Ni mazingira gani hatari uliwahi kujisaidia haja??

CCNP Engineer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
463
1,286
Cheki Hii:
Mwaka 2010 nimeenda kuripoti form five Ilboru Arusha....
Kesho yake nikasema ngoja niende nikazurure town niijue Arachuga ikoje...

Basi, asubuhi baada ya kunywa uji wa Shule huyoooo nikashuka barabara ya mianzini pale, vuka barabara (ya kwenda Moshi) ongoza mjini.. Sitaki kupanda daladala sitofaidi mji vizuri.

Si unajua tena ukishakunywa uji mwingi asubuhi na kile ki baridi baridi, wakati niko mitaa flani karibu na makaburi hivi, mkojo ukanibana kinyama (mjini hapo ujue)

Angaza huku na huko sioni public toilet, sioni Baa wala Msikiti......
Nikavuta picha nikimbie kuitafuta Stand ya mabasi ilipo ni mbali sanaa....

Nikasema niulize watu...
Nikaona uchuro huu, kwanza nitaonekana mshamba sana, mgeni wa mji. Na navosikia Arachuga wahuni wengi wanaweza kunikaba. Nikasogea kwenye mwembe karibu na makaburi fungua zipu nikaanza kukojoa chororororo.....

Khaaaa.... Hata sijamaliza nashangaa watu watatu wamevaa makoti hawa hapa...
Mmoja katokea huku, mwingine kule....
"We dogo, unachafua mazingira hujasoma hilo bango hapo??"
"nisamehe blaza nilizidiwa"
"Umetokea wapi wewe.... Afande huyu aende kituoni akalipe 50,000 fine"
"Nimetokea shule Ilboru"
"wewe mwenyeji wa wapi?"
"Shinyanga..."
"Sasa dogo, hapa hawaruhusu kukojoa, twende kituoni ukajieleze ulipe 50 hiyo uondoke zako"

Daaah
Jamaa walinikaba pale ikabidi niwatoe buku 8 kubabake ndio wakaniachia...
Kwa jinsi nilivopanic + ugeni mji wa watu+ hofu ya wavuta bangi Arachuga+ ni kweli kosa nimefanya Nilisahau hata kuwaomba nione ID zao kama ni maafande kweli...

Nyingine:
Niliendaga likizo Mwanza kwa mjomba. Sasa choo cha nyumba kipo nyuma ya nyumba.
Usiku ukitaka kutoka lazima ufungue mlango wa mbao, then Geti mlangoni kisha ukafungue geti la kwenye fensi ndipo uzunguke chooni.. kote hapo ni makufuli tuu...

Ebana siku moja night kali mkojo huoooo... Mavi hayooooo....
Kuanza kufungua mageti mpaka kufika Toy hapana, it was too late..
Nikachukua mfuko wa lambo, nikanya mle nikaufunga nikarudi nao chumbani.
Nakumbuka chumba kilikua kinatema kubabake...

Kisha asubuhi mapemaaa nikawa wa kwanza kutoka nje, nikazuga naenda kupiga mazoezi pale Thaqaafa Secondary.......
Nikafika mitaa ya Lake Secondary nikayatupa yale mavi hukooo nikarudi...

Ya mwisho hii hapa:
Tabora (Mboka Manyema) maeneo ya Mwinyi Kisarika kule chini...
Palizuka tabia ya vibaka kudumbukia nyumba zenye fensi na kuiba chochote ndala, ndoo, viti....
Kwa kujihami walikua na desturi ya kuingia na Nondo. ukimzingua ukajifanya unatoka kumu attack na yeye anakupiga nondo ya kichwa anaruka ukuta anasepa zake..

Baada ya tabia hiyo kupamba moto, ikabidi tuwe na tahadhari.
Ukitaka kwenda kulala kakojoe kabisaaa mkojo wote uishe, maana kutoka tena nje ni asubuhi..
Bana siku moja tulikula sana matikiti maji, wacha mkojo unibane usiku..
Nani atoke nje ale Nondo ya kichwa!!!

Palikua na jagi la maji ya kunywa, nikachukua nikakojolea chorororo...
Nikalala. Asubuhi mapema sana, toka nje, osha sana jagi kwa sabuni.
Maisha yakaendelea.

Je wewe.... Huna ka story kama haka... Karibu
 
Tumekunywa pombe wee Rocky City huko. Usiku kabla hatujalala jamaa kanionyesha choo ni huku. Usiku mkojo umenibana, nikatumbukia chumba wamelala na wife, si unajua pombe kumbukumbu zinapotea.
 
Kwenye basi dreva alidinda kusimamisha gari, mimi dirishani mkojo, chorooooooo zipu wapi ,ngada,safari ikaendelea
 
Haukumkojolea mtu wa seat ya nyuma..
Maana gari inakimbia mkojo lazima urudi nyuma kwa ule upepo...

Ulikua seat ya nyuma kabisa nini!!

Hukuona aibu wanawake!!
Nilibendi tumbo na mshubebe mbele ukawa unatoka kwa kasi. Sikusikia kelele zaidi ya vicheko na hongera nyingi.
Japo nilikuwa fm5 sikuona noma. Nilifikiria aibu zaidi ni IPI kati ya kujikojolea na kukojoa dirishani? Nikachukua hatua sahihi
 
Back
Top Bottom