Ni mawaziri wabovu alio nao Raisi na sio Raisi mbovu

jogijo

JF-Expert Member
Mar 29, 2019
260
490
Wakuu habari, niende kwenye mada moja kwa moja, ni kwa muda sasa nimekua nikiona namna mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavohangaika na tengua teua hizi kila kuchwao. hapa juzi nikajua kumbe Tanzania tunae Raisi mzuri sana kwa vigezo vyangu nilivokua navyo wakati napambana kumtaftia kura mh. Lowasa.
Mh Rasisi ako na uthubutu wa hali ya juu sana, ila tatizo ni mawaziri alio nao, either wanamwogopa kiasi kwamba hawamshauri uhalisia uliopo, au wanajipendekeza ili kupendwa kwa kumpaka mafuta kwa mgogo wa chupa. Hapa kati nilisikia Kabudi anavosema katolewa jalalani, nikajiuliza hivi Waziri kama huyu anaweza akarisk tumbo lake kwa maslahi ya nchi? na nimekuwa nikiona mawaziri wengi wanavopambana kuisifu serikali kwa kutetea matumbo yao (Mwijage) mwisho wa siku akatenguliwa na ugali ukaishia pale.
hivo hata hivi vikao anavokaa Raisi na wadau mbali mbali anakua hajashaurian ana mawaziri wahusika ndio maana baada ya kikao ni lazima kuna mtu anachomoka nae. ninaamini kabisa Raisi akipata mtu wa kusimama katika kweli anaweza fanya vizuri sana.
Kwenye eneo la democrasia hakuna waziri anaeweza mshauri Raisi kulingana na uhalisia, huyu Lugola na kujipendekeza kule anaweza kweli kukohoa mbele ya Raisi kwa kumwambia mheshimiwa hili halifai na hili linafaa...

Nirudi kwako mh. Raisi, tafadhari bora uteue viongozi unaoona wana uwezo wa kukucriticise mkiwa kwenye vikao vyenu kuliko watu wa kupokea maagio na kusema yes sir, criticism zitakuumiza lkn zitakuponya sana.
asante...
 

Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    7.5 KB · Views: 15
Back
Top Bottom