Ni mfumo upi wa uzalishaji mali unaowafaa watanzania kwa sasa?

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
1,571
873
Bila kuangalia vipengele vidogo vidogo vya mifumo ya uzalishaji mali, ipo mifumo mikuu miwili; yaani Ujamaa na Ubepari. Kutokana na maendeleo ya dunia imedhihirika sasa hakuna mfumo ambao unaoweza kujisimamia ukaleta tija kwa taifa lolote lile. Matokeo yake umezaliwa mfumo mwingie ambao ni uchumi mchanganyiko( Mixed economy). Katika uchumi huu, tofauti zilizopo kati ya nchi moja na nyingine ni viwango vya mgawayo ya uwekezaji. Nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya uwekezaji wake inashikiliwa na umma na serikali tunaweza kuiita nchi ya kijamaa na hivyo hivyo, nchi ambayo asilimia zaidi ya 50 ya uwekezaji wake inashikiliwa na watu binafsi, serikali inamiliki sehemu ndogo iliyosalia tunaweza kuiita nchi ya kibepari.

Katika mazinga haya inajitokeza misingi mingine miwili ambayo inatumiwa na mifumo yote ya uzalishaji mali, ambayo ni nguvu ya soko na bei elekezi. Nguvu ya soko hutumika kupanga bei za bidhaa na huduma ili kuongeza ufanisi na kuleta ushindani unaomnufaisha mlaji wa kawaida. Bei elekezi hutumika kwa bidhaa na huduma ambazo zikiachiwa huria zinaweza kufifisha uchumi wa jumla na kuleta madhara kwa watu wengi.

Ki msingi ubepari ulitafsiriwa vibaya kwa kuuhusisha na unyonyaji uliokithiri na kwa watanzania ubepari uliitwa unyama; badala ya mfumo wa uzalishaji mali unaotegemea mtaji wa raslimali fedha ( capital intensive). Ninasema ulitafsiriwa vibaya kwa maana, kila mfumo wa uzalishaji mali unahitaji ziada kati ya mtaji uliowekezwa na gharama za uendeshaji. Tofauti au ziada hiyo huitwa faida, ambayo hutozwa kodi na serikali. Kiasi kinachopatikana hutumika kuendeshea serikali na kutoa huduma za kijamii kwa watu wote.

Vile vile msingi wa ujamaa upo katika umilikaji wa mtaji hata kama mtaji unaosemwa ni raslimali watu au ni wa serikali. Ili uwekezaji uwezekuendelea, ziada au tofauti kati ya mtaji na gharama za uendeshaji ni lazima. Usipofanya hivyo mradi utakufa. Sisi tuliokuwepo enzi za viwanda vya serikali, maduka ya vijiji, miradi ya halmashauri za wilaya, makapuni ya uchukuzi ya mikoa, Makapuni ya biashara ya mikoa,nk, suala hili linaeleweka sana. Katika mazingira haya ya uwekezaji kodi ya serikali ni lazima.

Ninaomba ieleweke, hakuna mfumo wa uzalishaji mali usionyonya! Baada ya maelezo hayo ya kina, je, Tanzania itumie mfumo gani wa uzalishaji mali kati ya ujamaa na ubepari? Tukichagua ni mfumo upi unatufaa, tutaacha kuwaona wawekezaji binafsi kama watu wa baya. Ninaziona dalili za kuanza kuwachukia walionacho na baya zaidi kuwachonganisha wasionacho na walionacho bila kujali walionacho wamekipataje?
 
Back
Top Bottom