Ni maziwa gani mazuri kwa watoto wachanga wa chini ya mwaka mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni maziwa gani mazuri kwa watoto wachanga wa chini ya mwaka mmoja

Discussion in 'JF Doctor' started by MAKALA, Aug 16, 2010.

 1. M

  MAKALA Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hi
  kuna taarifa nimeisoma michuzi kua leo TFDL wametangaza kua maziwa ya s26-gold na mengineyo ni feki yanasababisha watoto kuugua ini na figo so naomba ushauri kama kuna mtu ambaye anajua ni maziwa gani hapa kwetu ambayo kwa sasa yanafaa nikimaanisha hayajaanza kufojiwa,tafazali naomba nisaidiwe.
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,955
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Ya Ng'ombe!
   
 3. M

  MissKitim Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SMA Gold , ni mazuri. Ila kopo ni 25,000/=. Maziwa ya ng'ombe hawashauri watoto chini ya mwaka mmoja labda uchanganye na maji.
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwaujumla maziwa ya ng'ombe hayafai kwa mtoto chini ya mwaka mmoja, one of the reason ni kwamba yanacontent ndogo saana ya iron. Km huko ulipo unaweza kupata SMA au Cow & Gate ni mazuri saana kwa watoto.
   
 5. K

  KiparaDar Member

  #5
  Aug 18, 2010
  Joined: Mar 20, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Tumia Cow and Gate,lutoka london nadhani yanapatikana shoppers plaza supermarkets only.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  Kwa Ushauri wangu ikiwa Maziwa Mazuri ni ya Mama Mwenyewe aliyezaa mtoto ikiwa kama mama Mzazi maziwa yake hayatoki hapo ndipo kuna uwezekano wa kutumia maziiwa ya Kopo. Lakini ni vizuri zaidi Kutumia maziwa ya mama mwenyewe aliye zaa mtoto kuliko kutumia maziwa ya kopo. huo ndio ushauri wangu.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  Maziwa ya kopo ni hatari kwa watoto wachanga’

  Fredy Azzah
  WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewataka kinamama kuepuka kuwapa watoto wao maziwa ya kopo isipokuwa pale watakapokuwa wameshauriwa na daktari kwa sababu yana athari za ubongo, ukuaji na mengine ni sumu.

  Amesema maziwa mengi ya kopo ni hatari kwa afya za watoto wao hivyo akahimiza kuzingatia zaidi utaratibu wa kunyonyesha.

  Alitoa rai hiyo wiki hii Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuwahamasisha wanawake kuwanyonyesha watoto maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwazo.
  Katika hotuba hiyo ya Profesa Mwakyusa iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bilandina Nyoni kinamama wengi huamasishwa na matangazo ya maziwa hayo ambayo aliyaelezea yanatoa taarifa zisizo sahihi.

  “Usambazaji holela wa maziwa ya unga na vyakula vingine vya watoto ni changamoto. Maziwa mengi hayana ubora na baadhi ya matangazo ya biashara yanapotosha hivyo wanawake wanajikuta wakiwapa watoto wao sumu,” alisema.
  Hata hivyo, alisema serikali inaendelea kudhibiti uingizwaji wa maziwa hayo hapa nchini kwa kuwabana wafanyabiashara wanaoyapitisha njia za panya.
  Profesa Mwakyusa alisema takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia 41 tu ya wanawake nchini wanaonyonyesha watoto wao kama ilivyopendekezwa kitaalamu.
  Alisema baadhi ya wanawake huanza kuwachanganyia watoto wao maziwa na vitu vingine baada ya miezi miwili tangu wazaliwe.

  “Takwimu zinaonyesha kwamba, kwa watoto wenye umri chini ya miezi miwili kiwango cha unyonyeshaji maziwa ya mama pekee ni asilimia 70, wenye miezi miwili mpaka mitatu kiwango cha unyonyeshaji ni asilimia 42.3 huku wenye miezi mine mpaka mitano; kiwango cha unyonyeshaji kikiwa asilimia 13.5,” alisema.

  Alisema, athari za kuwachanganyia watoto wenye umri huo maziwa kinaathiri ukuaji wa miili na ubongo wao na pia uwezo wao wa kufikiri.

  Mbali na madhara hayo, alisema baadhi ya maziwa ambayo hayana viwango yanaweza kuwa sumu kwa watoto na hata kuwasababishia magonjwa yanayoweza kusababisha kifo.

  “Usambazaji holela wa maziwa ya unga na vyakula vingine vya watoto ni changamoto. Maziwa mengi hayana ubora na baadhi ya matangazo ya biashara ya maziwa haya yanayotolewa yanapotosha hivyo wanawake wanajikuta wakiwapa watoto wao sumu,” alisema.
  Naye mtaalam kutoka taasisi ya chakula na lishe Neema Joshua alisema kinamama wanaofanya kazi sehemu ambazo hawawezi kwenda na watoto wao wanapaswa kukamua maziwa yao na kuyaacha nyumbani ili motto anyweshwe.

  Source: ?Maziwa ya kopo ni hatari kwa watoto wachanga?
   
 8. H

  Haika JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kama mtoto ana mama yake, (hajafariki) maziwa ya mama ndo mazuri jamani!
  mbona mnahit around the bush?
  Nyie mnajibu swali, maziwa gani ni mazuri wakati mama wa kunyonyesha hayupo!!


  Mama anaweza kukamua maziwa yake na kuyaacha saa 24 bila kuharibika bila kuweka kwenye friji, mradi pawe mahali pamepoa tu.
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  maziwa safi ni ya mama mwenye mtoto tu
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Jana nimemuanzisha mwanangu ziwa la ng'ombe
  kwa kuwa TFDA walipita jiji lote kuondoa maziwa ya kopo madukani.
  tatizo la TFDA wanatibu tatizo bila ya kutoa kinga na njia mbadala
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  siwa elewi wote munaopinga maziwa ya ng'ombe wetu wakienyeji na kufumbatia maziwa yaliyoprocessiwa nawakati mwingine sio maziwa halali. Natoa mifano michache tu lakini huo ndio ukweli angali watu wengi wanaotoka kanda ya ziwz wanaafya sana na miili yao ni mikubwa kwa walio wengi maziwa haya hayana matatizo ni jinsi ya kuyatumia tu. yaani kuchemsha na kuongeza maji kidogo na vyakula vingine vya asili. tusiwe watumwa wa mataifa ya nje
   
 12. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br /
  kweli mkuu maziwa yamama mtoto ni bora zaidi.mengine ni mumbwebwe na madoido ya ulimbukeni kwa kutotaka kuwanyonyeshawa watoto.Je watoto wamezaliwa na makopo uwape maziwa ya kopo au ngombe na mbuzi.Mbona wanyama wanyonyeshao awana tatizo hilo liwe kwa binadamu .madhara ya hao makopo ni kunenepeana mtoto miaka 3 kilo 15 wajisifu afya
   
 13. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maziwa ya mama ni bora zaidi mradi tu yakamuliwe na kuhifadhiwa katika chombo kisafi.
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Maziwa ya ng'ombe ni kwaajili ya ndama ambao ni herbivores! Maziwa ya mama ndio mazuri kwa mtoto wa kibinadamu ambaye ni omnivore!

  Kama kwa sababu zilizo nje ya uwezo then ongea na wataalamu wa afya ambao wanajua formulae inauomfaa mtoto wa umri huo! Usidanganyike na brand names na mabei ya ajabu; kwa kwetu lactogen imekuza watoto wengi tu!
   
 15. s

  shosti JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kamua maziwa yako,hifadhi kwenye chombo...usafi uzingatiwe!
   
 16. Glue

  Glue Senior Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  What if mama ni muathirika wa HIV? Si atamwambukiza mtoto?
   
 17. The great R

  The great R Senior Member

  #17
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TFDL au TFDA?
  Anyways me nampa NAN bado ni mdogo ila ana afya sana. Jaribu,kuhusu kufojiwa cjui kwakweli.
   
 18. S

  Sharp lady Senior Member

  #18
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kumdi lipo facebook linaitwa "Bongo real mamaz" omba kujiunga utapata ushauri mzuri sn wengi wao wana experience nzuri na wako very active.
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Lactogen 1 toka france vip jamani,maana kuna mshikaji nimekuta anampa mwanae wa kiume as anamnyonya mamae mpaka anapata kizungzungu wameamua iyo iwe supplementary dose!
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hbu nyonyesha mtto huko.................vp unaogopa yatalala mapema ama?
   
Loading...