BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
kutwambia Watanzania nani ni mmiliki halali wa mgodi wa Buhemba? Je, katika kikao kijacho cha bunge kitakachoanza June 10 Waziri wa Madini, William Ngeleja ataweza kutwambia Watanzania ni nani mmiliki wa Buhemba? Je, Buhemba nayo kama ilivyokuwa Kiwira Coal Mining, Mkapa alijimilikisha katika mazingira ya kifisadi pamoja na swahiba wake Abdallah Kigoda?
CAG alitaka maswali zaidi yaelekezwe kwa msajili aliyeko hazina, kwa madai kuwa anaweza kuwa na majibu mazuri zaidi ya hilo, na kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka na asasi za serikali.
Naye Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja alipotakiwa kutoa ufafanuzi wake jana na msimamo wa serikali katika utata uliogubika mgodi wa Buhemba alisema jambo hilo linahitaji takwimu zaidi.
Jambo hili linahitaji takwimu zaidi halafu mimi sipo ofisini, tafadhali hebu wasilianeni na Kamishna wa Madini, atakuwa anafahamu zaidi, alisema waziri Ngeleja.
Aliongeza kuwa suala hilo linahitaji kujiandaa zaidi na kwamba yeye atamuagiza kamishna huyo wa madini atoe ufafanuzi kwa gazeti hili.
Suala la utata wa mgodi wa Buhemba limedumu kwa muda mrefu sasa, takribani miaka mitano, na kwamba mwishoni mwa mwaka jana wapinzani waliinyoshea kidole serikali kuhusu umiliki wake wa mgodi huo.
soma hapa