Ni miaka 22 au 50 ya kuilaumu ccm kwa upumbazaji wa uchumi wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni miaka 22 au 50 ya kuilaumu ccm kwa upumbazaji wa uchumi wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Jun 15, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kwanza tuachane na CCM kama CCM ilizaliwa lini, (tudhani /assume imeshika dola toka mwaka wa uhuru na hivyo kuifanya chama tawala kwa miaka 50 ya uhuru wa taifa hili).

  CCM kama taasisi na kipaumbele cha umoja wa kitaifa

  Sasa tuje kwenye dhamira, mazingira ya kisheria, ya kimataifa na usahihi wa utawala huu wa CCM kabla ya kuanzishwa kwa vyama vingi hapo mwaka 1991/92. Kisheria CCM ilikua inalindwa na katiba ya JMT kama chama pekee cha kisiasa. Kiuchumi CCM ilikua sana sana inafanana na taasisi zaidi ya chama cha siasa katika kupanga na kutekeleza sera za kiuchumi bila ya kua na ushindani wa kuzifanya sera hizi mahsusi kwa ajili ya chama kama ambapo imetokea wakati wa mfumo wa vyama vingi. Kwa kifupi CCM ilikua ni taasisi ya kitaifa kuliko chama cha kisiasa.

  Dhamira ya CCM na haswa baada ya uhuru ilikua ni kuweka kipaumbele zaidi kwenye mambo ya amani na umoja wa kitaifa zaidi ya maendeleo ya uchumi. kutokana na mazingira ya wakati ule ya kisiasa (mapinduzi ya kijeshi barani afrika, ukoloni nchi za jirani, uhasama wa kiitikadi kati ya mataifa ya magharibi na nchi za kikomunisti n.k) ilikua ni sawa kwa taifa changa, kubwa kijiografia na lenye tamaduni nyingi, na maskini kuanza kwanza na juhudi za kujenga utaifa huku tukiwa tunakua taratibu kiuchumi. CCM imefanikiwa sana kwenye hili haswa pale ilipokua kama taasisi na siyo chama cha kisiasa kwenye ushindani wa kisiasa.

  Uchumi na matatizo ya kimfumo ya nje

  Kiuchumi CCM ilifanikiwa kwa hali ya juu na katika miaka ya 60-70 katikati pato la taifa lilikua na per capita ilikua kubwa kuliko miaka ya 80's, 90's. Hii ilichangiwa sana na mkazo katika kilimo na bei nzuri za mazao yetu katika soko la dunia. Miaka ya 70 mwishoni na baada ya oil embargo ya mwaka 1974, bei za mazao ya kilimo ilishuka sana katika soko la dunia na kuziathiri nchi nyingi zilizokua zinategemea kilimo na muda huo huo kupunguza pato la taifa kwa uagizaji mafuta ambayo yalikua na bei kubwa kutokana na mgogoro wa mashariki ya kati.

  Baada ya hapa taifa lilipata shida sana kiuchumi maka wakati wa mageuzi ya kiuchumi mnamo mwaka 1985. Hapa watawala wapya wa CCM walikua na jukumu la kuepusha kufa kabisa kwa taifa kiuchumi na kiustawi na usalama na hivyo miaka mitano ya kwanza ya mwinyi hatuwezi kuijaji kama ni miaka endelezi ya sera za kiuchumi za taifa hili bali ni miaka ya sera okozi za kiuchumi. Katika hili wapinzani hawana haki ya kuijaji CCM kama chama cha siasa wakati kilikua hakifanyi kazi katika mazingira ya sasa.

  Hitimisho

  Tukijumlisha miaka yote hii mpaka wakati wa mfumo wa vyama vingi na kipindi cha pili cha Mwinyi tutaona CCM imekua kama chama cha kisiasa kwa miaka isiyopungua 20-22 na siyo miaka 50 kama wapinzani wanavyosema.
  Kwa kkifupi CCM ya Nyerere na Kipindi cha kwanza cha Mwinyi ilikua ni kama Taasisi yenye mamlaka ya kuongoza nchi, sera nyingi zilikua za kitaifa zaidi na siyo mahsusi kichama. Huku ikilindwa kisheria na katiba CCM iliweza kuweka kipaumbele zaidi katika dhana ya kujenga umoja wa kitaifa na amani badala ya ukuaji wa haraka wa kiuchumi. Kwa dhana hii, kimatinki ni vizuri kwa wananchi wakajua kua CCM ya 28 ya kwanza ya uhuru ni tofauti kabisa na CCM ya miaka 22 baadae mbayo ndiyo inayofaa kupewa lawama zote za kupumbaza uchumi wetu kwani awamu ya pili ya mwinyi, awamu zote za Mkapa na hizi za JK CCM iko kwenye ushindani wa kisiasa ikiendeshawa zaidi kisiasa huku ikiwa imeweka kipaumbele ukiaji uchumi kwa kutumia sera zake mahsusi.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Upumbazaji ndo nini tena?
   
 3. m

  mharakati JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kufanya kitu kua hakipigi hatua inazotakiwa..


  ningetumia kudidimiza siyo haki kwa sababu uchumi wetu haujawahi kua mkubwa na kwamba sasa unashuka
  kulemaza inakuja kuja kuja
   
Loading...