Ni model ipi Serikali ya Rais Magufuli inatumia kupambana na ufisadi?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,461
8,669
Hii vita ya Ufisadii ya JPM ni ya kipekee kabisa na huenda kuliko nchi yoyote ile Duniani kwa ni nini?

1. Vita ya ufisadi huenda sambamba na uhuru wa kutisha wa vyomba vya habari hilo huku halipo kabisa.

2. Vita ya ufisadi huenda sambamba na sheria kali mno za kudili na mafisadi. Huku hilo halipo bali ni one-man show tu.

3. Idara kama za ukaguzi hupewa nguvu za kupitiliza kabisa na hufikia sehemu wao wanakuwa na kitengo kinacho jitegemea kwa kila kitu. Hilo halipo kwenye hii ya Rais Magufuli.

4. Kuna kuwa na uwazi wa kutisha kwenye vita dhidi ya ufisadi hilo huku halipo kabisa. Bunge haliko live na yoyote anaye hoji pesa huitwa sio mzalendo.

5. Kwenye manunuzi ya umma kuna kuwa na uwazi mkubwa sana. Hilo halipo, ndege anachagua mwenyewe wanafanya kumtumia picha na yeye anachagua.

Sasa je, kwenye hii vita Rais Magufuli anatumia model gani?
 
Hii ni vita dhidi ya mafisadi ambao hawamuungi mkono, kwa upande mwingine ni neema kwake yeye na mafisadi wenzake wanaomuunga mkono. Huwezi kuwa na taasisi dhaifu alafu unaigiza kuwa unaleta mabadiliko.
 
Nenda Keko na Segerea uulize wakupe majibu walioko huko, kisha upite ofisi za DPP uone foleni ya mafisadi yakilipa pesa ya wananchi then pitia Ufipa uone watu walivyoshika mashavu wakilalama hakuna agenda. Tena, pia usisahu kumuuliza Zitto jinsi anavyoumia kumuona Rais Magufuli akiwa hai.

State agent
 
Mwacheni Rais afanye kazi yake, apewe muda, uongozi hauna formula, akimaliza muda weke tumpime.
 
MURUSI,

Kamtoa CAG orijino na kuweka CAG feki wa 'ndiyo mzee' kisa eti CAG orijino aliwaumbua juu ya upotevu wa Trilioni 1.5 na upotevu wa mabilion ofisi ya Bunge na huko ACTL kwenye ufisadi wa kutisha duniani kote.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa.
 
hii ni vita dhidi ya mafisadi ambao hawamuungi mkono, kwa upande mwingine ni neema kwake yeye na mafisadi wenzake wanaomuunga mkono. huwezi kuwa na taasisi dhaifu alafu unaigiza kuwa unaleta mabadiliko.

Haina tofauti na vita feki ya madawa pale genge moja kumtumia mwenye nguvu kulisambaratisha genge pinzani huku likiteka akili za wajinga kupata umaarufu wa kisiasa.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa
Hati chafu zipo CCM kwani wakurugenzi wote wa CCM wilayani mikoani kila mwaka wana hati chafu, huyo CAG kaenda kulinda ufisadi wizara ya miundo mbinu hasa ACTL na ujenzi wa reli ambapo wamepiga sana bila huruma
 
Hii vita ya Ufisadii ya JPM ni ya kipekee kabisa na huenda kuliko nchi yoyote ile Duniani kwa ni nini?

1. Vita ya ufisadi huenda sambamba na uhuru wa kutisha wa vyomba vya habari hilo huku halipo kabisa.

2. Vita ya ufisadi huenda sambamba na sheria kali mno za kudili na mafisadi. Huku hilo halipo bali ni one-man show tu.

3. Idara kama za ukaguzi hupewa nguvu za kupitiliza kabisa na hufikia sehemu wao wanakuwa na kitengo kinacho jitegemea kwa kila kitu. Hilo halipo kwenye hii ya Rais Magufuli.

4. Kuna kuwa na uwazi wa kutisha kwenye vita dhidi ya ufisadi hilo huku halipo kabisa. Bunge haliko live na yoyote anaye hoji pesa huitwa sio mzalendo.

5. Kwenye manunuzi ya umma kuna kuwa na uwazi mkubwa sana. Hilo halipo, ndege anachagua mwenyewe wanafanya kumtumia picha na yeye anachagua.

Sasa je, kwenye hii vita Rais Magufuli anatumia model gani?
Magufuli mwenyewe fisadi.
 
Akimaliza mda wake ni yeye peke yake mwenye kinga atapona lakini wengine wataelekea magerezani hususani ufisadi wa ACTL utawapeleka wengi jela huko mbeleni
Maisha ni upepo ya kesho uyajui,kama aliishi nyumba za kioo je,siti ya daladala haina mwenyewe,ikiingia team pinzani je?.Katiba ni makaratasi si musaafu ndo usiobadilika.Kinga ya kutokushtakiwa ni busara za atakaekuwepo maana vifungu vina uwazi mwingi tu hata vya kumlaza mtu mahabusu miaka bila kumsthaki.Hakuna sheria yeyeto isiyo na udhaifu wake.
 
5. Kwenye manunuzi ya umma kuna kuwa na uwazi mkubwa sana. Hilo halipo, ndege anachagua mwenyewe wanafanya kumtumia picha na yeye anachagua.
Hii vita ya Ufisadii ya JPM ni ya kipekee kabisa na huenda kuliko nchi yoyote ile Duniani kwa ni nini?

1. Vita ya ufisadi huenda sambamba na uhuru wa kutisha wa vyomba vya habari hilo huku halipo kabisa.

2. Vita ya ufisadi huenda sambamba na sheria kali mno za kudili na mafisadi. Huku hilo halipo bali ni one-man show tu.

3. Idara kama za ukaguzi hupewa nguvu za kupitiliza kabisa na hufikia sehemu wao wanakuwa na kitengo kinacho jitegemea kwa kila kitu. Hilo halipo kwenye hii ya Rais Magufuli.

4. Kuna kuwa na uwazi wa kutisha kwenye vita dhidi ya ufisadi hilo huku halipo kabisa. Bunge haliko live na yoyote anaye hoji pesa huitwa sio mzalendo.

5. Kwenye manunuzi ya umma kuna kuwa na uwazi mkubwa sana. Hilo halipo, ndege anachagua mwenyewe wanafanya kumtumia picha na yeye anachagua.

Sasa je, kwenye hii vita Rais Magufuli anatumia model gani?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom