Ni mchakato gani unatumika wa kuwapata washiriki wa Olympic hasa hii ya London??

cement

JF-Expert Member
May 5, 2012
581
218
Na sema hvy coz tumeona nchi kama Jamaica kule mpaka Bolt akapata mpinzani!kuna na juhudi za mapema kabisa za kupata washiriki wenye viwango vya hali ya juu,sijajua sisi inakuwaje kila mara tunapata aibu tuu mbn wafukuza upepo wapo tena wa hali ya juu tu,waogeleaji wapo tunaona mtu anaogelea kutoka ferry hadi kigamboni fasta tu hawa si ndo wakuwapa mazoezi ina maana HAKUNA kabisa Tanzania watu wenye viwango hvy??zamani wkt nasoma shule jamaa wa mita mia walikuwepo na walikuwa wanakimbia sanaaaa sasa hebu Filbert Bayi atwambie watanzania anafanya fanya vipi mpk anapeleka watu wabovu na wachache kiasi kile???kuna nn au hz nafasi pia ni za kindugu ndugu??Filbert Bayi tuambie watanzania maana yaani warusha hata tufe hawapo Tanzania??hapana kwa hili Kuna mcheo mchafu hapa!!!!wahusuka fungukeni!!!!
 
lower GDP make people get less time for sports, may be, i dont know!!!
 
Ukiangalia takwimu utaona kwamba Tanzania imekuwa ikipunguza idadi ya wanamichezo wake kushiriki mashindano hayo kutokana na uhaba wa fedha na maandalizi mabovu.

Tokea Tanzania ianze kushiriki mashindano hayo ni mwaka huu imetokea hakuna timu hata ya judo, table tennis, volleyball, netball, basketball, waendeshaji baiskeli, ubebaji vyuma, na mbio fupifupi kama mita 200 na michezo mingine midogomidogo.

Nafikiri tatizo ni uhaba wa fedha na ukosefu wa ubunifu wa vyanzo vya fedha hizo. Kamati ya olympic inaweza kabisa kutafuta wadhamini (sio wafadhili) ambao watakuwa wakisaidia kugharamia wanamichezo kwa kujenga vituo vya kujifunzia (facilities) michezo hiyo na kufadhili safari za wanamichezo wanapokwenda kufanya majaribio na sio lazima Ulaya bali katika nchi hata za jirani.

Pia kamati hiyo haifahamiki kama inasaidia vipi ukuzaji wa vipaji mashuleni kwa kuchagua wanamichezo wanaoonyesha uwezo mkubwa katika mashindano ya ngazi ya UMISHUMTA au UMISETA katika maeneo yote niliyoyataja hapo juu.

Lakini kikubwa ni ubunifu wa vyanzo vya mapato maana hata shirika la bahati nasibu linaweza kuchangia mfuko wa Olympic kwa kutoa sehemu ya mapato yake ambayo kama mchezo wa bahati nasibu ukibuniwa upya unaweza kulipa shirika hilo mapato makubwa na likawa linasaidia maeneo kama haya ya michezo.

Pia kamati hiyo ingeweza kuhamasisha wananchi wawe wanapenda michezo mingine na sio Simba ya Yanga tu kwa kubuni hata fulana tu au badge na kufungua kaduka fulani hivi ambacho katauza vitu vinavyoshabihiana na masuala ya olympic.

Sasa kuna watu wamo humo kwenye kamati miaka nendarudi na hakuna kitu.

Ni ubunifu tu na kutumia akili.
 
Timu ya Tanzania iliondoka ikiwa na jumla ya wachezaji 6, makocha 3, mkuu wa msafara 1 = watu 10. haitoshi, viongozi wengine nao wa toc wamekwenda kujumuika na timu huko kama sikosei viongozi wa4 hivi, akiwemo na mwenyewe Filbert Bayi, sasa hapo uwiano uko wapi? Ukiwauliza kwa tumekuwa na ushiriki wa wanamichezo wachache watakwambia fedha haitoshi, ila ya wao viongozi kwenda kutalii inatosha! Na wanakula bata si mchezo, tee tee tee tee
 
Back
Top Bottom