. Sera zinazotupeleka kwenye kanuni ya ubairi/frugal principles wa matumizi bora ya rasimali inaonekana ni tatizo.

Baada ya kuangalia itikadi zinazoongoza Ilani za vyama husika hapo juu, sasa tunaenda kuangalia kwa kiufupi namna gani dhana za haki ya soko dhidi haki ya kijamii zinavyojidhihirisha kwenye viumpale vinavyolenga huduma za kijamii. Katika uchambuzi huu makala italinganisha Ilani ya CCM na CHADEMA kwa sababu tayari wametoa nakala zao za ilani kusambaa kwa matumizi ya umma. Tutaangalia eneo la elimu, afya, na maji.

Elimu; imepewa msukumo katika ilani za vyama vyote lakini utofauti wa namna ya kuioberesha unaonekana katika fikra kuu zinaongoza chama husika. Kwa upande wa CCM, elimu ya msingi na sekondari imejengwa katika uelewa kuwa upataji wa maarifa ya msingi ni haki ya kijamii inayopaswa kutopewa thamani ya vipande vya pesa. Ikijengwa katika uzoefu wa awamu yake ya uongozi, ushuhuda wa mafanikio chanya. Katika kushawishi umuhimu wa kufanya elimu kutokuwa na malipo takwimu za uwekezaji huu wakijamii katika sekta ya elimu kibajeti, miundombinu, rasimali watu na idadi ya uandikishaji inatoa tumaini na ushawishi unaomgusa mtu wa tabaka la chini moja kwa moja. Na katika hotuba ya kunadi ilani iliyotolewa na mgombea Urais kuhusu mabadiliko ya shule za umma kufanya vizuri na zinazochukua watoto wa kimasikini linasisitizwa zaidi.

Kwa upande wa CHADEMA, inaendelea kusukuma fikra kuwa vitu vinavyosimamiwa na umma havina tija. Wanasisitiza kupanua wigo wa kubidhaisha elimu kwa hoja kuwa utaratibu wa kufanya ubia wa shule binafsi kutoa elimu bure kupitia ruzuku za serikali. Kilichoficha hapa ni dhamira ya wawekezaji wenye lengo la kuvuna faida mara dufu halizungumziwi. Hata hoja ya kuwa elimu tuliyonayo imekuwa ya mitahani na vyeti, inashindwa kufafanua kuwa chanzo kikubwa ni mashindano ya kibiashara yanayoongzwa na falsafa ya kukumbatia soko huria, au holela kama alivyowahi kusema Profesa Chachage.

Ufaulu ndio bango la kunadi biashara ya elimu na kupata wateja zaidi, lakini pia uzoefu unaonesha wanasiasa wamepeleka mitaji yao kwenye uuzaji wa elimu. Kwa hiyo mtazamo huu ni wa kushadadia uwekezaji binafsi katika elimu kama sehemu ya kulinda maslahi binafsi ya walanguzi wa elimu. Kwenye ilani, inasomeka kuwa ndani ya siku 100, “Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.” Hii haitakuwa bure. Bali kama nilivyoeleza hapo juu, ni mauzo ya elimu kupitia kodi za walalahoi, kuwaneemesha wachuuzi wa elimu. Lakini tofauti na CCM inayosisitiza elimu ya kujitegemea katika nyanja zote, tunaona fikra ya elimu bora kama picha zilivyowekwa inaonesha elimu inayokonga matamanio ya tabaka la juu linalozalisha wategemezi wa kidigitali katika ufanyaji kazi, hali inayopelekea kile wanachokiita “uchumi wa kidigitali” ambao hatuna uthibiti nao. Badala yake ni uchumi wakuwanufaisha zaidi wanavuna data, kama eneo jipya la unyang’anyi wa nchi za Magharibi.

Maji na afya; msukumo wa kuendesha miradi ya kijamii kwa nguvu ya soko kwa upande wa CDM siyo eneo la elimu, tunaona hata kwenye upande wa huduma za maji msisitizo upo hapa. Na wanaliweka bayana katika ilani kuwa “Kwa kushirikiana na sekta binafsi kuongeza ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, salama na ya uhakika kwa wote”. Vile vile afya nayo inaonekana katika mrengo huo huo wa kisoko na ndani ya ilani imefafanuliwa kwa neno la kisoko kuwa “Ni kweli kwamba huduma bora ya afya hapa nchini imekuwa ni bidhaa adhimukuweza kupatikana….”(uk.41). Ubidhaishaji wa huduma hii unaendelea kujitokeza katika nia yake ya kuwa “Itahimiza sekta binafsi kuwekeza katika katika kuanzisha huduma ya usafiri kwa wagonjwa katika hospitali za umma.” Na hili pia limesisitizwa katika uzalishaji wa dawa kuwa utachukua mkondo wa soko. Hapa inaoneka tatizo la afya ni kutokuwepo nguvu ya soko yenye msukumo wa kifaida ndio maana inakuwa mbaya. Hivyo kwa kuleta soko mambo yatakuwa vizuri.

01.JPG

View attachment 1595017

View attachment 1595018

View attachment 1595019

View attachment 1595020
Nilichojifunza katika kampeni hizi CCM wana mfumo mzuri sana wa kuwaandaa viongozi na wamewaacha wenzao kwa mbali sana, yani hadi sasa ukisikiliza sera za wagombea wengine hata hupati agenda ya kueleweka, simply CCM na mgombea wao wako vizuri na wanastahili kuongoza Tanzania.
 
Back
Top Bottom