Ni mbinu gani unaweza kukabili wivu wa kimapenzi endapo mpenzi ataingia kazini masaa 12 bila simu?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,801
Ni mbinu gani mtu unaweza kuikabili kushinda wivu wa kimapenzi endapo mpenzi wako akiwa ameingia kazini basi anatakiwa kutotumia simu kwa masaa 11 au 12?

Nauliza hivi kwakuwa kila binadamu ameumbwa na silika yake ambapo kuna wengine kwa aina ya upendo ulioshikamana na wivu uliokubuhu hawawezi kukaa muda mrefu bila ama kuwasiliana kwa simu na mpenzi wake au hata kuchati nae na unakuta huyo mpenzi wake anafanya kazi katika kampuni ambayo ukiingia tu ofisini simu zote zinazimwa na zinawekwa mahala mpaka jioni akitoka.

Kwa walio wa wivu wa kupitiliza kwa wapenzi wao hapa mtaweza kuwasaidiaje wana jamvi?

Karibuni.
 
Vumilia tu tayari ushajua ni masharti ya kazini kwao. Kama sio basi jua huna chako
 
Kama ni Mwanamke/Mke wangu akipewa hayo masharti, basi na hiyo kazi aiche kuanzia siku ya sharti hilo.

Mwanaume pekee Mtanzania asiye na wivu ni Naseeb Abdul.
 
Mkusanye mtaji mfungue Duka kubwa mkae wote muangaliane mpaka jioni Ila Kama anataka kuliwa ataliwa Tu!
Na wivu utakwisha siku ukijua analiwa!
 
Vumilia tu

Kama ilipangwa akusaliti atakusaliti hata simu ikiwa on 24/7

Jaribu kuishi kwa imani kuwa muda aliozima simu hakuna baya analofanya(Fanya kwa ajili ya amani ya moyo wako)
 
Mkuu mbinu kuu hapo ni kutulia tu na maisha yaendelee..ukimzuia itakuwa tabu kazini kwao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom