Ni mila ama ni utumwa wa kiakili??

fundiaminy

JF-Expert Member
Jun 4, 2009
355
51
Natanguliza na salaam.
Kuna dada flani amepatwa na tukio ambalo hakutarajia japo ni mtu amekomaa.Anadai kuwa katika kabila na mila zao hajawahi kuliskia ila ndilo hili linamsumbua akili.
Ni wa tatu katika familia ya waschana watatu.Ana miaka 28 na dadazake wanaomtangulia wana miaka 32 na 36 mtawalia.Alipata mchumba na katika kupanga mikakati ya kufunga ndoa walienda kujitambulisha kwa wazazi wote.Tatizo ni kwamba walipoenda kwa wazazi wa dada,wazazi walimkatalia kuolewa mpaka dada zake waolewe kwanza..ukiweka akilini kwamba dada zake wana miaka zaidi kumliko na wala hawajafikiria kuolewa..pili walichosema wazazi wa dada ni kwamba iwapo dada ana lazima kuolewa na huyo kaka ama kaka yeyote yule kabla dada zake kuolewa,ni sharti huyo kaka alale na kati ya dada zake wakubwa ndipo apate rukhsa ya kumuoa.Dada yuko katika njia panda.Je, ushauri gani unafaa?
 
mi najua wahindi,wale baniani wana utamaduni huo,kuolewa lazima aanze wa kwanza....

hilo la kulala na dada zake sijawahi sikia....kabila gani hilo tukaoe? lol
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbona simple tuu... Kama wewe ungekuwa ndio bwana harusi mtarajiwa unadhani ungefanyaje?... Mie raha tuu nagonga wote wakubwa then naoa mdogoukistaajabu ya firauni/farao utakoma na ya mussa/moses...mbona nishasikia wahindi kabla binti hajaolewa baba anatakiwa amuonje bint na kaka kabla hajaoa lazma apige zoezi na maza...so hili la hapa kwetu mie halinishangazi saaana...ukienda romaaaaaaa fanyya kama wafanyavyo warumiiiii.
 
mi najua wahindi,wale baniani wana utamaduni huo,kuolewa lazima aanze wa kwanza....

hilo la kulala na dada zake sijawahi sikia....kabila gani hilo tukaoe? lol

Hahahaah lol! na lazima kabla ya kuoa uhakikishe mchumba ana dada ambao bado hawajaolewa :):):)....Mimi kwa maoni yangu hizi mila zimepitwa na wakati. Huyu dada kajipatia bahati yake ya kumpata mtu ambaye yuko tayari kumuoa lakini kutokana na mila za mwaka 47 inabidi asiolewe hadi wakubwa zake waolewe kabla yake. Kwa maneo mengine kama hao dada zake wakidodea nyumbani basi naye ndiyo hivyo tena inabidi adode tu!!!
 
mi najua wahindi,wale baniani wana utamaduni huo,kuolewa lazima aanze wa kwanza....<br />
<br />
hilo la kulala na dada zake sijawahi sikia....kabila gani hilo tukaoe? lol
<br />
<br />

ni kabila flani nchini kenya.kwa sasa nalihifadhi.

Na kuna hili pia kwamba iwapo mume na mke wameoana na mume atangulie kufariki bila ya kupata mtoto halaf na mke nae afariki basi italazimu mwanamume mmoja wa huo ukoo amle uroda marehemu ili kutakasa ukoo..ushaliskia hilo mkuu Boss? Na hapo pia utataka kuoa? Ha ha ha..kweli inasemekana kuwa uone.
 
binti amekubalika kiumeni??
tukikumbana na vikwazo kama hivyo huwa tunachukuana tu, then tunakuja bariki ndoa badae wazee wa binti watalainika tuuuuu...
 
Hahahaah lol! na lazima kabla ya kuoa uhakikishe mchumba ana dada ambao bado hawajaolewa :):):)....Mimi kwa maoni yangu hizi mila zimepitwa na wakati. Huyu dada kajipatia bahati yake ya kumpata mtu ambaye yuko tayari kumuoa lakini kutokana na mila za mwaka 47 inabidi asiolewe hadi wakubwa zake waolewe kabla yake. Kwa maneo mengine kama hao dada zake wakidodea nyumbani basi naye ndiyo hivyo tena inabidi adode tu!!!

Nina mashaka na hizo mila kama kweli zipo. Isiwe ni tatizo la hiyo familia pekee na siyo kabila
 
mnnnh hakuna hao wazazi wamekua manipulated na hao dada zake wa 1................pana uwalakini hapa
 
Afadhali ya mila hiyo kuliko kuleeee...kwa mh.maiki mstaafu. Eti ukiwowa mwanamuke kabla uja du kuna kizee kwanza kinatakiwa kipitie kwa ajili ya kumtakasa lol.
 
Mila mila niwakati sasa wakujaribu kwenda kwa wakati ilopo huyu dada aishi na jamaa mpaka pale wazazi watakapo kubali wajekubariki ndoa tu
 
Nina mashaka na hizo mila kama kweli zipo. Isiwe ni tatizo la hiyo familia pekee na siyo kabila
Zipo mkuu. Mimi nina rafiki yangu ni mchaga wa machame, aliolewa mwaka huu mwezi wa nne. Ana wadogo zake wawil wakike, walipata wachumba wakaja kujitambulisha wakazuiliwa eti mpaka kwanza dada aolewe, mtaan wakawa wanamsema huyo dada eti anawazuia wadogo zake kuolewa cz yeye bado hajaolewa hivyo hao wadogo zake hawawez kuolewa, nkajarib kumwuliza akasema ni kweli wadogo zake hawawezi kuolewa mpaka yeye aanze kwanza. Nilistaajab vile mimi pia ni mchaga( sio wa machame ) na cjawah sikia hvyo kwetu. Ila huko kwao hakuna hiyo ya wachumba kulala na dada!
 
Back
Top Bottom