Ni miaka 3 sasa tokea Rais aingie madarakani. Je, haya yamekaje na nini hatima ya watanzania?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
{1} Je, Mtanzania yule anaeishi Kijijini na wa Mjini anaweza akamsifu kwa lipi?

{2} Je, Kuna juhudi zozote ambazo amezionyesha kushirikiana na Wapinzani?

{3} Je, Rushwa imepungua au imeongezeka?

{4} Je, Usalama wa raia na mali zao umeimarishwa?

{5} Je, Kuna mahusiano mazuri (URAFIKI) Kati ya Serikali na Wananchi?

{6} Je, Watu kuuwawa kwa kupigwa risasi na kukatwakatwa mapanga mpaka kufa,au kupotea na wengine kutekwa nani awajibishwe?

{7} Je, Uchumi wa watanzania umeimarika au umedorora?

Changia vyema kama hauwezi pita tu Matusi hayatakiwi, Ninaamini wewe ni muelewa na unaipenda Tanzania.
 
Jamani watanzania kwanini tunakuwa sio watu washukrani? Mh Rais kafanya mengi yanahitaji kupongezwa na watanzania wote. Kaokota treni zaidi ya 13, Je ni rais gani hapa Tanzania alishawah kuokota treni? Huyu ni chuguo la mungu, tumuombee.
 
Huyu jamaa kaletwa kusaidia kudidimiza democracy na kuleta machafuko.watanzania tuwe macho na huyu mtusi



Swissme
 
Kizazi kile kilikuwa na agenda kadhaa kuhusu ubaguzi katika kila nyanja iwe elimu walichaguliwa watoto wao ajira watoto wao kila eneo zuri unapata kwa rushwa kukawa na matabaka ufisadi nk wahenga wale walijadili sana mpaka walipo sikia Lyatonga mrema anataka kuwakomboa wakahisi anaweza kuwatoa pale lkn haikuwa hivyo hali ikawa ileile kukawa na wao na sisi walala hoi.
Ikatokea awamu ya tano ikajaribu kuondoa kero baadhi lakini watumishi wakabaki hoi wahenga wakatoweka kwenye mijadala wakabakia wanapambana na hali zao sasa kimekuja kizazi kipya hakijui wahenga walikotoka na kiu ya wahenga ilikuwa yafanyike haya yanayofanyika lkn kizazi kipya kinadai kwamba huo ni ukiukwaji wa Demokrasia bila kujua kwamba wahenga waliwahi kuchoka na nchi hii mpaka wakaomba Mungu apatikane kiongozi wa namna hii!!Nchi za kiafrika ukiwalea lea utajuta mifano ipo fuatilia Ghana,Msumbiji,Libya nk ni mfano tosha kabisa.Angalia eti leo wanahamasishana maandamano hewa hivi ikitokea wakafanikiwa kusikilizwa hoja zao na zikatekelezwa nini kitafuata wanampango thabiti wakuendesha nchi?wanadhani katiba inawafanya wawe na chuki binafsi kuliko kuikosa!Wahenga walisema ukizoea kula nyama ya mtu hutaweza kuacha kamwe mnaweza kuipindua nchi lakini haitakuwa mwisho wa mapinduzi kama ilivyo Libya njia sahihi ni kutafuta muafaka ya kile watanzania wote tunachokitaka kwa njia iliyotukuka lakini siyo kwa mabavu na kutukana wakubwa wenu matusi ya nguoni hata Mungu hapendi hivyo mtabaki na aibu mchana kweupe.Ugonjwa mkubwa unao tumaliza waafrika ni ukoloni mamboleo na kutokuwa na maadili ya kweli.
 
1. Kasi ya kuhamia mijini imepungua, watu wameanza kurudi vijijini. Sijui ni suala la kupongezwa au la.

2. Mmhhh ntaitwa mchochezi. Tyu tyu tyu, plaizi sehemu za siri, picha za utupu kulawitiwa, vitisho nk

3. Tukawaulize traffics kama ujenzi wa nyumba zao bado unaendelea.

4. Hapana kwa upande wangu, naogopa kutembea usiku vibaka wameongezeka.

5. Hapana, wananchi hatuogopi polisi bali TRA, TANESCO na maafisa wao wanaofanya ziara usiku wa manane.

6. Hili swali atujibu Mh. Waziri Mwigulu Nchemba.

7. Tumekatazwa kusema vyuma vimekaza. Ikawa uchumi huendeshwa kwa vyuma basi ninaimani umedorora kama vyuma vilivyo kaza.
 
Back
Top Bottom