Ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika au ya marais wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika au ya marais wa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalunguine, Nov 4, 2011.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Salaam:
  Pamoja na kwamba huwezi kutenganisha moja kwa moja ''role" ya marais walioongoza nchi hii kwa vipindi mbalimbali na historia ya Tanzania, mwelekeo unaoonekana hasa katika vyombo vingi vya habari vinavyotoa taarifa kuhusu miaka 50 ya uhuru wetu havitendei haki Watanzania. Kila kukicha baadhi ya Magazeti na TV yanayoonyesha matukio mbalimbali ya miaka iliyopita yanaelezea kwa sehemu kubwa zaidi Nyerere, Nyerere and Nyerere again. Hebu fikiria eneo moja la mfano moja kama usafiri wa aina mbali mbali tangu uhuru hadi leo - watu walivyokuwa wakienda kwa treni toka Kigoma hadi Dar, au wakati kukiwa na Mabasi ya East African Railways na mabadiliko yaliyoendelea kutokea hadi sasa. Ingepedeza zaidi tukapewa experiences za mambo yalivyokuwa katika sekta / shughuli mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine watu huzizungumzia kwa hisia zenye furaha na fahari kwa ujasiri na ukakamvu walioonyesha katika mazingira hayo yaliyopita - (JKT,MICHEZO NA BURUDANI,MAISHA YA SHULENI,UGALI WA NJANO, FOLENI ZA SUKARI, nk,) .Frankly inapofika mahali baadhi ya watu wanapotaka kutufanya wengine tusiwaze wala kuona mengine zaidi ya Nyerere .........INABOA!
   
Loading...