Ni movie gani ambayo ulishawahi kuiangalia halafu baadaye ukajuta kwanini umeiangalia?

koba lee

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
964
1,552
Wakuu kwema?

Niende kwenye mada husika,nauliza hivi ni movie gani ulishawahi kuiangalia lakini baada ya kuisha ukajuta kwanini umeingalia kutokana na mambo ambayo umeyaona humo yanaweza kua mauaji,usaliti,uchawi n.k.

Mimi binafsi ni mpenzi wa kuangalia filamu ile sana na nimetazama nyingi sana lakini kuna movie moja mpaka leo hua najuta kwanini niliiangalia.Filamu yenyewe inaitwa A SERBIAN FILM.

Wakuu siwashauri muingalie hiyo movie kama roho yako ni nyepesi na kama kuna mdau alishawahi kuicheck hebu njoo utoe mawazo yako uliionaje.

Na pia hebu taja movie yako ambayo unajuta mpaka leo kuitazama

Nawasilisha
 
Mkuu SAW na yenyewe naielewa ina mambo mengine unayaangalia kwa jicho moja ukiwa umeliminya,ila hii A serbian film inakuharibu mpaka kifikra na kihisia
dah,kama hiyo nizaidi..mkuu kwangu hapana maana hiyo saw tu nilivyocheki chakula hakikushuka kabisa na ilichikua mda kutoka kichwani..sasa hiyo a serbian film sindo itakua balaa
 
dah,kama hiyo nizaidi..mkuu kwangu hapana maana hiyo saw tu nilivyocheki chakula hakikushuka kabisa na ilichikua mda kutoka kichwani..sasa hiyo a serbian film sindo itakua balaa
Mkuu hiyo ina unyang'au wa kutosha,mpaka unajiuliza hii movie director au alieandika scripts ni binadamu au ni wakala wa shetani,kiufupi ilipigwa ban isionyeshwe kabisa nchi nyingi Duniani
 
Mkuu hiyo ina unyang'au wa kutosha,mpaka unajiuliza hii movie director au alieandika scripts ni binadamu au ni wakala wa shetani,kiufupi ilipigwa ban isionyeshwe kabisa nchi nyingi Duniani
kha!! acha niwaachie wenye roho ngumu kwakweli
 
Hivi imeshaendelea maana si alifika mpk duniani..😂
Balaa duniani sijui kitaumana vipi tu
Alifika duniani akidhani pweza kabaki angani,kumbe yuko nae,jinsi ilivyoisha inabidi iwe na muendelezo,ngoja tusubiri.
 
Back
Top Bottom