Ni matatizo gani ya Kijamii wanayoyapata wananchi Mkoani au Wilayani mwako?

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,619
1,710
Ndugu Wanabodi,
Kwa kuwa Jamiiforums ni mtandao unaosomwa na watu wengi kuanzia Vijana, Watu wazima, paomoja na Wazee bila kuwasahau Viongozi wa siasa pamoja Kiroho.

Kupitia uzi huu ningeomba tuhainishe matatizo wanayoyopata Wananchi wa kipato cha chini hasa vijijini, changamoto wanazozuipata. Huduma gani za muhimu zinakosekana ambazo huenda hata huko Bungeni hawajaziongelea au wameziongelea lakini hazijapata suluhisho.
Hili linawezakuwa Bunge nje ya Ukumbi wa Bunge.

Mimi nitoe baadhi ya changamoto zilizopo Mkoani Kagera.
  1. Mkoani Kagera Kuna changamoto nyingi, lakini kubwa ni kushuka kwa bei ya kahawa na ugonjwa wa migomba kukauka (Mnyauko). Kuna juhudi zinafanywa na Kituo cha utafiti wa kilimo cha Maluku lakini bado hakijatoa jibu sahihi.
  2. Changamoto ya maji hasa Wilaya ya Misenyi na Karagwe, ili limekuwa tatizo sugu hasa wakati wa Kiangazi.
Zipo changamoto nyingi lakini hizi ni baadhi, vipi Mkoani/Wilayani kwako?
 
Back
Top Bottom