Ni mimi tu ninamkosi na wachaga au ndiivyo walivyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mimi tu ninamkosi na wachaga au ndiivyo walivyo?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dr. Sakis One, Dec 27, 2010.

 1. D

  Dr. Sakis One Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa Wana JF,

  Mimi Naomba msaada wenu wa Ushauri ili niondokane na hii hali ya utumwa wa kupenda. Kuna mtoto mmoja wa kichaga simuelewi nini lengo lake! Nilikuwa na mahusiano naye toka mid. April, sijahusiana naye kwa tendo takatifu hadi sasa. Mie nipo huku napiga box, yeye alikuwa huko Waja leo na sasa yupo DSM lakini kilichonishangaza awali alikuwa akiniambia kuwa next week or kesho naenda DSM kuna kazi nimetumwa kuifuatilia.

  Baada ya hapo safari zikazidi, mawasiliano hadi mie nianze, mbaya zaidi kanistukiza ghafla eti kahamia kikazi Dar, na hapo napewa taarifa wakati tayari yupo DSm anasema "aaa haa nipo ofisini kazini, nimechoka hata kutuma msg muda sina"! Je ndio mapenzi ya wachaga yalivyo? Najiuliza au sababu mie sio mchaga? Ni kitu gani hasa wanawake wa kichaga wanapenda zaidi toka kwa wanaume ukiachilia mbali mapenzi? Mwisho naomba kuuliza hivi kwanini wanawake wengi wa kichaga huwa hawaolewi haraka na utakuta umri unakwenda yeye bado haolewi lakini mali ukiomba anagawa kama kawaida lakini ndoa hazifungwi?

  plse wana JF naomba mnijuze ili kama vipi nihame huko migombani na nisipende tena hii kabila!
   
 2. s

  shosti JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kashakuona huna maana ndio maana
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Pole sana
   
 4. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  duh,halafu we kalale bana labda kesho utakuja kivingine
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Duh!Kaazi kweli kweli!Anatafuta maisha yake kwanza..!Alafu nyie wanaume bwana...hamna jema kabisa...tukiweka kuolewa mbele mnakimbia,tusipoonyesha nia mnauliza kulikoni!Jibu ni kwamba wanaotaka kuolewa lakini wanachelewa wanataka kujipanga kwanza kimaisha kabla ya kutulia kutengeneza familia...wengine hawataki kabisa!Na tunachotaka zaidi ya mapenzi ni maendeleo kwahiyo zichange ufanye mambo ya maana ndo utamnasa vizuri!
   
 6. D

  Dr. Sakis One Member

  #6
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LIZZY,

  Asante kwa huo mchango wako, nimeuelewa lakini laiti angeniweka wazi juu ya hilo kuwa yeye na kazi kwanza na mapenzi baadae nadhani nisingeumia hivi, ila mbona hamuwi wawazi au kapata jamaa mwingine?? ni hapo tuuu
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa we unataka awe tegemezi bwana?Mwache mtoto wa kike afanye kazi hata akikupotezea mauchungu hayatalingana na kama angekua anakuchuna!Kuhusu kua na bwana mwingine inabidi umpige maswali ya nini anataka kwako na kama hakutaki akuambie!
   
 8. s

  shosti JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Babu vipi jamani mbona wanikimbiza,sawa bwana ngoja nikapumzike maana hali mbaya
   
 9. D

  Dr. Sakis One Member

  #9
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thankx Mkuu,
  Nahaidi kuyafanyia kazi mawazo yako, ila dah moyo wangu nahisi nyongo imeshapasuka si unajua tena mtu ukimpenda alafu unahisi anakutenda!! but thankx for U're advice
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Karibu!
   
 11. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Mkuu sioni hayo matatizo ulionayo na huyo msichana yana husiana vipi na uchaga wake .Thread kama hii ndio zinaletaga chuki za ubaguzi.Wewe unatatizo na mchaga mmoja halafu tabia yake ndio una generalize kwa wachaga.
  Halafu unajiita doctor, Shame on you!
   
 12. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2010
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hapa sio uchaga ni kutapeliwa na binti huyo

  anakuchuma pesa kwa western union yeye anaendelea na bwana wake

  hauna haja ya kukandia wachaga bali ni uamuzi wako tafuta labda wahaya au makabila mengine

  ni mtu alivyo nawe unakutana na wasiokupenda kaka
   
 13. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  kwanza achana na mambo ya ukabila. Nashangaa uko nje bado hujapata exposure au mabox yanakukeep busy sana.
  Pili nikushauri tu kwamba fimbo ya mbali haiuwi nyoka. Kutokana na uzoefu wangu hapo huna mpenzi, kuna mtu anamkeep busy. Wewe uko mbali sana na kwa jinsi hali halisi ilivyo duniani na hasa tz kwa sasa, msichana hawezi subiri mapenzi ya face book na sms...
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kesha kuona hujui kuhonga wenzio wamesha honga pamoja na kazi wewe honga visa na ticket atakuwa wako tu ni kuzidiana dau
   
 15. D

  Dr. Sakis One Member

  #15
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nadhani umenisoma sivyo ndivyo. Kumbuka Tanzania ina makabila zaidi ya 120 lakini wachambuzi wa mambo ya mahusiano wanajua almost kila kabila lina tabia zipi kuu katika suala la mapenzi au ndoa. Binafsi sikuwa na maana ya kuponda wachaga ila nilikuwa namaanisha msichana niliyekuwa nimempenda ni wa kabila hilo ili niweze kupata mchango wa mawazo ulio na reference sahihi ya mtu maeneo atokayo kuliko wadau waanze kuuliza huyo ni wa wawapi.

  Anyway, kama kuna watu nitakuwa nimewakwaza kwa hilo sina budi kuadmit kuwa sitarudia kufanya hivyo bali kwa sasa naomba mawazo yenu ili yaweze kunipa mwanga wa nini cha kufanya.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Very well said
   
 17. D

  Dr. Sakis One Member

  #17
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu nakushukuru kwa mchango wako lakini sio kuwa box zinanikeep sana busy hapana ndio maana hata muda mwingine huwa nautumia kuongea na huyu binti but now mambo yamekuwa sivyo ndivyo kabisaa hadi inachangia kushuka kiwango changu cha kupiga box si unajua tena mambo ya mapenzi ni noma!

  Kuhusu kutaja kabila sikuwa na nia mbaya mkuu ila binfsi niltaka iwe wazi ili nijue ni mimi tu naumizwa katika pande hizo au kuna wadau wengine walishawahi umizwa kama mimi?

  Fimbo ya mbali huo ni msemo tu ila kuna watu wapo mbali na wapenzi wao lakini mambo yanakuwa safi @ sasa sijui kama ni kweli au ndo hivyo siri ya mtungi kata ndio ijuayo kama kuna maji au laa but still am appreciating U're contribution.

  Thankx
   
 18. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,374
  Likes Received: 3,211
  Trophy Points: 280
  Kilichomo ndani ya habari kinatofautiana na heading, hujaeleza hiyo mikosi, habari yako siyo mikosi kwani hujatueleza ni mademu wangapi wa kichaga wamewahi kukuzingua, sana sana unaomba ushauri kama mademu wa kichaga wanafaa kuoa. Ni vigumu kusema kabila fulani hawafai kolewa karibu wote na kabila lingine ni wazuri kwa kuolewa
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Usitishwe na umbali Dr.!Hata wa karibu akitaka kuibiwa ataibiwa tu...yote inategemea na mtu mwenye na sio umbali wala pesa!
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280
  Pole sana.

   
Loading...