Ni miaka 1003 sasa tangu afariki mtaalumu wa fizikia ya hesabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni miaka 1003 sasa tangu afariki mtaalumu wa fizikia ya hesabu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Yericko Nyerere, May 5, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Leo ni Jumamosi tarehe 13 Mfunguo Tisa Jamadi Thani mwaka 1433 Hijria, inayosadifiana na terehe 5 Mei mwaka 2012 Miladia.

  Siku kama hii ya leo miaka 1003 iliyopita alifariki dunia mjini Cairo Misri mwanafizikia, mtaalamu wa hesabu na msomi mkubwa wa Kiislamu Ibn Haytham.

  Alizaliwa mwaka 354 Hijiria katika mji wa Basra ulioko kusini mwa Iraq ya leo. Baada ya juhudi nyingi za kusoma na kufanya utafiti Ibn Haytham alitokea kuwa mtaalamu mkubwa wa hesabu. Mbali na fani hiyo ya hesabu Ibn Haytham alikuwa pia mtaalamu na mwalimu wa elimu za fizikia, tiba, falsafa na nyota ambapo aliweza kufanya utafiti yakinifu kuhusiana na mwanga. Miongoni mwa mambo mengine aliyoyafanya Ibn Haytham ni kuanzisha mbinu na njia mpya katika elimu ya hesabu. Ibn Haythamameandika vitabu vingi katika fani za elimu ya hesabu na tiba. Miongoni mwa athari zake muhimu ni kitabu kiitwacho "Al Manadhir" ambacho kimetarujumiwa kwa lugha ya Kingereza.
  Siku kama hii ya leo miaka 31 iliyopita alifariki dunia Bobby Sands, mwanamapambano maarufu wa Ireland baada ya kukaa katika jela ya Uingereza, kupambana na kugoma kula chakula kwa siku 66 akipigania uhuru wa nchi hiyo. Kufuatia kifo cha Bobby Sands na wanaharakati wenzake wa Ireland waliosusia chakula wakiwa jela, serikali ya kikoloni ya Uingereza ilikabiliwa na wimbi la malalamiko kutoka ndani na nje ya nchi hiyo. Aidha kifo cha mwanamapambano huyo kilizusha hali ya ukosefu wa amani huko Ireland Kaskazini. Kwa ajili hiyo Bobby Sands akatambulika kuwa bingwa wa mapambano ya wananchi dhidi ya wavamizi Waingereza huko Ireland.
  Na siku kama ya leo miaka 37 iliyopita aliuawa shahidi Majid Sharif Waqifi ndani ya ofisi ya taasisi ya Mujahidina Khalqi wa Iran maarufu kwa jina la MKO na wapinzani wa serikali ya Iran wenye kufuata siasa za Umaksi. Taasisi hiyo iliundwa mnamo mwaka 1344 Hijiria Shamsia na vijana kadhaa kwa lengo la kupambana kwa silaha na vikosi vya utawala wa Shah wakati huo. Hata hivyo baadhi ya wajumbe dhaifu wa taasisi hiyo waliathiriwa taratibu na fikra za umaksi na kuzusha mivutano ya ndani sambamba na kuwaua wanachama walioonekana kuwa na imani thabiti ya Kiislamu, kwa ajili ya kuwania madaraka katika taasisi hiyo. Baada ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran mwaka 1979, na kutokana na siasa za viongozi wa MKO za kufuata mirengo isiyo sahihi na tamaa yao ya kuwania madaraka, kundi hilo liligeuka na kuwa mpinzani mkubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Tokea mwaka 1981 taasisi hiyo iliendeleza vitendo vya kigaidi vya kuwalenga viongozi na watu kawaida mitaani. Hatimaye viongozi wa taasisi walishindwa kudumisha siasa zao za kigaidi nchini na kulazimika kukimbilia nchi za kigeni. Wananchi wa Iran wanalitambua kundi hilo kama kundi la "Munafiqina" yaani wanafiki, kutokana hiana pamoja na jinai zao dhidi ya taifa la Iran na vilevile ushirikiano wao mkubwa na dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein dhidi ya taifa hili.
   
 2. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  pamoja na kusoma kwangu phyics&mathematics mpaka chuo kikuu sijawahi kukutana na theorem yoyote ya huyu mtu,labda huko kwenye hesabu za madrasa.
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Aligundua hesabu za madrasa au?
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  hii imekaa ki mujahidina mujahidina!
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Yupo mkuu tafuta machapisho ya kale zaidi hasa ukijikita enzi za tawala za kiyunani na makuzi ya shujaa za kipiramidi!
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Zikiwemo nazo na mengineyo mengi!
   
 7. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hahaa dah mbona sijawahi kusikia wala kumsoma kwenye fizikia kweli labda madrasa
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Haahaa mkuu mimi ni muamini wa ukatoliki na nimkatoliki safi na hai!
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  @Yericko Nyerere wewe Mwalimu wa Madrasaa kwani, haya mambo magumu umejifunziaa wapi ?
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Amabo hawajamsoma na kumsikia huyo, hao ni wasomi feki. Utakuta hata hawajui walifanyalo.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo mpaka kuna "crater" ya mwezini imepewa jina lake na kuna "asteroid" imepewa jina lake kwa mchango wake katika science.

  A crater on the moon is named in his honor, as is the asteroid 59239 Alhazen.

  Abu Ali al-Hasan ibn al-Hasan ibn al-Haytham (965 in Basra – c. 1040 in Cairo) was a prominent scientist and polymath from the ‘Golden Age' of Muslim civilization. He is commonly referred to as Ibn al-Haytham, and sometimes as al-Basri, after his birthplace in the city of Basra. He is also known by his Latinized name of Alhzen or Alhacen.
  Ibn al-Haytham made significant contributions to the principles of optics, as well as to physics, astronomy, mathematics, ophthalmology, philosophy, visual perception, and to the scientific method. He was also nicknamed Ptolemaeus Secundus ("Ptolemy the Second") or simply "The Physicist" in medieval Europe. Ibn al-Haytham wrote insightful commentaries on works by Aristotle, Ptolemy, and the Greek mathematician Euclid.
  Born circa 965, in Basra, Iraq, he lived mainly in Cairo, Egypt, dying there at age 76. Over-confident about practical application of his mathematical knowledge.
  Source: ibn al-Haytham
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  peleka jukwaa la dini haya makitu..!!
   
 13. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf hebu tujaribu kuwa wenye mwono chanya, yaani nimesikitishwa na hao juu eti wamesoma hawajawahi kumwona, eti unapo soma basi kila kitu unakijuwa? maana elimu tunayo isoma itawakuza kina newton, na kuwaacha wengine. Sio kama wengine hawapo bali utaifa kwanza, hii husababisha michango ya wengine ifunikwe. elimu zetu ni za kingereza.

  Hebu tutafute bbc islam and science ali kalili alieleza vizuri na kwa undani mchango wa waislam katika maendeleo ya science na technology.

  Kuna mtu kama abdallah musa al khawarizmi anaitwa BABA wa hesabu, mzee wa algebra na mtu aliyeweza kufanya hesabu ziwe rahisi kwa kuchangia kuwa namba 123456789 na 0 ziweze kuandika namba zote duniani. Kabla ya hapo wanahesabu walikuwa wanatumia njia za kirumi ambazo zina ugumu saaaana.

  angalia tu namba hizi 22 * 4 = utapata kwa kirahisi

  sasa fanya hii XXII * IV =

  sasa kama umesoma hesabu alafu umeshindwa kujiuliza vipi wanahesabu wameacha namba za kirumi na kutumia ARABIC NUMERALS, na bado mbaguzi wa dini kwa kusema hayo ni ya madras basi weye ni bado sio msomi wa hesabu.
   
 14. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,703
  Likes Received: 2,383
  Trophy Points: 280

  helloo kilaza, we kila kitu mpaka utafuniwe na mhadhiri wako?subiri mitihani uliyokariri. mie darasa la saba nafahamu hawa watu,wewe na CHOO KIKUBWA chako huna ulijualo bali ufidhuli mtupu.elimu nizaidi ya kuhudhuria vyumba au hallhusika ndugu yangu.
   
 15. MSATULAMBALI

  MSATULAMBALI Senior Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Alhazen (965-1040?), Arab scientist and natural philosopher, who made important contributions in optics, astronomy, and mathematics. His Arab name is Abu Ali al-Hasan ibn al-Haytham. His major work, Optics, included valuable analyses and explanations of light and vision.
  Alhazen was born in Basra, in what is now Iraq. He was invited to Cairo by the Muslim ruler al-Hakim. After failing in an attempt to regulate the flow of the Nile, Alhazen feared that al-Hakim would punish him. To avoid punishment, he pretended to be insane until al-Hakim's death. He devoted the rest of his life to scientific study.
  Alhazen's most important and original contributions were in optics. He developed a broad theory that explained vision, using geometry and anatomy. This theory says that each point on a lighted area or object radiates light rays in every direction, but only one ray from each point, which strikes the eye perpendicularly, can be seen. The other rays strike at different angles and are not seen.
  In astronomy, Alhazen added to the theories of the 2nd-century astronomer Ptolemy. He also summarized or explained some of the difficult mathematical theorems of the ancient Greek mathematician Euclid.
   
 16. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mwanazuoni wa kihafidhina, ninasoma kila andiko kwaajili ya kuujenga upeo wangu!
   
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Mada umeielewa? Hii ni kumbukumbu ya mwanazuoni wa hisabati sio vingine, kwakuwa historia yake imeambatana na imani yake ndio maana tumeitaja imani yake!
   
 18. M

  MR.SILVER JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dunia ina propaganda sana..kuna mambo mengi yamefanyika na watu fulani hila hawapewi promo kama za wengine....

  Na kuna wengine walikuwa watu makini sana walitokea Africa ila tunaambiwa walikuwa wazungu..eg.New study proves it, Julius Caesar was black – and from Africa.

  Cairo kuna vyuo vingi na vya zamani kuliko ...na kweli habari nyingi za namba north africa na arabs wamechangia kiasi kikubwa.
  That the truth and I'm not a Muslim either
  [h=1]
  [/h]
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Ukisoma machapisho mengi ya kihistoria yamepotoshwa kwa makusudi tu, lengo lao ni kuwa ugunduzi ubaki kwa mzungu ilihali mengi yamegunduliwa jamii nyingine matharani watu weusi, waarabu wachina na wahindi! Mfano mdogo tu ni ugunduzi wa utengenezaji wa vyungu uliogunduliwa na mchina Fang Cha mnamo karne ya Pili katika pwani ya Macacao nchini china!
   
 20. C

  Che-lee JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana Yeriko we ni mtata sana, haya mambo mazito umesomea wapi? Mimi nilidhani wewe ni siasa tu kumbe hata mambo haya mazito hivi??
   
Loading...