Ni mkoa gani Tanzania unatamani kuishi?

Tanzania ni nchi kubwa sana, Mungu ameibariki kuwa na maeneo makubwa na yenye watu wa tamaduni mbalimbali.

Mimi ni mwenyeji wa Nachingwea. Huko ndiko asili ya familia yangu. Napapenda sana kwetu. Na huko nitazikwa siku nikiaga dunia.

Nilipokuwa mdogo nilitamani sana kutembelea mikoa mingine, nje ya Lindi kujionea uzuri wa nchi na watu wake.

Alhamdulillah, elimu ilinifanya niishi mikoa sita Tanzania hii.

Nilipomaliza shule ya msingi, nilichaguliwa shule ya vipaji ya Shy Bush. Huko Shinyanga sehemu wanapochimba almasi.

Mazingira ya huku sikuyapenda sana japokuwa hayana tofauti na ya Nachingwea.

Maji ni shida sana mkoa wa Shinyanga. Ila kizuri cha mkoa huu ni watu wake ni wakarimu sana, japokuwa huwa wanawateta wageni kwa kilugha pia watu wake ni washamba ila wana mioyo poa sana.

Baada ya kuhitimu O Level, nilichaguliwa Kibaha Boys PCB. Mazingira sio mabaya na sio mazuri kihivyo. Wenyeji ni wazembe sana ila wachangamfu mno. Ni waswahili sana, hawaogopi linapokuja suala la mazumgumzo.

Chuo nilichaguliwa UDSM, huku sitapasema sana maana watu wake Havana tofauti na watu wa pwani. Japokuwa huku makabila ni mengi.

Field yangu ya kwanza nilifanya Kilimanjaro( Moshi), hulu mazingira ni mazuri sana, hali ya hewa inavutia sana. Wenyeji wa huku ni wachapakazi haswa ila shida yao kubwa ni wabaguzi mno. Mwenyeji wangu, (Mtu wa kwetu Lindi) aliniambia huku ukifanya biashara unaweza usipate wateja kwa sababu ya kabila lako.

Field yangu ya pili nilifanya, Musoma, huku nikakutana na kina Mwita na Chacha.

Mazingira niliyapenda na watu wake pia. Ni wachapakazi na wakarimu kwa wenyeji. Shida yao kubwa wana-element ya ubabe.

Leo nikiambiwa nichague wali pa kuishi, nitachagua Lindi nyumbani, maana nimepazoea. Wewe je?
Njoo hapa swax , tangu jakaya alete huu mkeka(lami) ,hakika panapendeza sana
Kama una akili za kushika jembe na ishu za mazao ,unatoboa Asbh Saa mbili kabla jogoo hawajaamka
Karibu swax muyomba...

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wewe unainywa bila ya Nyama yenye pilipili hua unakosea
Duh, kumbe ndo huwa hivyo!? Kuna jamaa huwa nawaona hawatumii hiyo kitu bila nyama.

Sasa hiyo nyama, wanakata kata nyanya, vitunguu, pilipili kwa wingi halaf wanaleta na kikopo kile cha Mo XTRA kilichojaa nyongo either ya ng'ombe au ya mbuzi then wanamix hivyo vitu vyote halafu wanakuwa wanachovya nyama humo!

Sasa ule uchungu wa nyongo + pilipili ni hatari aisee!
 
Tanzania ni nchi kubwa sana, Mungu ameibariki kuwa na maeneo makubwa na yenye watu wa tamaduni mbalimbali.

Mimi ni mwenyeji wa Nachingwea. Huko ndiko asili ya familia yangu. Napapenda sana kwetu. Na huko nitazikwa siku nikiaga dunia.

Nilipokuwa mdogo nilitamani sana kutembelea mikoa mingine, nje ya Lindi kujionea uzuri wa nchi na watu wake.

Alhamdulillah, elimu ilinifanya niishi mikoa sita Tanzania hii.

Nilipomaliza shule ya msingi, nilichaguliwa shule ya vipaji ya Shy Bush. Huko Shinyanga sehemu wanapochimba almasi.

Mazingira ya huku sikuyapenda sana japokuwa hayana tofauti na ya Nachingwea.

Maji ni shida sana mkoa wa Shinyanga. Ila kizuri cha mkoa huu ni watu wake ni wakarimu sana, japokuwa huwa wanawateta wageni kwa kilugha pia watu wake ni washamba ila wana mioyo poa sana.

Baada ya kuhitimu O Level, nilichaguliwa Kibaha Boys PCB. Mazingira sio mabaya na sio mazuri kihivyo. Wenyeji ni wazembe sana ila wachangamfu mno. Ni waswahili sana, hawaogopi linapokuja suala la mazumgumzo.

Chuo nilichaguliwa UDSM, huku sitapasema sana maana watu wake Havana tofauti na watu wa pwani. Japokuwa huku makabila ni mengi.

Field yangu ya kwanza nilifanya Kilimanjaro( Moshi), hulu mazingira ni mazuri sana, hali ya hewa inavutia sana. Wenyeji wa huku ni wachapakazi haswa ila shida yao kubwa ni wabaguzi mno. Mwenyeji wangu, (Mtu wa kwetu Lindi) aliniambia huku ukifanya biashara unaweza usipate wateja kwa sababu ya kabila lako.

Field yangu ya pili nilifanya, Musoma, huku nikakutana na kina Mwita na Chacha.😀😀

Mazingira niliyapenda na watu wake pia. Ni wachapakazi na wakarimu kwa wenyeji. Shida yao kubwa wana-element ya ubabe.

Leo nikiambiwa nichague wali pa kuishi, nitachagua Lindi nyumbani, maana nimepazoea. Wewe je?
ROCK CITY
 
Mimi niko tayari kuishi popote Tanzania ila tu kuiwe na mambo haya
1. Joto kali
2. Ushirikina
3. Shida ya maji
4. Ubaguzi wowote ule

Mikoa pendekwa ni hii
1. Mbeya
2. Kilimanjaro
3. Arusha
4. Iringa
Wilaya
1. Lushoto
2. Kyela
3. Tunduma
4. Same
5. Moshi
6. Usariva
Wachanga bwana utadhania ushirikina hawaujui!!? Wakati December lazima akatabike
 
Back
Top Bottom