Ni mgombea yupi mwenye nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu (Ubunge) jimbo la Kawe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mgombea yupi mwenye nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu (Ubunge) jimbo la Kawe?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Sep 15, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Mpaka sasa, Jimbo la Uchaguzi la Kawe lina wagombea wafuatao wa Ubunge, ambao ndio wanaosikika.


  1. Angela Kizigha (CCM)
  2. Halima Mdee (CHADEMA)
  3. James Mbatia (NCCR-Mageuzi)
  Kinyang'anyiro hiki kinaonekana kuwa zaidi kwa vyama hivi vitatu, ambapo umejitokeza ushindani mkubwa.

  Tetesi zinasema kwamba wakazi wengi jimboni wanamtaka zaidi Halima Mdee, huku nyingine zikisema kwamba huenda James Mbatia akashinda.

  Wako watu wengi wanaosema Angela Kizigha hana la kuongea, na akiwa kwenye kampeni anashindwa kuongea, anakwepa kujibu maswali anayotupiwa. Inadaiwa kwamba yeye hayuko mbali na Hawa Ng'umbi, ambaye CCM imetamka kwamba italazimika kutumia nguvu nyingi kurekebisha hali ya hewa aliyoichafua wakati alipopandisha jazba kwenye mdahalo wa TBC1, ambapo Hawa alipandisha jazba na kumjibu mwandishi wa habari aliyemwuliza maswali kuhusu tuhumba mbali mbali dhidi yake.

  Ningependa kupata maoni yenu. Nani atashinda?

  Asanteni.

  -> Mwana wa Haki
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wewe ambaye uko katika eneo hilo wasemaje kwanza?
   
 3. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  siyo la kuuliza hili....
  ubungo=Mnyika
  kawe =Mdee
  nimesahau kigambo = mama yangu Matilda Komu
   
 4. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mimi naona Halima atashinda lakini Mbatia naye ana hoja zake za msingi. Ndio maana nikaulisaaaaaa!
   
 5. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Angela Kizigha hajulikani. Mwenye taarifa zake azilete tumjadili. Hana skendo kweli huyu? LOL
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  jamvi la wakubwa. (maybe)
   
Loading...