NI MTAZAMO TU
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 1,203
- 998
WanaJF ninaleta kwenu iwe faida kwangu na kwa wadau wengine.
Wengi wetu tuna ndoa haijalishi mama ni mfanyakazi au lah ila majukumu ya familia yanamuhusu baba, kikubwa kilichozoeleka baba ndio mkuu wa nyumba.
Hoja yangu ni mfumo upi unapaswa kufuatwa katika kuacha matumizi ya ndani?
Namaanisha kuacha kila siku pesa ya matumizi; mfano, elfu kumi au tano kutegemea na kipato na ukubwa wa familia, au kumwachia mwanamke pesa ya mwezi mzima, ili ikiisha mwanaume atakuwa hapo hahusiki.
Nyumba nyingi zimeingia katika shida kubwa sana, mwanaume mwingine utasikia nilikuwa naacha pesa ya matumizi kwa mwezi, ila ikawa haifiki mwisho wa mwezi mwanamke anadai pesa imekwisha, na kumwingiza kwenye mipango mipya ya kutafuta pesa ili kuifikisha familia hiyo mwisho wa mwezi.
Na mwishoe kuepuka hilo wengine huamua kutoa pesa ya matumizi kwa kila mwezi kwa kupanga kiasi.. Wengine 5,000 , 10,000 kutegemea na kipato na ukubwa wa familia.
Naomba mchango wenu wadau. Wengine sisi wachanga kwenye ndoa tunahitaji kujuzwa na wazoefu.