Ni matumaini yangu wana CHADEMA wote si tu mmemsikia bali mmemuelewa vyema tu Kada wa CCM Pascal Mayalla

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
" Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla

Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.

Najua hapa JamiiForums kuna wana CHADEMA wengi tu na wale walio Neutral kama Mimi Krav Maga hivyo kwa pamoja ama tutaweza Kukubaliana nae au Kumpinga kwa Hoja.

Na wakati mnamjibu mwana CCM Pascal Mayalla kumbukeni kuwa huyu ni Msomi wa Fani nyingi nchini Tanzania za Habari na Sheria, Mjasiriamali mkubwa, Mjuaji wa Mambo mengi nchini Tanzania, Member Mkongwe JamiiForums, Mwanasiasa mwenye Mafanikio na Mtu mwenye Network kubwa sana ya Viongozi ( Watawala ) wa Tanzania hii na huenda hata katika Teuzi zijazo za DC au DED safari hii akawemo.
 
Mtanisamehe labda uelewa wangu ni mdogo.

Nilichoelewa kwamba CHADEMA kama chama cha siasa basi kipo chini ya msimamizi wa vyama vya siasa ambaye amepewa mamlaka ya kuweza kushugulikia matatizo yote ya vyama vya siasa na hata kukifuta chama.

Hoja yangu ni kwamba kama CHADEMA wanakiuka Katiba yao je huyo msimamizi wa vyama vya kisiasa alichukua au amechukua hatua gani mpaka leo hii.

Kushindwa kwa msajili wa vyama vya kisiasa kuwachukulia hatua CHADEMA inaonyesha wazi kuwa Katiba yetu ya nchi ambayo imempa mamlaka msajili kusimamia vyama vya siasa haipo sawa inaitaji marekebisho Mana hakuna mtu au chama chochote ambacho kipo juu ya Katiba.

Pili, hauwezi kufananisha Katiba ya nchi na Katiba ya chama, Yani ni kusema kwamba kwa vile Katiba ya CHADEMA haijafika basi katiba ya nchi hisibadilishe, au udhaifu wa Katiba ya CHADEMA madhara yake ni kwa wanachama wake ila udhaifu wa Katiba ya nchi madhara yake ni kwa wananchi wote.

Nahisi kuwa hapo hoja ya uyo bro ilibidi iwe je tunaitaji mabadiliko ya Katiba au la. Na sio kutumia madhaifu ya chama kuficha hoja ya msingi.
 
Hivi hii Katiba Mpya tunayodai ni ile ya Maoni ya Warioba au ile iliyochakachuliwa ya Sitta au tunaanza moja?

Sababu upya sio necessarily uzuri, na kwa watanzania niwajuavyo hapo tutakuta vitu wananchi watakavyopigania sana ni mambo ya Imani.
 
Yuko sahihi sana....

Paschal Mayalla AMENENA UKWELI.....

Chadema wana MAPUNGUFU mengi....

1)Mosi ,nafasi ya UENYEKITI ni ya "kifalme" sijui huko nyuma ya "mapazia" imeelekezwa KURITHISHWA?!!!!
Hili ni tatizo kubwa....si DOGO HATA.....

2)Pili ,kwa kuwa nafasi ya MWENYEKITI imeng'ang'aniwa......basi mwenyekiti ANAROPOKA atakavyo....mathalani juzi amenukuliwa akisema kuwa inabidi wasitegemee KUPEWA FEDHA ZA RUZUKU katika kujiendesha....ajabu kubwa hii.....WALIMPINGA SANA HAYATI MAGUFULI PALE ALIPOSEMA KUWA TUPUNGUZE KUOMBAOMBA NJE YA NCHI...."
(Huu ni ukigeugeu wa kinafiki).

3)Mapato matumizi na mishahara ndani ya CHADEMA imekuwa ni kizungumkuti......

Hivi kweli inapita MIEZI 6 HUJALIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI WAKO KWA KIGEZO TU CHA KUTOPEWA RUZUKU ?!!!

Yaani CHAMA kikuu Cha upinzani chenye uzoefu wa MIAKA ZAIDI YA 20 kweli kinakosa KUWEKEZA katika biashara zitakazowazungushia fedha ili angalau ziwe ni vyanzo vya mishahara kwa WATUMISHI wao wachache?!!!!!

🤣🤣🤣🤣🤣

*************************

PASCAL MAYALLA yuko sahihi sana.......
 
" Ili CHADEMA tuwaamini kuwa AGENDA yao ya Kudai Katiba Mpya ina Mashiko na wana Hoja ya Msingi hebu wao kama Chama waanze Kwanza kuonyesha kuwa wanaheshimu Katiba ndani ya Chama chao ambapo kuna uvunjifu mkubwa tu wa Katiba " Pascal Mayalla

Nukuu hii nimeitoa baada ya Kumsikia na Kumtizama jana Usiku Star Tv akiwa Mgeni rasmi kwa Dar es Salaam katika Kipindi kilichokuwa Kinasimamiwa na Mtozi Aloyce Nyanda.
Mkuu Krav Maga, kwanza asante kwa hoja hii.
Hoja iliyokuwa mezani jana ni hitaji la Katiba mpya, jee tumshinikize Mama Samia, lazima utupe katiba mpya au tumpe muda zaidi.

Hoja zangu ni hitaji la katiba mpya ni hitaji genuine, tena nikasema katiba mpya Tanzania sio kuwa inahitajika leo, katiba mpya ilihitajika toka juzi, jana na leo. Nikasema, kwa miaka 30, Tanzania imekuwa chini ya mfumo wa chama kimoja, na katiba iliyopo ya mwaka 1977, ni katiba ya chama kimoja, hivyo tulipoanzisha mfumo wa vyama vingi, tulipaswa tubadili katiba na kuwa na katiba ya vyama vingi. Kilichofanyika ni katiba ile ile ya chama kimoja, ikaongezewa kiraka cha vyama vingi, lakini mfumo ni ule ule wa chama kimoja, hivyo bila mabadiliko ya katiba, CCM itatawala Tanzania milele.

Suala la Katiba lililetwa kwa hisani tuu ya uungwana wa JK, halikuwemo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM.

Nikaishauri Chadema, badala ya kususa na kupiga kelele tuu, wajifunze tabia ya kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kudai haki zao, na kwa kuanzia, charity begins at home, kwa Chadema kuanza kufuata katiba yake katika timua timua za wanachama wao.

Kwa msiofahamu utaratibu wa Chadema kutimua wanachama wake, karibuni mitaa hii

Baada ya Chadema kufuata katiba yao ndipo watu organize Watanzania kudai katiba mpya. Nikawasisitiza, kwa vile hoja ya katiba ilikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi ya 2015- 2020, lakini very unfortunately katiba haikuwa ni kipaumbele cha JPM na hawakumshinikiza JPM, na sasa hoja ya katiba mpya haipo tena kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025, then wasimshinikize Samia kuendelea na mchakato, bali wajenge hoja zenye mashiko, halafu Samia akiingia huruma na kufanya uungwana kama wa Kikwete, ndipo Tanzania itapata katiba mpya.

Kitendo cha Chadema kususa, sio tuu ni wastage of time, but Chadema is bed ridden on its deathbed, if it won't change its strategies, it is going to die and soon it will be 6ft under!.

P
 
Ya Warioba mkuu
Kwahio ile Kamati iliyokaa Bungeni na kurekebisha mambo / kubadilisha na Samia mwenyewe akiwemo unadhani itarudiwa ? Unadhani hapa kuna Serikali Tatu hapa ?

Are we Serious ?, Unadhani wakikaa tena Bungeni ili kusahihisha mambo yatakuwa tofauti na ya Sitta ?, Unadhani wananchi wapo informed watakubali kwamba hii huku tunayosema huku mtaani ni nzuri na propaganda za Bungeni ni uongo ? Unadhani Viongozi wa Imani zao wakipewa hiki au kile hata kama mengine yote ni mabaya wataacha kuunga mkono ?

In short what has changed between then and now ? Bila mwananchi kuwa informed chochote kitakachopikwa atakila hususan kikichanganywa na propaganda.... Katiba Mpya itakuwa kweli Mpya / Nzuri au Upya utakuwa kwenye Chapisho
 
Sorry nachoelewa ni kwamba CHADEMA,,,CCM,,,ACT au vyama vyote vya siasa vitapita lakini TANZANIA itabaki milele. Ivyo au ni kwamba Katiba mpya ni kwa manufaa ya chadema au nchi nzima.
Ni kama nchi nzima basi hayo madhaifu ya chadema hayana mantiki Katika Katiba mpya.
Chadema kuvunja Katiba yao tumuachie msajili wa vyama,,yeye ndio anapaswa achukue hatua.
 
Umenena vyema, Paschal wakati anauliza issue ya katiba pale ikulu alikuwa hajui kama katiba ya CHADEMA ina mapungufu? ukimtoa Dotto Buledu hakuna mwandishi mwingine Tanzania wengine wote ni wasaka tonge.
Mkuu Babati, mimi nimeizungumzia sana katiba ya Chadema, angalia tarehe za mabandiko haya


P
 
Paschal unafeli sn kwahiyo katiba mpya iwe ni huruma ya Samia na siyo hitaji la watanzania? kwa namna hii bora uachane na uchambuzi wako maanake unajivunjia heshima sn
 
Back
Top Bottom