Ni mkasa gani wa mapenzi umewahi kukuumiza moyo na ni kama umekutia ulemavu moyoni?

Nilimpenda binti mmoja hv basi nikawa na date nae basi siku akapata ajali ya Pikipiki jicho lake moja nusura litoke huku mazaake hana mpunga kwa dingi yake napo ndo hivyo walikuwa wameshaachana kitambo, basi nikapigiwa simu na rafiki yangu kuwa manzi kapata ajali na mazaake hana pesa za matibabu na wako hospitali, nikatoka home kwenda kumuangalia manzi pale hospitalini nimefika basi kumkuta manzi analia tu mazaake nae yupo tu hana ramani na matibabu bado kabisa, mwanaume nikaingia chumba cha daktari nikamuuliza huyu mgonjwa atapona kwa sh? Akajibu 20000 nikamcash palepale daktari. Akaanza matibabu pale akawa anaenda kuchoma sindano asubuhi na jioni, nilikuwa sijui akawa anaenda na mchana kumbe kuna kitu kipo nyuma ya pazia ambacho sikufahamu kumbe daktari alikuwa amemchumbia tayari na nyumbani kwao wakaelewana mahali, basi binti kwa wakati huo alikuwa ameshapona. Nyodo zikaanza na binti huyo akawa Haji kwangu na hata anaweza kushinda hayupo hata nyumbani kwao yupo kwa jamaa tu, muda huo hana kovu hata moja usoni, ikafikia hatua akawa anapita na huyo daktari wakiwa wameambatana kwa macho yangu hv naona yaani niliumia na sikuwahi kuwa na maumivu makali kiasi hicho before,,. Kumbe hata daktari mwenyewe alikuwa tapeli tu hakuna kitu. Hata hakumuoa kabisa na nikikumbuka hiki kitu kutoka moyoni nasema binti yeyote yule akiwa mbichi huwa wanajisikia saaana na tena saaana. Nakumbuka huu mkasa na nakumbuka msemo mmoja unasema, Usiheshimu kila kitu hapa duniani maana hata chumvi huonekana kama sukari.
Ikawaje sasa mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi mkasa mbashara kabisa wa kimapenzi ambao unaishi na mimi na kamwe siwezi kuusahau kwani Moyo bado unavuja damu. Ilikiwa April 17 mvua za vuli zikielekea kukoma huko Iringa basi kuna manzi mmoja moto wa kuotea mbali nilikuwa nampenda kinyama. Nikawa nampigia misele kimyakimya na sikutaka mtu yoyote ajua kwani sikuwa na hakika kama atanikubalia. Kimsingi sikuwa nimewahi mtamkia ila nilikuwa namvutia kasi kwa mwendo wa kobe. Siku moja manzi kaja room hata dakika 10 hazijaisha akaja jamaa yangu kunitembelea nilipiga naye O-level, mwanangu sana enzi zile za secondary. Hivyo nikawa na wageni 2 at once. Nikaona isiwe hatari niwachekie soda kwa mangi mtaa wa pili. Ile nimetoka tu sms ikaingia toka kwa jamaa......Oyaaa hii pisi yako mzazi? Mi nikasema NO.....just friend. Bwanabwana ile nimenunua mazaga nataka nigeuke toka kwa Mangi nakuta test tena toka kwa jamaa......Oyaaa kausha kwanza namuimbisha huyu demu anaelekea kabisa. Kilambo cha soda kilinipokonyoka, niliishiwa nguvu. Mwili ulinitetema. Nikamwambia kweli? Jamaa akasema uchune kwanza jomba mi namla huyu manzi kalegea kabisa na lita nishapiga.
Basi nikawa sina namna jamaa akagonga. Sikurudi hadi baada ya saa hivi kuja nakuta jamaa katembea anasema mwanangu nimemla huyo dogo. Pembeni demu kalala usingizi wa pono na kichwani timtimu. Alivyoamka sikusema chochote nikaaachana na mpango huo hadi leo hii. ILA MOYO UMELEMAA HADI LEO na sidhani kama CCRBT wanaweza nifanyia tiba.

Kwa sasa mimi ni mstaafu wa mambo ya mapenzi nikiishi kijijini niliko zaliwa
Idodi-Iringa

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaaaaaa Mkuu polee sanaa, ulikosea step mwanzo tu, ungemwambia huyo Shem wako!!!
Mkuu upo Idodi kabisa au mapogoro, lyangolo haaaaaaaaa!!

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Back
Top Bottom