Ni miaka 40 kamili toka Hat trick ya Kwanza na Pekee kufungwa katika Kariakoo Derby

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,688
45,001
Jioni moja ya mwaka 1977 katika uwanja wa Taifa ( sasa Uhuru ) Simba SC ilifanya mauaji ya Shurabela, kwa kuwakandamiza Yanga goli 6-0 huku Abdalllah Kibadeni Mputa akitupia Hat trick katika mchezo huo.

Sasa ni takribani miaka 40 kamili tangu maajabu yale yatokee jioni ile ya mwaka 1977 pale Uhuru Stadium.Ni umri wa mtu mzima kabisa.

Je wadau ni nini kimesababisha wachezaji wengi wa vilabu vya Simba na Yanga kushindwa kuvunja rekodi hii adhimu licha ya Vilabu hivi kujaaliwa washambuliaji matata kwa vipindi tofauti kama Lunyamila, Zamoyoni Mogella, Madaraka Suleiman, Okwi, Tambwe na wengineo wote ambao wameshindwa kuvunja rekodi hii.

Je ni imesababisha rekodi hii iendelee kudumu huku wachezaji wakishindwa kuivunja?
 
Timu hizo zilishaacha kucheza "mpira" kila zinapokutana,

Zinaamini ujinga wa nguvu za Giza kupita timu zote zilizowahi kuwa ktk uso wa Dunia tangu iumbwe.
 
Hat trik watatoa wapi? Unakuta mchezaji anaamkia kiporo cha kande iliyochacha. Lunch mchana anavizia kwa jirani arage haijaungwa na dona. Jioni kabla ya kwenda mazoez kashata na kahawa anaiga wazungu "snacks". Gym uani kwa masela. Hapo utapata hattrik kweli? Halafu kwenye utawala huu wa Sizonje wameiba matrillioni hata ya wizara ya michezo
 
Back
Top Bottom