The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Nina rafiki yangu mmoja ambae tulisoma pamoja ana mahusiano na msichana mmoja takribani mwaka mmoja sasa, juzi aliamua kwenda kumtambulisha mchumba wake huyo kwa wazazi wake baada ya kumtabulisha kijana alipatwa na mshangao pale alipoambiwa na wazazi wake kuwa bado hajakomaa na hana uzoefu kwenye mambo ya mahusiano akaambiwa mwaka mmoja hautoshi.
Wazazi wake huyo kijana wakamwambia asubiri kidogo walau wakae kwa muda wa miaka mitatu ili wafahamiane zaidi na huyo binti, msichana wa watu alikuwa dissapointed kwa kuwa aliona kama vile wazazi wa huyu kijana hawamuamini yeye(msichana) pia wazazi wamemwambia kijana wao asubirie mpaka baada ya miaka mitatu ndio atakuwa amekomaa kuingia kwenye ndoa.
Baada ya rafiki yangu kunieleza hali halisi automatically nilianza kujiuliza maswali yafuatayo:
Je ni muda gani ambao mtu unapaswa kukaa kwenye uchumba kabla haujaoa? Je ni mwaka 1, 2, 3, au zaidi?
Je wazazi wamefanya sawa kumwambia kijana wao kuwa hajakomaa na kwamba anahitaji muda wa miaka mitatu zaidi?
Je kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu zaidi ni kigezo kimojawapo kinachokufanya uonekane kwamba umekomaa na sasa uko tayari kuingia kwenye ndoa?
Naomba kuwasilisha