Ni Mgombea yupi atapoteza maisha kabla ya Jumapili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Mgombea yupi atapoteza maisha kabla ya Jumapili?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mbea, Oct 25, 2010.

 1. m

  mbea Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  • Posted by GLOBAL on October 25, 2010
  [​IMG]
  Na Issa Mnally
  Hali ya Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ali Omar Juma ikielezwa inarejea vizuri, kiwewe kinatawala kuhusu anayetajwa kufariki dunia kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010.

  Ingawa wagombea wenyewe hawaoneshi kutetereka kwa namna yoyote kutokana na tishio la mmoja wao kufariki dunia, lakini uchunguzi unaonesha kuwa swali la ‘nani atakufa' linasumbua ubongo.
  [​IMG]
  Dk. Slaa (CHADEMA)
  Tayari imekwisharipotiwa kwamba baadhi ya Watanzania walikata tamaa mapema, tangu waliposikia utabiri kuwa mwaka huu hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu kwa sababu mmoja wa Wagombea Urais mwenye nguvu atafariki.

  Mnajimu alwatan barani Afrika, Sheikh Yahya Hussein ndiye sababu ya sakata hilo kupitia utabiri wake na katika mazungumzo na gazeti hili Ijumaa iliyopita alisisitiza kwamba siku zimebaki chache lakini mgombea mmoja ataaga dunia.

  Sheikh Yahya aliliambia Ijumaa Wikienda ‘The Biggest IQ Paper' kuwa ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ijiandae kuhairisha uchaguzi kwa sababu macho yake yameona na yana uthibitisho wa kifo cha mmoja wa wagombea.
  [​IMG]
  Hashim Rungwe (NCCR-MAGEUZI)

  Alisema, anachokifanya yeye ni kutabiri kwa kufasiri nyota lakini siyo uchawi kama ambavyo wengi wamekuwa wakiamini.

  "Huu ni utabiri siyo uchawi, siku bado zipo, kwahiyo tungoje siku kati ya hizi chache zilizobaki, yatatimia tu niliyoyasema," alisema Sheikh Yahya.

  Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa utabiri wa Sheikh Yahya ni mtihani kwa taifa kwa sababu ngoja ngoja inatia kiwewe.

  "Sisi wananchi tunawaza sana, labda nisiwasemee watu nijiseme mimi mwenyewe, nina mawazo mengi kusema kweli," alisema Faustine Kimadao wa Boko, Dar es Salaam katika mahojiano yaliyofanyika Kituo cha Daladala, Mwenge.

  Kimadao alisema: "Watu ambao tunaamini katika siasa, hii inatugusa sana, tunaweza kudharau ya Sheikh Yahya lakini tukumbuke kwamba mwaka 2005 alitabiri na ikatokea.
  [​IMG]
  Jakaya Kikwete (CCM)
  "Alisema Rais Mkapa (Benjamin) ataongezewa muda wa kutawala kwa sababu uchaguzi utaahirishwa na kweli ikatokea. Tuyatazame haya katika pande mbili, binafsi nina hofu."

  Mtanzania mwingine, Bora Steven katika mahojiano hayo alisema kuwa mwanzoni alikuwa anapuuzia lakini siku zinavyokaribia anaanza kupata mchecheto kwa sababu kuna alama za huzuni.

  "Kwa vyovyote vile, mgombea yoyote wa Urais akifariki ni maumivu kwa taifa, kwa kuanzia kuangalia chama chake, wafuasi na gharama ambazo nchi itaingia baada ya uchaguzi kuhairishwa," alisema Bora.

  Aliongeza: "Tunamuomba Mungu atuepushie kwa sababu Sheikh Yahya ametabiri tu lakini mwisho wa siku, Mungu ana nafasi kubwa ya kuamua kinyume chake."
  [​IMG]
  Ibrahim Lipumba (CUF)
  Maoni zaidi
  Khatib Mitea, muuza mafuta, alisema: "Mimi kwa mtazamo wangu Sheikh Yahya katabiri lakini akumbuke kuwa yeye sio Mungu, sidhani kama itatokea kwa mtazamo."

  Salum Nassor, dereva taksi alisema: "Sheikh ni haki yake kutabiri lakini atambue kuwa Dini ya Kiislamu inasema utabiri ni dhambi, mimi nawafuatilia sana hawa wagombea wa Urais mpaka sasa sidhani kama kuna mgombea atakufa."

  Majaliwa Robert, muuza vocha Bamaga, Mwenge: "Mimi kwa upande wangu namwamini sana Sheikh Yahya, nawataka Watanzania wakae chonjo. Unakumbuka mwaka 2005 alitabiri uchaguzi utahairishwa na ukahairishwa kweli."

  Khatibu Idd, alisema: "Siwezi kuamini kama mmoja wa Wagombea wa Urais atapoteza maisha, kwa mtazamo wangu yule mtabiri alikuwa anawatisha tu Watanzania wasijitokeze kuchukua fomu."
  [​IMG]
  Mugahywa Muttamwega (TLP)
  Thomas Maganga: "Mimi sipendi sana kuamini mambo hayo ya utabiri, lakini yule Sheikh ni mtabiri wa Kimataifa nawataka Watanzania wenzagu tusubiri tuone kile kitakacho tokea."

  Upande mwingine, baadhi ya wananchi wameeleza hofu yao kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Freemasons kuichagulia Tanzania Rais.

  "Tunasikia Freemasons wakimtaka mtu fulani ndiye ashinde Urais basi atashinda na yule wasiyemtaka hatapata kitu, kwahiyo tunaogopa hilo," alisema Halima Jaffar wa Ubungo, Dar.

  Mkazi wa Kinondoni, Jadu Kitani alisema kuwa tishio kwamba nchi nyingi marais ni Freemasons ndiyo linafanya ahisi wanaweza wakasimika mtu wao Tanzania.

  [​IMG]
  Peter Kuga Mziray (APPT-MAENDELEO)
  "Mimi sijui kama kuna mgombea yoyote wa Urais ni Freemason lakini najua wanataka kuitawala dunia, kwahiyo inawezekana kabisa wameandaa mtu wao. Mungu asaidie washindwe," alisema Jadu
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Biashara ya kuroga watu kwa kutumia majini na vibwengo ni kunadi biashara ya huyo mchawi wa mchana - Yahaya. Hafai kabisa na ashindwe kabisa!! Watanganyika hatuna wasi wasi maana huo ni uzushi wa mchana. Mbona yeye hajajitabiria afe. Alipougua alisema kunawatu wanasali ili afe! Muoga wa kufa yeye alafu analoga wengine. Kuna ulinzi wa damu ya Yesu Kristo Tanzania hii. Anaua watu anasingizia utabiri kutimia. shame on him.
   
 3. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Wakati anaejiita mnajimu bw sheikh yahya hussein amelitangazia umma mh mmoja(MGOMBEA URAIS) maarufu atakufa kabla ya tar 31 oct watanzania wanazidi kuona na kusubiri aibu hii ya mnajimu atakayokumbana nayo...
  wakati kila mgombea alijitahdi kwenda kuomba maombezi ya kuhifadhiwa watumishi wa mungu wamemtangazia sheikh yahya si MUNGU na kama alikuwa anacheza na nyakati za watu muda wake umeisha

  wengine walidiriki kusema kama yeye amwamini mungu basi niwakati muafaka kuamini MUngu alie hai na kuachana na mapepo anayokimbizana nayo kila siku.......

  6DAYS LEFT
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hahahaaa! we humjui sheikh Yahya. Huko "kufa" atakutolea tafsiri mpaka utashangaa! Atakwambia kwamba hakumaanisha 'kufa' physical bali ni kufa kisiasa/ kushindwa katika uchaguzi/kura. We subiri uone!
   
 5. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  kwani huyu mtu si nilisikia amelazwa yu mahututi? vp amepata nafuu.... any way muulizeni utabili wake wa kwamba simba haitachukua ubingwa wa vodacom 09/10 ulikuwaje?
   
 6. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Aisee nimemuona kwenye tv awezi ata kuongea ananyosha mkono mkewe kadada kamoja binti yake kabisa ndio anawadanganya watu nyota zao......akifanaya mchezo na mungu atawah yeye shauri yake
   
 7. M

  MTOKAJASHO Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kusikitisha na kustaajabu umma wa Watanzania aliyotabiri sheikh Yahaya yanaelekea kutimia.

  Mnajimu huyu ambaye anafahamika na wengi Tanzania na Afrika kutokana na utabiri wake unahisiwa huwa unatimia na wengi.

  Hali ya Rais wa sasa wa Tanzania inazidi kudorora na wataalam wa maswala ya afya ya siasa wametanabaisha kufariki tarehe 31 mwezi oktoba kwa mgombea huyo wa chama kilicho tawala kwa miaka takribani 49 pale uma wa watanzania utakapo mpatia kura ya Hapana.
   
 8. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Nakushauri kichwa cha habari ukiweke kwa wakati ujao vinginevyo unapotosha wana JF
   
 9. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Duh! This is too much!
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  mmmh !
   
 11. M

  MTOKAJASHO Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani sheikh yahaya alipokuwa anayasema haya alijua hali itakavyokuwa wewe hutaki kuuamini ni ndugu yangu Agustino. Huhitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu kuliona hilo limetimia.
   
 12. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  He meant the incumbent President will be ousted! Haha!!!!
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  atakutupia jini mahaba wewe - shauri yako!! huogopi - ha ha ha

  Mwenzio anamuongezea ulinzi wewe unasema mgonjwa anafariki tarehe 31 Oct.
   
 14. E

  Erica85 Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi hili swala linanitatiza,
  sijapata maeleao ya kunifanya nikaielewa hii mada, nimekuwa nikiisikia juu juu tu. Naomba mwenye kuielewa anijuze tafadhali
   
 15. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari kinaonyesha tukio limeshatokea wakati wewe unamaanisha litatokea 31/10/2010. Suppose 31/10 ikanyesha mvua ya mawe na wasijitokeze watu kupiga kura....
   
 16. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sometimes you ask yourself if some of the messages on this forum reflects the Slogan of "The Home of Great Thinkers"

  Just thinking aloud!
   
 17. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hukumwelewa mnajimu
   
 18. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  2005 alitabiri TZ itapata raisi mwanamke, utetezi wake ukawa raisi tuliyenae na sura ya kike. Ina maanda utabiri wake una maana pana zaidi ya binadamu kufariki. Inawezekana Prof. Lipumba atatangaza kuwa hatakaa agopewe tena uraisi
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hapo mi sisemi natuone yatakayojiri.
   
 20. B

  Banika New Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Kama kampeni zitahitimishwa uwanja wa jangwani kama ilivyo desturi, utabiri wa shekhe yahaya utamuangukia mzoefu wa kuanguka, na safari hii akianguka ni moja kwamoja hainuki tena
   
Loading...